Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu naweza nisieleweke haya maneno kwa Sasa kutokana na muda kuwa haujafika, nimeona niyaseme haya ili ibaki katika kumbukumbu, CHADEMA lazima wafahamu kuwa katika mazingira na siaza za kiafrika Ni ngumu Sana kumpata Rais aina ya Rais Samia, viongozi aina yake hupatikana katika nchi chache na hutokea kwa nadra na ndani ya muda mrefu.
Kupata kiongozi aina ya Rais Samia anayeweza kukaa meza moja na mpinzani wake mkuu kusikiliza madai yake, mapendekezo Yake, kero Yake, malalamiko Yake, dukuduku lake,maumivu yake,majeraha Yake na maoni yake Ni wachache Sana. Kwa kuwa wengi wa viongozi wa kiafrika huona Kama hawahitaji ushauri Wala kushauriana na yeyote kutoka upinzani Wala kupokea mawazo mapya kutoka upinzani na kuyafanyia maboresho.
Wengi huona upinzani ni uadui kutokana na Tabia ya upinzani kukosa lugha za busara,hekima,uvumilivu na Subira katika ukosoaji wao,hivyo watawala hujihami kwa kuendesha nchi kwa mkono wa mamlaka kamili yasiyohitaji kupunguzwa kwa yoyote na kwa lolote kupitia maridhiano, Wengi huamua kuzungumza kwa matendo.
Rais Samia Ni mama na kiongozi anayeamini kuwa sote tunaweza kujenga nchi yetu bila kujari itikadi zetu za kisiasa, anaamini kuwa Tanzania inaweza kujengwa na sote bila kuumizana Wala kujeruhiana, anaamini tunaweza tukasimama pamoja Kama Taifa katika shida hata Kama tunatofautiana kisiasa, Anaamini tunaweza kukosoana bila kuvunjiana heshima, kutukanana, kubezaba, kukomoana, kuombeana dua mbaya,kulipiziana ,kuviziana,kushikiana mapanga,kurushiana mawe,au hata kutangaziana vita hadharani.
Rais Samia anaamini tunaweza tukaishi Kama watani wa jadi katika mpira ,anaamini tunaweza kutofautiana kisiasa lakini tukaweza kushirikiana katika shughuli za kijamii Kama vile misiba ,harusi,vipaimara na aina yoyote ya shughuli ya kijamii kwa kushikamana na kushirikiana vizuri.
CHADEMA lazima wafahamu kuwa katika mazingira ya kiafrika na siasa zake unaweza ukawa na katiba mpya nzuri na Bora katika Bara la Afrika lakini nchi ikaendeshwa ni Kama kumetangazwa Hali ya hatari, Ikumbukwe kuwa wasimamizi wa katiba Ni sisi wenyewe tunaofahamiana Tabia zetu
Inasikitisha Sana unapoona viongozi Hadi wanachama wa chadema wanapoongozwa na kutawaliwa na matusi, kejeri,dharau,kiburi,lugha za kudhalilishana na maneno yasiyo na staha kwa mamlaka, Chadema Ni watu wasio na Subira Wala uvumilivu,hawana kusema tupate hili kwanza tungoja lile au tufanikiwe hili halafu tutaanza na lile, Ni watu wa kukurupuka kimaneno ,mihemuko,jazba, utoto mwingi na watu wanaoonyesha kukosa ukomavu wa kisiasa. Hawafahamu kuwa huwezi ukapata yote kwa wakati mmoja, hawajuwi kuwa Kuna wakati unatakiwa upunguze ujazo wa matarajio yako na mahitaji yako. Wao chadema wanajuwa Ni lazima upate kila kitu kwa wakati mmoja utafikiri wao ndio watawala.
CHADEMA lazima wajifunze kuwa na Subira, kuwa na uvumilivu. Wajuwe Ni Nani awe msemaji wao katika masuala ya msingi, wajuwe Nani anapaswa kwenda kwenye meza ya mazungumzo, wasiendeshwe na mihemuko ya vijana wao, wawe viongozi wa kuwaongoza vijana wao na kuwapa muelekeo sahihi,tofauti na Sasa Haieleweki Nani Ni msemaji wa chama Wala Nani Ni katibu wa chama, wala nani ni Mwenyekiti wa vijana,Haieleweki upi Ni msimamo wa chama kwa kuwa kila mtu anakuwa na msimamo wake katika Ukurasa wake na kila mtu anaona yeye ndiye chama na ndiye anapaswa asikilizwe na wote.
CHADEMA kwa Sasa kimekosa dira na muelekeo kwa kuwa kimekosa mtendaji wa kukiongoza vizuri,ndio unaona kila mtu akitoa matamko yake atakavyo na ajisikiavyo. Naiona chadema ikishindwa kutoka katika shimo ililoangukia kutokana na kutokumuoa mtu wa kuitoa shimoni
Rais Samia lazima Aheshimiwe na akosolewe kwa lugha za heshima,busara na staha, Mama Samia Ni Rais na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Na Urais Ni Taasisi kubwa Sana ambayo huwezi ukaitikisa Wala kuidhalilisha kwa namna yoyote Ile,huwezi ukaichafua Wala kuipaka matope, huwezi ukaandika maneno yako machafu Kama mlevi, Rais Samia lazima Aheshimiwe na kila mtanzania, Mama Samia Ndio Nembo yetu Ya Taifa, Ndio Taifa Lenyewe, Ndio Amani Yenyewe, Ndio mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vyote tunavyovijuwa na tusivyoviona.
Kazi iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.