Ipo siku tutajenga sanamu ya Hayati Magufuli na kufungua Maktaba yake ili vizazi vijifunze Uzalendo

Ipo siku tutajenga sanamu ya Hayati Magufuli na kufungua Maktaba yake ili vizazi vijifunze Uzalendo

Mimi kama mimi, kwa heshima yake yeye kama yeye, ambaye aliaminiwa kuishika nafasi ya Rais wa nchi yetu katika awamu ya 5, kesho sintakuja jukwaani kwa ajili ya maoni yoyote yule kuhusu yeye.

Nathamini nafasi ya familia katika maombolezo, kumbukizi na hata kusheherekea mazuri yake kama mume, baba wa familia, mjomba, baba mkubwa, baba mdogo, kaka, mpwa, rafiki, jamaa wa karibu, mwana jumuiya, muumini, mteja, mpangaji, mlipa kodi, kiongozi wa CCM, dikteta, muimla, dhalimu, fedhuli, amiri jeshi mkuu, Rais, Mwenyekiti Taifa wa CCM, jirani, mchepuko, na sifa nyingine yoyote ile aliyokuwa nayo kama binadamu wa kawaida mwenye sifa ya kuwa "possessed to many societies" na jina ake kubadilika kutokana na matakwa ya wakati.
Sawa kabisa ,
lkn kumbuka kua mchuma janga hula na WA kwao.
 
Wenyewe wanamuita shujaa wa Afrika
Hana ushujaa wowote bana.
Mtesi wa watu.
Katika Hali ya kawaida mtu mmoja huwezi kua kocha,golikipa,beki,mchezaji,refalii,mshika kibendera na mshangiliaji.

Nikikumbuka

Wapinzani nchi nzima walishindwa au kukosea kujaza fomu za uchaguzi,Tena wengine walishakua wabunge ama madiwani kabla,nachoka kabisa.

Wapinzani kutekwa wakirudisha fomu zao nachoka kabisa.

Wapinzani kushindwa ubunge nchi nzima nachoka kabisa.

Shujaa anawagawa raia wake na kupandikaiza chuki?

Nyerere aliwaunganisha watanganyika nchi nzima,aliwafanya wahaya wakafanyw kazi mtwara na wamakonde wakafanyw kazi Tanga,wasukuma wakafanye Kilimanjaro na wachaga Mara,alivunja ukabila na kiwafanya watanganyika wajione Kila mkoa ni wao.
Leo anakuja mtu anaanza kubagua watu wake anaowaongoza.
Mfano wabomolee watu wa Kimara lakini watu wa Mwanza usiwabomolee.
pia alowaagiza watu wake wasipeleke maendeleo Huku kwa sababu wamechagua mpinzani

Aisee Mimi ni msukuma lkn yule bwana wala hakunishawishi kabisa.
 
Nyie mamburula ndio hamuwezi kumkumbuka 🤣🤣🤣
Shilingi Ina pande mbili ndugu,
Kama wewe alikufaa,Kuna wengine walikufa.

Isifikiri ukimpenda wewe wote watampenda.
Ukimuona anafaa wengine wanamuona hafai.


Kwa kifupi aliharibu na ameshaharibu maisha ya wafanyakazi, wafanyabiashara na wakulima.

Kumbuka ukipandisha mishahara ya wafanyakazi kwa mujibu wa muundo na utaratibu wa kiutumishi kama ulivyowekwa na watangulizi wake ni kuinua maisha wa watanzania wote.
Kwa sababu mkulima na mfanya biashara watafaidi na maisha Yao yatakua Bora.

Sasa hivi katengeneza gepu kubwa mno la kipato atakacho enda kulipwa mfanyakazi aliekuwepo wakati wa Jiwe atakapo staafu.

Wafanyakazi wengi walitumikia nchi kwa uaminifu wakitegemea mishahara TU.huyu amistaafu atastaafu na mafao kidogo sana kwa sababu mshahara wake haukupanda kwa Mika mitano ya Jiwe.
Kumbuka wengi wetu hapa Tanzania ni watoto wa ama waalimu,manesi na watumishi wengine wa uma.

