Raia mtiifu
Member
- Apr 26, 2019
- 31
- 93
Niende kwenye hoja yangu moja kwa moja! Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la viwanda katika wilaya ya Mkuranga hususani maeneo ya Kisemvule na Dundani.Kwa namna moja ama nyingine hii ni fursa kwa vijana kupata ajira.
Kutokana na ongezeko hili la viwanda, kumesababisha ongezeko kubwa la watu hada vijana wanaofanya kazi kwenye viwanda hivyo na kutokana na hali halisi ya kipato chao wengi wao nyakati za asubuhi na jioni wanapokwenda au kurudi viwandani humo wamekuwa wakitembea kwa miguu pembezoni mwa barabara hiyo kuu ya Kilwa.
Kulingana na idadi yao kuwa kubwa(mamia kwa mamia) na ufinyu wa barabara hiyo inawalazimu kutembea hadi ndani ya eneo la barabara hiyo yenye malori mengi ya mchanga na mizigo pamoja na mabasi ya Kusini, na kama tujuavyo barabara hiyo ni "highway" magari huwa yana kasi kubwa sana endapo siku gari ikaacha njia na kuwafuata huko pembeni kutakuwa na msiba mzito sana.
Rai yangu kwa vyombo husika vya maamuzi,angalieni hili mapema tusisubiri kunda time ya uchunguzi wala kutoa msaada wa majeneza na kugharamia mazishi, fanyeni linalowezekana kuokoa maisha ya hawa vijana wanaohangaika kujitafutia riziki.
Waziri Ulega, Mbunge wa Mkuranga na Waziri wa Ujenzi maeneo yale yana nafasi zenye nyasi pembeni mwa barabara,jaribuni hata kuyafyeka mpanue barabara kidogo kwa ajili ya wapita kwa miguu au angalieni namna mtakayoona inafaa.
KINGA NI BORA KULIKO TIBA.
Pia soma - Ongezeko la Viwanda Mkuranga ni mipango ya Serikali au nguvu ya fedha inachukua nafasi yake?