Uchaguzi 2020 Ipo mifano hai kuwa Lissu atashinda Urais 2020, CCM tusijipe matumaini nawaambieni


Mkuu - wakati wa WaTanzania kuchagua watu kwa "MANENO" umepita. Watanzania wa sasa wanataka vitendo. Hao unaowasema walikuwa ni watanzania wakati nchi ikiwa bado Masikini. Sasa hivi nchi iko uchumi wa kati. Watanzania wanataka "MATENDO"; sio maneno waliyokuwa wanaambiwa tangu nchi hii inapata uhuru. Huo muda umeshapita. Lissu hana "TRACK RECORD" yoyote kwa Tanzania. Hata huko kwenye jimbo lake, hana chochote alichofanya mpaka sasa. Ingawa ameshika ubunge kwa muda mrefu.
 
Paka akishindana na Chui, aliyechanganyikiwa atapasa sauti bila aibu "eti " paka atashinda.
 
Nina mashaka sana na hii tume ya uchaguzi. Wajumbe wote ni kada wa CCM, tena wakisaidiwa na polisi na mahakama wakiwa pamoja na msajiri wa vyama. Je, wapinzani watapenya kweli? Itakuwa miujiza kama alivyopona TAL. Tusubiri kuona!!!!
 
Utoto ndiyo tatizo lako, eti mfano hai Lissu atashinda, ni nini hiyo, una maana gani? Kama Lissu akishinda ina maana watanzania wengi ni wajinga.
 
Tundu lisu atashinda tu urais Kwanza kabisa sera zake kubwa kurudisha wafanyakazi kazini wote waliofukuzwa kazi kwa kisingizio Cha vyeti fake tofauti kabisa kwa mujibu was Sheria yetu ya nchi wafanyakazi wale walilazimika kutumia vyet hivyo kutokana na sera mbovu za ccm katiba ya nchi inasema mtu yeyote mwenye kujua kusoma na kuandika anahaki ya kufanyakazi au kuajiliwa mahara popote sera mbovu za ccm wanakuja kubadili sera hii wakati watu wanajua katiba haisemi hivyo nikosa kubwa Sana wamefanya wangebadilisha Kwanza katiba ndipo utaratibu mungine ungefanyika leo hii watu waliofukuzwa wanateseka mitaani na hii yote ilikuwa ili wanyonge watoke na watoto wa matajiri waingie
 
Chadema bado ni wanaharakati siku mkiwa wanasiasa tutawapa nchi ila kwasasa tunachama kimoja makini nacho ni ccm na Magufuri ndio baba lao
2020 wananchi twende tukawaanyooshe hawa wanaharakati wanaopenda.shali kuliko maendeleo ya wananchi.

Lumumba kweli mnatisha!! Hata jina la mwenyekiti wenu hamlijui ? Magufuri ni nani au ulikuwa na maana ya Magufuli.
 
Me nashauri mkawahoji kwanza wananchi haswa huko vijijini then ndio mje na mahandiko kama haya.
Wengi hawana simatifoni mabandiko kama haya hawayapati.
 
Kitu kimoja CCM hawashtuki, kwa miaka hii yote ya magufuli ni wao tu walikua wanapiga kampeni, hakuna mpinzani aliyekua anajinadi wala kunadi chama chake. Hali iliyopo sasa hvi mnayojidanganya kwamba mnakubalika sana ni sababu tu watanzania hawajasikia chochote kutoka upande wa pili zaidi ya kusikia propaganda za CCM ambazo hazini maajabu yoyote ni zile zile za miaka yote barabara maji umeme n.k

Sasa kampeni zinafunguliwa wapinzani wataanza kuongea na watanzania msitegemee hali itabaki hvi ilivo. Mbaya zaidi ni Lisu ndo atakaekua anaongea huyu jamaa n next level, naamini ndani ya muda mchache wa kampeni wananchi wataenda kufumbuliwa macho na kuelewa ukweli wa mambo nin chanzo cha machungu na mateso wanayopitia tangu kuanza kwa awamu hii.

Vote for Tundu A. Lisu
 
LISU hashindi.
Mshindi hutangawa na tume ya taifa ya uchaguzi.

Hawawezi kumuacha aliyewateua wamtangaze Lisu.

Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
 
LISU hashindi.
Mshindi hutangawa na tume ya taifa ya uchaguzi.

Hawawezi kumuacha aliyewateua wamtangaze Lisu.

Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
Wakimtangaza Lisu atawafanya Nini ? wakati huo yeye atakua kashindwa?
Lissu Sasa atakua keshakua Rais
Kauli ile iliwahusu wabunge na madiwani na serikali za mitaa hasa chaguzi za marudio.
 
π™°πšœπšŠπš•πšŠπšŠπš– π™°πš•πš’πšŽπš”πšžπš–
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…