Mfanyakazi akipata mshahara anaenda kwa mfanyabiashara kununua magitaji,mfanyabiashara akiishiwa bidhaa anaenda kununua kwa mkulima hii inaitwa mzunguko wa pesa.
je huoni hapa maisha ya mtanzania yalivunjwa kwa akili za mtu mmoja TU?
Je huyo ni shujaa ama dharim?
 
Shilingi Ina pande mbili ndugu,
Kama wewe alikufaa,Kuna wengine walikufa.

Isifikiri ukimpenda wewe wote watampenda.
Ukimuona anafaa wengine wanamuona hafai.


Kwa kifupi aliharibu na ameshaharibu maisha ya wafanyakazi, wafanyabiashara na wakulima.

Kumbuka ukipandisha mishahara ya wafanyakazi kwa mujibu wa muundo na utaratibu wa kiutumishi kama ulivyowekwa na watangulizi wake ni kuinua maisha wa watanzania wote.
Kwa sababu mkulima na mfanya biashara watafaidi na maisha Yao yatakua Bora.

Sasa hivi katengeneza gepu kubwa mno la kipato atakacho enda kulipwa mfanyakazi aliekuwepo wakati wa Jiwe atakapo staafu.

Wafanyakazi wengi walitumikia nchi kwa uaminifu wakitegemea mishahara TU.huyu amistaafu atastaafu na mafao kidogo sana kwa sababu mshahara wake haukupanda kwa Mika mitano ya Jiwe.
Kumbuka wengi wetu hapa Tanzania ni watoto wa ama waalimu,manesi na watumishi wengine wa uma.

Mfanyakazi akipata mshahara anaenda kwa mfanyabiashara kununua magitaji,mfanyabiashara akiishiwa bidhaa anaenda kununua kwa mkulima hii inaitwa mzunguko wa pesa.
je huoni hapa maisha ya mtanzania yalivunjwa kwa akili za mtu mmoja TU?
Je huyo ni shujaa ama dharim?
Umeandika message ndefu nonsense
Kwa hiyo sasa hivi kuna unafuu gani wa maisha
Mimi mwenyewe ni mtumishi mbona sijaona cha maana labda kwa wabunge ndio kuna unafuu maana wameongezewa mshara wa maana kutoka milioni 12 hadi milion 16.5
Sisi watumishi tumeongezewa elfu 20 sasa huyo elfu ishirii nayo ni ya kutamba mmeongeza mshahara

Bora Kipindi cha Magufuli tuliona miradi mingi inafanyika sasa hivi sijaona mradi mpya wa maana mingine alivyofariki tu Magufuli na yenyewe imekufa mfano mradi wa mwendokasi mbezi kibaha hao watangulizi wake wangekuwa wamefanya la maana nchi isingekuwa maskini hadi leo.

Nyie mna chuki binafi sio za kujenga na maendeleo tunajua wengi wenu mnaomchukia mlikuwa wapiga dili,vyeti feki,wengine mnatumwa kumchafua hasa hapa Jf lakini kwa taarifa yenu na yanayoendelea sasa hivi wananchi tutaendelea kumkumbuka sisi na vizazi vijavyo mnahangaika sana🤣🤣🤣🤣
 
Binadamu huwezi kuwafurahisha watu wote lakini muhimu kuliko vyote kuhakikisha unachukia maovu na kutetea wanyonge.
Kwasasa je,wanyonge wanasaidiwa? au hata kupewa matumaini? Kama jibu ni ndiyo basi tunaelekea kwenye mafanikio.
Je,Mafisadi wezi wa Mali za Umma wanashughurikiwa ipasavyo?basi hata kukemewa tu inatosha.
Watumishi wanaibiwa hawalipwi stahiki zao matokeo yake wanatengeza mfumo wa kuwaibia wananchi wasio na hatia.
Inawezekana JPM alikuwa mbaya lakini kwa hali inayoendelea ni bora kuwa na mbaya kuliko kuwa na mzuri wa aina hii?
 
