Ipo haja ya Hotuba ya Rais kabla ya kufunga mwaka 2020

Ipo haja ya Hotuba ya Rais kabla ya kufunga mwaka 2020

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Heri ya Sikukuu ya Krismasi ndugu zangu?

Naona ipo haja ya kuwa na hotuba ya Rais kwa Taifa kabla ya kufunga mwaka 2020.

Hata akitoa Salamu za Mwaka Mpya nayo sio mbaya.

Hii itamuwezesha kufanya mambo makubwa mawili;

1. Kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kwa awamu ya pili ( najua ameshafanya hili wakati wa ufunguzi wa Bunge lakini sio mbaya akifanya tena).

2. Kutoa muelekeo wa Serikali yake kwa mwaka 2021 katika mambo mbali mbali ikiwemo Uchumi, elimu, afya , ajira kwa vijana na mambo mengineyo.

Naamini wasaidizi wake watamkumbusha hili.

Baada ya kusema hayo machache.

Niwatakieni tena Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya.
 
Namba 2. Alisha toa muelekeo alipokuwa bungeni. Na hasa hasa alipokuwa akipita huko kkwenye kampeni nileteeni naniliiiiiii nireteeeeni naniliiiiiiii
Hiyo itakua ni muelekeo wa mhula wake wote (5 years).

Sasa tunasubiri kusikia kwa mwakani serikali imepanga kutufanyia nini sisi wananchi.

Sio vibaya tukafahamu na tukaulizana maendeleo yake.
 
Heri ya Sikukuu ya Krismasi ndugu zangu??

Naona ipo haja ya kuwa na hotuba ya Rais kwa Taifa kabla ya kufunga mwaka 2020....
Hana Jipya.

Yeye asubirie tu muda wake uishe asepe.

Kama atakatalia madarakani tujue la kufanya.

Hakuna Mtanzania mwenye matumaini naye tena, wengi wameamua kusubiria amalize asepe. Na siku hazigandi
 
Wezi wako wengi lakini hukumu za wezi wengine hutolewa na Mungu.
Pole Sana kwa kuibiwa mkuu ila hujasema umeibiwa nini.

Hivi muda wa kukata rufaa kwa wale wabunge 19 si umeshapita??

Ngoja tusubiri sarakasi zenu maana sioni namna hao 19 wataondoka Bungeni, Chama kitawasamehe tu na maisha yataendelea, sema kinachotafutwa hapa ni timing tu ya kufanyika hilo.
 
Binafsi suala la CHADEMA na wabunge 19 naona ni issue ndogo sana, SUALA KUBWA na lisilopewa kipaumbele ni KWANINI NEC walifoji Majina na kupeleka bungeni kinyume na sheria na taratibu zilizopo kama taifa ???
 
Mkuu inaelekea una ushahidi kuwa NEC imefoji majina maana sioni uhalisia wa hili wakati wahusika wamekwenda wenyewe bungeni na kuapa??
 
Mkuu inaelekea una ushahidi kuwa NEC imefoji majina maana sioni uhalisia wa hili wakati wahusika wamekwenda wenyewe bungeni na kuapa??
CHADEMA kupitia katibu mkuu wao wamekiri hawajapeleka majina na form za NEC Mnyika anazo mpaka leo, sasa hayo majina ya wabunge 19 yalipatikana vipi na kwa taratibu zipi?

Unaposema walijipeleka wenyewe kuapa, probably YES lakini Je, huo ndio utaratibu wa upatikanaji wa wabunge wa viti maalumu tuliojiwekea kama taifa?
 
CHADEMA kupitia katibu mkuu wao wamekiri hawajapeleka majina na form za NEC Mnyika anazo mpaka leo, sasa hayo majina ya wabunge 19 yalipatikana vipi na kwa taratibu zipi ??

Unaposema walinipeleka wenyewe kuapa, probably YES lakini Je, huo ndio utaratibu wa upatikanaji wa wabunge wa viti maalumu tulioniwekea kama taifa ?
Wahusika watueleze wenyewe walifikaje bungeni na kiongozi wao anadai walikua na baraka za chama.
 
Heri ya Sikukuu ya Krismasi ndugu zangu??

Naona ipo haja ya kuwa na hotuba ya Rais kwa Taifa kabla ya kufunga mwaka 2020..
Wewe unataka aongee nini zaidi ya habari ya manunuzi ya ndege, SGR, Bwawa la Stiegliers, kununua Meli, Mikopo ya Wanafunzi, Elimu bure, ujenzi wa vituo vipya vya Afya, makusanyo ya TRA nk, such things like that etc, ambavyo tumezoea kusikia, hakuna jipya. lakini uchumi wa mtu "the public economy" is dead na hili hatoweza kulisema.
 
Back
Top Bottom