Hizbollah wameamua kufa na kuwapigania Wapalestina, Iran wameamua kuumia, kuteseka na kufa kuwapigania Palestina.
Dunia upande mwingine imewaacha wapalestina na kuamua kusimama na mwenye nguvu Israeli.
Kwani hawa Hizbollah na Iran siwangeamua tu kuendelea zao na maisha na kuachana na mambo ya Palestina? wameamua kutokubali uonevu baadala yake wanahitaji kuona haki ya waPalestina ambayo Dunia haitaki kuona inatokea.
Wapalestina wanahitaji Taifa lao nao waendelee na maisha yao na si kuishi chini ya slave masters-Israel, Dunia inahitaji kuwa na suluhu dhidi ya maisha ya wapalestina.
Nimeguswa kuandika uzi huu kutokana na bandiko ninaloliweka hapo juu.
Injili imesheni upendo mkuu usiokuwa na kifani aliokuwa na Yesu Kristo na Mungu baba kutupenda mno sisi hata akamtoa mwanawe wa pekee kuja kutufia ili tusipotee.
Yohana 3:16 - 17:
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda sana ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee ili tusipotee."
Tunafundishwa makanisani, na swali hili limezoeleka kuufikisha ujumbe huo, vilivyo:
"Nani anaweza kukubali kufa badala ya rafiki yake?"
Ama kwa hakika Yesu hakuwa na cha kupata kama yeye kwa kuja kutufia. Alikuwa na vyote kwa baba yake. Lakini kwa kutupenda kwake tu, akakubali kuja kutufia ili tukapate kuokoka.
Huu ndiyo unaoitwa upendo wa agape.
Hebu tujikumbushe upendo walio nao Hezbollah, Iran, Houthi au wale wengine wa kule Iraq kwa ndugu zao wa Palestina walioko kwenye jitihada zao kuupata uhuru wao:
"Kipi ambacho walikosa Hezbollah, Houthi au Iran kwenda kujiingiza kwenye sokomoko hili linaowagharimu vifo na hata vitisho vya kuteketezwa wote?"
Hivi kwa matendo ya hawa ndugu kwa wapalestina, inahitajika nguvu kuuelezea upendo wa Yesu kwetu au hata tunaofunzwa makanisani, kuwa nao kuwaelekea wengine?