Bila Magufuli makao makuu dodoma kingebaki kuwa kitendawili daima!!! SGR ingebaki kuwa ndoto!! na bwawa la mwalimu Nyerere (Stigler's George hydroelectric power) lingebaki kuwa ndoto ya mchana daima!! Hii miradi yote ilikuwapo kwenye makaratasi lakini hakuna aliyekuwa na uthubutu wa kuianza!! Hapo ndipo wapinzani wa Magufuli wanapogeuka kuwa wapole ghafla!!
 
Magufuli angekuwepo saizi tungekuwa tunashuhudia ujenzi wa barabara ya njia 4 kuanzia mail Moja mpaka chalinze ama Morogoro.
 
Itakua vizuri sana.
Maana sisi tulioharibiwa maisha yetu na kuumizwa tutapata sehemu rasmi ya kwenda kumwaga laana zetu kuwaonesha wajukuu na vizazi vyetu jinsi mtu alieharibu maisha yetu alivyokua.
Tutapata nafasi ya kuchapa viboko sanamu hiyo.
Maana shilingi Ina pande mbili,hata tukiwa watatau TU nchi nzima tulio tendwa na bwana yule,tunatosha kuonesha hisia zetu.
Kumbukumbu sio lazima kwa mambo mazuri TU,hata mambo mabaya yanawekewa kumbukumbu,ndio maana Leo hii Kuna kumbukumbu za picha na vifaa sehemu mbalimbali nchini na duniani kote za jinsi wakoloni na waovu wengine walivyotumia kutesea babu zetu.
Sasa mwenye vyeti feki ulitegemea nini
 
Huwezi kumkumbuka wewe peke yako malaya unaefumuliwa malinda. Ila wazalendo wanamkumbuka kila leo. Bandari isingeuzwe kifala namna hii shwaini mkubwa. Kavae bikini uendelee kuliwa
Bandari ipi imeuzwa wewe lofa toka Chato? Weka risiti hapa kuthibitisha
 
Mungu wewe unachukua majabali una chukua wanaume ambao kweli jando lao halikuwa la ganzi. Wanaume wenye misuli ya Imani na uwezo wakuona kesho kwa Imani na matendo. Kwa Tanzania Ulitupa Hayati John Pombe Magufuli. Kijana alie zaliwa ktk ufukara ila ukampa kukikalia kiti cha Jamuhuri ya watu Wa Tanzania na kweli akatupa darasa ambalo kamwe kwa tulio Baki hatuto msahau.

Kama ilivyo kwa mzazi alituchapa na alituadabisha kiukweli kweli, akiwa na ndoto za mzazi siku moja siku moja tutamkumbuka nakwenda ktk kaburi lake nakusema baba tunakukumbuka kama Mungu angetupenda basi angalau angekupa mwaka mmoja tu zaidi utuchape viboko ili tuwe na akili zaidi ya hizi tulizipata kwa viboko na adhabu zako. Tungetubu kama mtoto anavyotubu kwa mzazi baada ya kugunduwa viboko alichapwa ndio vimemfanya kuwa Bora leo. Kwa hakika kama sio kifo kilikuwa na nia yakumpa kiti muda wa ziada jambo halikutokea ktk Historian yetu.

Jemedari huyu wa awamu ya Tano aliitikisa nchi ikatikisika, aliitikisa majabali yakatikisika na alivitikisa viti visivyoguswa vikatikisika kwake usawa ndio ilikuwa ndoto. Alipambana na majangili mpaka wanyama Porini na miti maporini ikawa inamuombea kwa Mungu. Alilinda kwa mkono wa chuma mipaka na siri za serikali kiasi kila alie na siri aliona kuliko kuitoa Bora kunywa sumu. Kwake Jamuhuri ndio ilikuwa ibada yake mbele za Mungu wake nawana Jamuhuri walimtambua hivyo. Hakuna mission alipanga Ika fail japo mwisho uwenda some thing wrong happen ktk mission zake itabaki kuwa top secret japo madhara makubwa yatakuwepo huko mbeleni.

