Ipi top 3 yako ya nyama tamu?

Ipi top 3 yako ya nyama tamu?

Hapo kwenye kuku tupo pamoja
Namba 2 ni kitimoto then cow

Ila nyie kuku ni mtamu asee
Kuku hawalingani ladha.
Ukitaka kustaajabia ladha ya nyama tamu ya kuku, kula broiller aliyekomaa wa miezi 6 ama 8.
Nilikuwaga mbishi kwa kuwa mlaji wa broiller pre mature za mwezi mmoja mmoja ambao test yao haisomeki sawa sawa mdomoni.

Sasa nilipoletewa "gift" ya broiller aliyepea, mkubwa nyama yake kg4, kuja kumla, dah!
 
Salam!

Wale wazee wa misosi ipi top 3 yako ya nyama tamu. Ya kwangu hii hapa:

1. Kuku
Asee huyu ndege hadi leo binafsi naona nyama yake haina mpinzani yani hana mbadala yani nyama iwe mchemsho rosti choma au ya kukaanga nitamu zote nadhani sote tunafahamu jinsi supu ya kuku ilivyo tamu

2. Ng'ombe
Akitoka kuku anafata ng'ombe huyu myama nae yupo vizuri lakini huyu utamu wa nyama yake una depend na maufundi ya mpishi. laini na yeye nyama yake iwe mchemsho rosti choma au ya kukaanga nitamu zote

3 Kitimoto
kwangu huyu namba yake inashika namba 3 kwasababu tu nyama yake inanoga tu kwa rosti na kukaanga lakini mchemsho wake hahaha hapana asee

hiyo ndo top 3 yangu ya nyama tamu Je, ya kwako ni ipi?

NB: Kuku anautamu wa asili tu yeye haitaji ata ufundi wa mpishi.
Ngiri wa kukausha, sungura mwitu na digidigi.
Nyama zao ni tamu sana na ni laini kutafuna.
 
1. Samaki sato wa limao asiungwe

2. Kondoo vyovyote vile

3. Kitimoto we acha tu

4. Kuku anasa
 
Kuna watu hawajala nyama pori
1)Kware
2)Digidigi
3)Ndo huyu kuku wenu anafuata
 
Kitimoto imepita bila kupingwa. Mungu anatupenda Sana kutupa mnyama mtamu.
 
Sijaona watu wakiandika ile aliyosema Hayati Mwl. J. K. Nyerere kuwa ukiila huwezi kuiacha
 
Kuna siku kiboko kafariki huku kwetu,nasikia alipigwa na ndugu zake wakimfukuza kwenye ukoo,ile nyama tuliigawana karibia kijiji kizima na vitongoji vyake kama 10 na zaidi,kwenye familia yangu tulichelewa kuipata hii nyama tulipewa kidogo tu lakin cha kushangaza ikipikwa inaongezeka ni tamu balaa tuliitumia karibia siku tatu na list yangu itakuwa hivi
1.Nyama ya kiboko
2.kuku
3.Ng'ombe ikipata fundi unaweza hisi ina sukari
Kwenye kiboko umeleta stori za kusadikika usitudanganye kama hvo ww kiboko mkubwa ana kilo 800 mpka tani moja sasa vitongoji 10 na zaidi kijiji kina watu wa ngapi na walipata kilo ngapi ngapi.

Ikumbukwe kuwa wanaopigana na kufukuzana kwenye eneo ni madume wanaokua kugombania sehemu ya kupanda majike sasa huyo dume kwa makadirio anakuwa na kg800 wale waliokomaa kabisa ndo wanasogea mpka 1tn hebu weka stor yako sawa isje ikawa chai ya maziwa mgando

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom