Ipo siku CHADEMA watamkumbuka Rais Samia na kuelewa dhamira yake ya kuwatumikia Watanzania kwa uzalendo na upendo

Ndo maana ndugu YANGU nikasema ACHA ajivute vute kufika 2025 na kupumzika na chama chenu ,akumbukwe KWa machache ,uchaguzi ukifanyika. Hakuna jipya ndugu, ila wanaccm wachache waona Kuna jipya KWa maana ya wanafulsa ya upigaji, hakuna Cha Ziada anatenda ,
Mama Samia Hazuiliiki katika uchaguzi ujao, Mama Samia Ni Kama maji Usipoyanywa utayaoga tu
 
Aya bwana ,Kati ya SSH NA MUNGU nani mkubwa? Kati ya Serikali ya ccm na Mungu nani mkubwa?

Kati ya vyombo vya Dola na Mungu nani mkubwa?

Kati ya wafuasi wa ccm na Mungu nani mkubwa?

Jiandae dholuba kali chini ya jua inakuja juu ya ccm , sio mwanadam yeyote ataweza izuia , nasema hili KWa ujasili mkubwa Sasa maana najua wapi natoa huu ujasili, umeelewa Lucas , wambie Hali ilivyo viongozi wako na WENDA ukabarikiwa , thanks
 
Napendekeza huyu mleta uzi huu apewe kazi huko Ikulu hata ya kufanya usafi vyooni ingalau tupumzike na utopolo wake wa kusifu na kumuabudu chifu Hangaya. Hana kiasi naona hata watoto wa kuzaa wa Mama Samia hawawezi kufikia hatua aliyofikia huyu kiroboto.
Majitu mengine hayakustahili kuwepo Tanzania
 
Chadema? [emoji28][emoji28].How in hell have you managed to get them into this conversation.. Jamiiforums imekua ze komedi siku hizi..
Usiilaumu jf,laumu members wa jf ambao akili zao zimeshikwa na kutu ya njaa kama mleta mada.
 
We nae na maandiko yako duh, mbona unaongea mambo ambayo sio ishu Kwa sasa tanzania?

Ongea mambo ya maji, umeme, vitu kupanda bei,

Leo hakuna tena bando la 1Gb Kwa elf 2000,

Ukiongea hizi ishu ndio unaweza kupata teuzi na sio unalia lia Tu chadema chadema

Hao chadema Wana nn now hawana nguvu tena, hawana ela, hawana mikutano, wapo Tu kama kijiweni

Ongea mambo ambayo kila mtu yanamgusa,
Kwao hao machawa bila kuitaja cdm hawapewi posho
 
Ndugu zangu naweza nisieleweke haya maneno kwa Sasa kutokana na muda kuwa haujafika, nimeona niyaseme haya ili ibaki katika kumbukumbu, CHADEMA lazima wafahamu kuwa katika mazingira na siaza za kiafrika Ni ngumu Sana kumpata Rais aina ya Rais Samia, viongozi aina yake hupatikana katika nchi chache na hutokea kwa nadra na ndani ya muda mrefu.

Kupata kiongozi aina ya Rais Samia anayeweza kukaa meza moja na mpinzani wake mkuu kusikiliza madai yake, mapendekezo Yake, kero Yake, malalamiko Yake, dukuduku lake,maumivu yake,majeraha Yake na maoni yake Ni wachache Sana. Kwa kuwa wengi wa viongozi wa kiafrika huona Kama hawahitaji ushauri Wala kushauriana na yeyote kutoka upinzani Wala kupokea mawazo mapya kutoka upinzani na kuyafanyia maboresho.

Wengi huona upinzani ni uadui kutokana na Tabia ya upinzani kukosa lugha za busara,hekima,uvumilivu na Subira katika ukosoaji wao,hivyo watawala hujihami kwa kuendesha nchi kwa mkono wa mamlaka kamili yasiyohitaji kupunguzwa kwa yoyote na kwa lolote kupitia maridhiano, Wengi huamua kuzungumza kwa matendo.

Rais Samia Ni mama na kiongozi anayeamini kuwa sote tunaweza kujenga nchi yetu bila kujari itikadi zetu za kisiasa, anaamini kuwa Tanzania inaweza kujengwa na sote bila kuumizana Wala kujeruhiana, anaamini tunaweza tukasimama pamoja Kama Taifa katika shida hata Kama tunatofautiana kisiasa, Anaamini tunaweza kukosoana bila kuvunjiana heshima, kutukanana, kubezaba, kukomoana, kuombeana dua mbaya,kulipiziana ,kuviziana,kushikiana mapanga,kurushiana mawe,au hata kutangaziana vita hadharani.

Rais Samia anaamini tunaweza tukaishi Kama watani wa jadi katika mpira ,anaamini tunaweza kutofautiana kisiasa lakini tukaweza kushirikiana katika shughuli za kijamii Kama vile misiba ,harusi,vipaimara na aina yoyote ya shughuli ya kijamii kwa kushikamana na kushirikiana vizuri.

CHADEMA lazima wafahamu kuwa katika mazingira ya kiafrika na siasa zake unaweza ukawa na katiba mpya nzuri na Bora katika Bara la Afrika lakini nchi ikaendeshwa ni Kama kumetangazwa Hali ya hatari, Ikumbukwe kuwa wasimamizi wa katiba Ni sisi wenyewe tunaofahamiana Tabia zetu

Inasikitisha Sana unapoona viongozi Hadi wanachama wa chadema wanapoongozwa na kutawaliwa na matusi, kejeri,dharau,kiburi,lugha za kudhalilishana na maneno yasiyo na staha kwa mamlaka, Chadema Ni watu wasio na Subira Wala uvumilivu,hawana kusema tupate hili kwanza tungoja lile au tufanikiwe hili halafu tutaanza na lile, Ni watu wa kukurupuka kimaneno ,mihemuko,jazba, utoto mwingi na watu wanaoonyesha kukosa ukomavu wa kisiasa. Hawafahamu kuwa huwezi ukapata yote kwa wakati mmoja, hawajuwi kuwa Kuna wakati unatakiwa upunguze ujazo wa matarajio yako na mahitaji yako. Wao chadema wanajuwa Ni lazima upate kila kitu kwa wakati mmoja utafikiri wao ndio watawala.

CHADEMA lazima wajifunze kuwa na Subira, kuwa na uvumilivu. Wajuwe Ni Nani awe msemaji wao katika masuala ya msingi, wajuwe Nani anapaswa kwenda kwenye meza ya mazungumzo, wasiendeshwe na mihemuko ya vijana wao, wawe viongozi wa kuwaongoza vijana wao na kuwapa muelekeo sahihi,tofauti na Sasa Haieleweki Nani Ni msemaji wa chama Wala Nani Ni katibu wa chama, wala nani ni Mwenyekiti wa vijana,Haieleweki upi Ni msimamo wa chama kwa kuwa kila mtu anakuwa na msimamo wake katika Ukurasa wake na kila mtu anaona yeye ndiye chama na ndiye anapaswa asikilizwe na wote.

CHADEMA kwa Sasa kimekosa dira na muelekeo kwa kuwa kimekosa mtendaji wa kukiongoza vizuri,ndio unaona kila mtu akitoa matamko yake atakavyo na ajisikiavyo. Naiona chadema ikishindwa kutoka katika shimo ililoangukia kutokana na kutokumuoa mtu wa kuitoa shimoni

Rais Samia lazima Aheshimiwe na akosolewe kwa lugha za heshima,busara na staha, Mama Samia Ni Rais na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Na Urais Ni Taasisi kubwa Sana ambayo huwezi ukaitikisa Wala kuidhalilisha kwa namna yoyote Ile,huwezi ukaichafua Wala kuipaka matope, huwezi ukaandika maneno yako machafu Kama mlevi, Rais Samia lazima Aheshimiwe na kila mtanzania, Mama Samia Ndio Nembo yetu Ya Taifa, Ndio Taifa Lenyewe, Ndio Amani Yenyewe, Ndio mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vyote tunavyovijuwa na tusivyoviona.

Kazi iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Jamaa unaandikaga maandishi mengi ila pointi moja.Badilika.
 
unaandika bila utafiti wowote kisa umeandika? my friend labda ukawadanganye huko simiyu
jana nilikuhoji maswali ya kitafiti nikaona umekimbia...... nikajua ni zao la shule zetu/vyuo vyetu vya kata
Tangu lini waramba miguu wakawa na majibu kwenye mambo ya msingi?
 
