Ipo siku Lissu atadondoka na kuumia vibaya sana kwenye Meza anazoandaliwa na CHADEMA atumie kama "Jukwaa"

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeona niseme haya mapema sana ili yakitokea ya kutokea CHADEMA wasije kuanza kusema wamehujumiwa na serikali au CCM. Kwa sababu mtu mvivu wa kutumia akili akipata tatizo huwa anakimbilia kutafuta majibu mepesi na rahisi, kama ambavyo amewahi kusema Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere katika kitabu chake cha "Tujisahihishe" cha mwaka 1962.

Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa CHADEMA kushindwa kumuandalia Makamu Mwenyekiti wake jukwaa zuri, la kueleweka na lenye usalama wa kutosha. Yaani Makamu Mwenyekiti anapewa meza ya kupangia nyanya na vitunguu sokoni tena iliyochakaa, kuchoka, kupauka na mbaya sana ili itumike kama jukwaa? Yaani CHADEMA inashindwa kuchangishana pesa kununua mbao ili kutengeneza jukwaa zuri, la kueleweka na lenye usalama?

Chama bora, makini, imara na chenye weledi kama CCM huwa kina mpangilio mzuri sana wa mambo yake ambayo yanakuwa yanaakisi afya njema ya akili ya wanachama pamoja na viongozi wake. Ukiiona chama kinashindwa hata kuandaa tu jukwaa la kiongozi wake mkubwa kama Makamu, basi ujue ndio akili za viongozi wake zilipogota na kufikia. Mpangilio wa vitu huanzia akilini, kichwani na kuja katika matendo. Haya ya kumpatia Lissu meza na kupangiwa matofali chini kwa hakika ni aibu ya karne, ni maajabu yanayostahili kuingia katika maajabu ya Nchi na Bara la Afrika.

CHADEMA haijawahi kuwa siriasi, ni chama kipo kipo tu, kinajiendea endea tu kama kipofu gizani. Kinajisukuma sukuma tu kama mtu aliyezidiwa na pombe kichwani. Hakina mipango wala mikakati, wala maono wala malengo hata ya urefu wa pua zao. Hakiwezi hata kupanga nini kitafanya kesho. Ndiyo maana hakiwezi hata kuweka mipango na maandalizi juu ya jukwaa atakalotumia kiongozi wake kuzungumza na watu.

CHADEMA walivyo wavivu wa kufikiri na kutumia akili vyema, ikitokea Lissu akaanguka na kuumia vibaya mwili wake, utaona kwa ufinyu wa akili wanaanza kuitupia lawama serikali yetu na chama chetu cha Mapinduzi CCM kuwa ndio imesababisha. Watasema Lissu na CHADEMA wamehujumiwa. Halafu haraka sana kama kawaida yao wataanza kutoa namba za kuomba michango ya kumtibu hospitali na gharama zingine. Maana hiyo ndio kazi ambayo CHADEMA inaweza kuifanya kwa ufanisi mzuri sana, kutokana na kupenda sana pesa za bila jasho.

Kazi iendelee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Asante kwa kuliona hili mkuu Lucas Mwashambwa , naona sasa umeanza kupevuka umeweka uchawa pembeni kuamua kuandika mambo yenye kujenga utengamano wa kidugu na kitaifa. Chadema itachukuwa ushauri wako.

Lkn hitimisho lako ndiyo linakwaza watanzania.
 
Asante kwa kuliona hili mkuu Lucas Mwashambwa , naona sasa umeanza kupevuka umeweka uchawa pembeni kuamua kuandika mambo yenye kujenga utengamano wa kidugu na kitaifa. Chadema itachukuwa ushauri wako.

Lkn hitimisho lako ndiyo linakwaza watanzania.
Ni Muhimu sana vyama vya Upinzani viwe siriasi na kuonyesha ule umakini na mpangilio mzuri katika mambo yake.
 
Umekuja kivingine na mifano iliyo hai! Wasipoelewa hapa tena basi...!🀸
Wasipoelewa kwa maneno haya wataelewa kwa maumivu yatakapowakuta. Usipojifunza kupitia historia ,ipo siku wewe ndio utakuwa historia.
 
Dunia ya sasa habari bila picha video clip sw na takataka TU.






KAZI ni kipimo cha UTU
 
for sure ni muda mrefu wamekua wakifanya mzaha na majukwaa ya kiongozi wao huyu, hembu check kwa mfano jukwaa hili hapa chini dah, ni hatari kabisaaaa. hao walinzi wataokoa nini mjamaa akidondoka apo?πŸ’
 

Attachments

  • IMG_20230525_060347.jpg
    150.1 KB · Views: 3
Narudia kusema kuwa CHADEMA mna matatizo makubwa sana tena sana. Mnahitaji kupata msaada wa kisaikolojia. Mmejaa matusi muda wote utafikiri watu mliochaganyikiwa.
 
Picha tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…