Ipo siku Mkuranga tutapata msiba wa Taifa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

Kuna vitu vinawezekana kabisaa kufanyika ni uhuni uhuni tu.

Cha ajabu Tanroads wako kila Mkoa..sijui wanafanya kazi gani hasa.
ajari nyingi zinasababishwa na uzembe wa tanroads ktk kuziba mashimo,kuweka vibao vya usalama barabarani,kufyeka majani pembeni mwa barabara nk. Ila kiukweli barabara zetu zipo katika hali nzuri na bora sana ukilinganisha na nchi nyingi AFRIKA. BURUNDI,RWANDA,CONGO,AFRICA YA KATI,NIGER,CHAD,hata kenya uganda,sudan, ethiopia barabara zao zinatia uchungu.

sema tu wabongo hatujikubali.
 
Msiba wa wengi, sherehe...serikali itagharamia mazishi na kutoa pole kwa wafiwa wote
 
mkuu, ni lazma uchukue tahadhari kabla ya majanga. Haiwezekani unaona barabara ni finyu na ni highway unakomaa tu kupita humo tena kwa miguu,alafu pembezoni nje ya barabara kuna sehemu unaweza kupita,ni wakati sasa hata sisi raia tuchukue tahadhari. Ujenzi wa Barabara unahitaji muda na gharama kubwa,meneja wa TANROADS anaweza peleka pendekezo serikali kuu na ikachukua zaidi ya mwaka kuwekewa bajeti, na mpaka kukamilika barabara ni 0.5mwaka,je hapa katikati mtaendelea kuisha tu? tuzinduke.
 
Mkuu kwa tulipofikia kwa sasa Tanzania.
Tunahitaji uwekezaji pia wa Barabara hasa kwa hii njia.

1.Dsm-Mbeye-Songwe-Tunduma (4 Ways)
2.Dsm-Mwanza-Mara ( 4 ways)
3.Dsm-Tanga-Kilimanjaro-Arusha-Namanga(4 ways)

Kwa kuanzia...inawezekana huko kuna pesa nyingi..Nakubali Bongo kwa sasa mambo yanakuwa mazuri,
Mifano ipo..ukiangakia mfano huduma za afya zimebadilika sana na kuna uwekezaji mkubwa mno umefanyika.

Sasa tunahitaji mageuzi ya miundombinu yenye akili hasa..
Tuachane na hao wengine,waje waige kwetu kama wanavyokuja Muhimbili kwa sasa kujifunza.

Tukimbie na kasi yetu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…