CHADEMA inakuumiza sana eeeh?
KashaurI kale kachama kenu mlikokapa ofisi Zanzibar,waache CHADEMA wapunzike mmewatesa sana.
MAISHA YALIVYO HIVI,SIJUI MTASEMA NINI 2025....Yaani tutawapiga kipigo kitakatifu,siyo Polisi wala tumr itawaokoa.
KIPIGO ZAIDI YA KILE LOWASA ALIMPIGA JIWE 2015.
Ujumbe mzuri sana hasa kwa hao waramba miguu
 
Mama yetu mpendwa mama Samia anataka watanzania wote tushiriki katika ujenzi wa Taifa letu,Hataki kuona mtu yoyote anabaki nyuma Wala kuachwa nyuma, anataka wote tujivunie Taifa letu na tujione Fahari kuzaliwa Tanzania
Yani tuone fahari kulala giza, maji hakuna, kubebeshwa mizigo ya tozo zisizo na idadi na kupanda kwa gharama za maisha mara dufu hivi ni vyva kuona fahari au kutumika kumwondoa madarakani mara moja?
 
Rais Samia kafanya mambo mengi na makubwa Sana Tena ndani ya kipindi kifupi Sana, Rais Samia kafanikiwa kwa kiasi kikubwa kukata kiu ya watanzania waliyokuwa wanahitaji ya ujenzi wa uchumi unaomgusa mtanzania mnyonge, Rais Samia anatekeleza miradi na kuelekeza pesa katika miradi na maeneo tanayogusa maisha ya watanzania, hii ndio sababu ya Kuendelea kukubalika Kwake na kuona Tanzania ikiwa Tulivu na yenye Amani
Punguza ushamba wewe chawa
 
Ndugu zangu naweza nisieleweke haya maneno kwa Sasa kutokana na muda kuwa haujafika, nimeona niyaseme haya ili ibaki katika kumbukumbu, CHADEMA lazima wafahamu kuwa katika mazingira na siaza za kiafrika Ni ngumu Sana kumpata Rais aina ya Rais Samia, viongozi aina yake hupatikana katika nchi chache na hutokea kwa nadra na ndani ya muda mrefu.

Kupata kiongozi aina ya Rais Samia anayeweza kukaa meza moja na mpinzani wake mkuu kusikiliza madai yake, mapendekezo Yake, kero Yake, malalamiko Yake, dukuduku lake,maumivu yake,majeraha Yake na maoni yake Ni wachache Sana. Kwa kuwa wengi wa viongozi wa kiafrika huona Kama hawahitaji ushauri Wala kushauriana na yeyote kutoka upinzani Wala kupokea mawazo mapya kutoka upinzani na kuyafanyia maboresho.

Wengi huona upinzani ni uadui kutokana na Tabia ya upinzani kukosa lugha za busara,hekima,uvumilivu na Subira katika ukosoaji wao,hivyo watawala hujihami kwa kuendesha nchi kwa mkono wa mamlaka kamili yasiyohitaji kupunguzwa kwa yoyote na kwa lolote kupitia maridhiano, Wengi huamua kuzungumza kwa matendo.

Rais Samia Ni mama na kiongozi anayeamini kuwa sote tunaweza kujenga nchi yetu bila kujari itikadi zetu za kisiasa, anaamini kuwa Tanzania inaweza kujengwa na sote bila kuumizana Wala kujeruhiana, anaamini tunaweza tukasimama pamoja Kama Taifa katika shida hata Kama tunatofautiana kisiasa, Anaamini tunaweza kukosoana bila kuvunjiana heshima, kutukanana, kubezaba, kukomoana, kuombeana dua mbaya,kulipiziana ,kuviziana,kushikiana mapanga,kurushiana mawe,au hata kutangaziana vita hadharani.

Rais Samia anaamini tunaweza tukaishi Kama watani wa jadi katika mpira ,anaamini tunaweza kutofautiana kisiasa lakini tukaweza kushirikiana katika shughuli za kijamii Kama vile misiba ,harusi,vipaimara na aina yoyote ya shughuli ya kijamii kwa kushikamana na kushirikiana vizuri.