Alimanisha alicho Maanisha na hakuwa na utani kwa kile alimanisha. Kwake dam na neno lake vilikuwa nijambo lakuchaguwa na hiyo ndio maana ya kiongozi. Wanafiki na mapandikizi walipata tabu sana maana aliwafanya wajione kama mapanzi mbele ya tai.

Hakuwa na mchezo hakuwa na masihara kwenye kitu kinaitwa hela ya serikali na nidham ya kazi kama ulitaka kuona rangi ya mtawala huyu basi cheza na hela ya serikali na kuwa mzembe kazin utachekea chooni. Watu walirudisha risiti na pesa ilio Baki ya serikali. Watu waliogopa pesa ya serikali kiasi ilifika mahali TUNAKUTANA kwa Mama ntilie Yani mama ntilie alipanda thamani kuliko 5 star hotels ama restaurant ama kwa hakika nchi ilisimama na vitambi vya upigani vilipotea.

Sito sahau story yakutisha ya kijana mmoja jirani kijana alie kuwa misheni town alie kuwa akila kwa kutumia sim yake aka misheni town. Nakama unakumbuka ili kuleta nidham kazin na mtaani Baba alikuwa sahani moja na misheni town. Kijana yule alikuwa akila maisha mjini pasipo kufanya kazi leo Tiss kesho Jwtz ila chini ya Mwamba kwa mara ya kwanza kijana yule alianza kujifungia ndani kama mbwa wakati wa mchana na kujifungulia usiku. Kijana alianza kukonda na mwisho alikufa kifo cha ghafla baada yakukutana na team hatari yakutokomeza wapigaji. Shikamoo Baba it was real top top secret never before. Kuna watu walijimaliza wenyewe baada yakugunduwa wamefanya madudu na adhabu yake ni kifo kwa usaliti wao. Huyo ndio Mwamba Magufuli.

Mbabe huyu alitufanya watu wawe na plan B ktk kila wakifanya na alifanya watu kuheshim mishara yao nakupenda ndoa zao while madada poa wakifa njaa nakutafuta kazi nyingine pasipo shurutishwa na mtu. Nikatika kipindi chake alifanya mageuzi makubwa na yaaina yake kwenye secta ya ajira sio hivyo tu alihakikisha masikini akiingia Ofisi ya serikali awe mfalme asikudanganye mtu masikini na mtu wa chini alikuwa mfalme maana ilikuwa akisikia mtu amedhulumiwa au akionewa na RC walile eneo hakufanyia kazi tatizo lake unakiwa kichwa bila notice. He was Iron Men. Acha chezea hii namba.

Nchi ilizimgirwa na hofu ya kuwa muwovu ktk Taifa lako nikujitafutia adhabu ya kifo jambo lilimfanya kila muhalifu kuacha uhalifu nakuwa Raia mwema kwakufanya kazi kwa bidii ila sio uhalifu ndio ktk kipindi hiki watu walifanya biashara ndogondogo kwa kiwango cha jabu sana Ali push watu kujiajiri nakutafuta ideas na yeye kuwapa nguvu free market. Wapo walimponda ila alikuwa na ndoto ambayo kaburi imeimeza ghafla.

Siwezi simulia au kueleza kile aliwafanya wauza unga ila mtafute muuza unga atakwambia ilikuwa mithili ya picha za CIA na mossad vile aliutokomeza huu mtandao alihakikisha either unalala chini au unaacha mama mkanye mwanao. He was master on Intelligence of finding crime. Nakweli wauza madawa na wala madawa walijikuta soba bila shuruti. Moja ya jambo sitosahau nimla mdawa mmoja kuniambia ameacha dawa maana hakuna dawa zakulevya... Lazima huko usalama huyu jamaa awe reference ya genius president on crime finding.

Hayati Magufuli hakuwa kiumbe cha kawaida hakuwa mwanadam au kiongozi wakawaida alipania na alikumbuka ahadi yake kwa Mungu na akiifanyia kaz kwa dam na jasho kwa ajili ya

Tanzania. Moja maisha yalio watisha wengi nikufanya kaz usiku wakati mwingine usiku mzito sana the guy was not normal human being lazima watu wakaribu watasimulia maajabu ya huyu kiumbe.