CHADEMA lazima wafahamu kuwa katika mazingira ya kiafrika na siasa zake unaweza ukawa na katiba mpya nzuri na Bora katika Bara la Afrika lakini nchi ikaendeshwa ni Kama kumetangazwa Hali ya hatari, Ikumbukwe kuwa wasimamizi wa katiba Ni sisi wenyewe tunaofahamiana Tabia zetu

Inasikitisha Sana unapoona viongozi Hadi wanachama wa chadema wanapoongozwa na kutawaliwa na matusi, kejeri,dharau,kiburi,lugha za kudhalilishana na maneno yasiyo na staha kwa mamlaka, Chadema Ni watu wasio na Subira Wala uvumilivu,hawana kusema tupate hili kwanza tungoja lile au tufanikiwe hili halafu tutaanza na lile, Ni watu wa kukurupuka kimaneno ,mihemuko,jazba, utoto mwingi na watu wanaoonyesha kukosa ukomavu wa kisiasa. Hawafahamu kuwa huwezi ukapata yote kwa wakati mmoja, hawajuwi kuwa Kuna wakati unatakiwa upunguze ujazo wa matarajio yako na mahitaji yako. Wao chadema wanajuwa Ni lazima upate kila kitu kwa wakati mmoja utafikiri wao ndio watawala.

CHADEMA lazima wajifunze kuwa na Subira, kuwa na uvumilivu. Wajuwe Ni Nani awe msemaji wao katika masuala ya msingi, wajuwe Nani anapaswa kwenda kwenye meza ya mazungumzo, wasiendeshwe na mihemuko ya vijana wao, wawe viongozi wa kuwaongoza vijana wao na kuwapa muelekeo sahihi,tofauti na Sasa Haieleweki Nani Ni msemaji wa chama Wala Nani Ni katibu wa chama, wala nani ni Mwenyekiti wa vijana,Haieleweki upi Ni msimamo wa chama kwa kuwa kila mtu anakuwa na msimamo wake katika Ukurasa wake na kila mtu anaona yeye ndiye chama na ndiye anapaswa asikilizwe na wote.

CHADEMA kwa Sasa kimekosa dira na muelekeo kwa kuwa kimekosa mtendaji wa kukiongoza vizuri,ndio unaona kila mtu akitoa matamko yake atakavyo na ajisikiavyo. Naiona chadema ikishindwa kutoka katika shimo ililoangukia kutokana na kutokumuoa mtu wa kuitoa shimoni

Rais Samia lazima Aheshimiwe na akosolewe kwa lugha za heshima,busara na staha, Mama Samia Ni Rais na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Na Urais Ni Taasisi kubwa Sana ambayo huwezi ukaitikisa Wala kuidhalilisha kwa namna yoyote Ile,huwezi ukaichafua Wala kuipaka matope, huwezi ukaandika maneno yako machafu Kama mlevi, Rais Samia lazima Aheshimiwe na kila mtanzania, Mama Samia Ndio Nembo yetu Ya Taifa, Ndio Taifa Lenyewe, Ndio Amani Yenyewe, Ndio mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vyote tunavyovijuwa na tusivyoviona.

Kazi iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Una matatizo Fulani.
Huo uzalendo ni upi au huo unawapa kupambana asali pesa za misaada zinapigwa kila kukicha, Rushwa imerudi palepale, umeme wanakata kila Leo! Maji ndio hatusemi japo sifa kibao eti wametua kina mama ndio!
Maofisini utendaji umeshuka, Wizara ya Ardhi wamerudi kuwapiga wananchi ulitaka huduma ni pesa.

Mleta mada hivi unayaona au umepewa asali kuleta huu uzi???
 
Tangu lini waramba miguu wakawa na majibu kwenye mambo ya msingi?
jamaa ukimuuliza mambo ya msingi anakimbia mf. anasema wana simiyu wanamkubali
nikamuuliza
aliongea na wangapi?
aliwapataje?
wana umri gani na kiwango gani cha elimu? lengo la kuongea nao lilikuwa nini?
dodoso la maswali lipo wapi?
kakimbia
 
Kwao hao machawa bila kuitaja cdm hawapewi posho

Huyu jamaa ndio kama Yule Naibu waziri ambae akiona mzungu hata kama sio mtalii anasema thank you mama Samia Kwa royol tour hahaha
 
Back
Top Bottom