Alilijua duka na alikuwa na kila siri ya duka na hili likiwatetemesha wengi japo wazalendo walio mpenda walisema Mungu Asante umetuletea mkombozi. Alizijuwa siri ambazo watangulizi wake uwenda hawakudhani angezijuwa na alisoma sana kila siri wakati mwingine files ZINGINE mezani mwake zilimtisha hata yeye mwenyewe na uwenda ndio maana alituacha ktk wakati hakuna aliamini angetuacha japo Yeye alishakiona kifo.

Mwamba ndio mwanaume alie Jenga hili Taifa kwenye miundo mbinu huwezi simulia miundombinu ya Taifa hili bila kumtaja Mwamba Magufuli. Alitandaza lami mpaka Malaika wa Mbinguni wakasema lazima utaliongoza hili Taifa. Wachambuzi wa mambo wanasema kama angekuwa kibaka uwenda ndio waziri angekuwa na ukwasi wakitisha ktk Taifa hili ila alikuwa wakawaida sana.

Ukikaa nakujiuliza why Kuna kundi lina mchukia sana jibu nimoja tu kitu alicho wafanyia na pin alizowawekea na makofuli aliwafungia milango yao ya ulaji kamwe hawatoweza kuifungua hata baada ya miaka 100 yani aliona zaidi yao mfano nani anapenda mradi wa bwawa la mwalim Nyerere kama unamacho ya mbali Yani huu mradi unawauma watu fulani sana Usiniulize kwanini.

Miaka inakuja Gemedari huyu atakuwa Habari ya Taifa na huwenda siku zinakuja kutakuwa na Magufuli day. Siku zinakuja kumdhihaki nakumsema huyu Mwamba vibaya unakosa kura siku zinakuja hata upinzani watamtaja kwa mema. Wajukuu watamuimba nakumsoma mashuleni.

Maana ndie kiongozi alie sema moyoni mwake kuliko kuishi nakupigiwa mizinga 21 na heshima na kukaa ktk magorofa nakula Pepo za Dunia ni Bora kufa nikiacha alama ambayo kila mtu hatoangalia mabaya yangu ila mema yangu. Nayeye mwenyewe kabla ya kutuacha aliwahi sema "Ipo siku Watanzania Mtanikumbuka sio kwa mabaya yangu ila Mazuri hivyo tuzidi kushikamana na kupenda" Hayati Baba wa Ujenzi wa Taifa la Tanzania John Pombe Magufuli.

Hayati Magufuli ni nyota iliozima wakati wa mchana ila lijapo giza atamulika kwa milele. Asante Baba Asante Mzee Magufuli umetufundisha Uzalendo wa kweli kwa Taifa letu. Amen
Mnara wa kwanza
Tarehe 20.05.2023 tunazindua ikulu mpya Dodoma. Naomba muweke kumbukumbu maono yangu
Yule mpuizi ajengewe sanamu eti shujaa alichoma nyavu zetu kwa kutuonea na alikuwa nauwa elimu yetu kafirisi mifuko yote kwa kweli mungu amlani kabisa mwizi yule
 
Yule mpuizi ajengewe sanamu eti shujaa alichoma nyavu zetu kwa kutuonea na alikuwa nauwa elimu yetu kafirisi mifuko yote kwa kweli mungu amlani kabisa mwizi yule
Wewe ndui jambazi la majini na makao makuu yenu pale Kirumba mtaa wa Ghana unathubutu kutoa maneno ya kufuru kwa jabali?
 
Huwezi kumkumbuka wewe peke yako malaya unaefumuliwa malinda. Ila wazalendo wanamkumbuka kila leo. Bandari isingeuzwe kifala namna hii shwaini mkubwa. Kavae bikini uendelee kuliwa
Mtoto wa malaya wewe, unachojuwa ni matusi tu uliyorithi kutoka kwa mama yako.
 
Mzilankende Mnyago
Chuma , Jiwe, Ngosha
Baba Jesca
 
Back
Top Bottom