Wakuu wa Iran wanaishi katika wasiwasi mkubwa, kiasi cha kutojiamini.
Fikiria kuwa hakuna nchi, si Israel au USA iliyosema itaishambulia Iran wakati wa maziko ya Ayatollah, lakini wakuu wa Iran, muda wote wamekuwa wakisema, ole wao atakayewashambulia wakati wa maziko ya Ayatollah!! Inashangaza sana, wasiwasi na hofu ni mbaya sana. Hakuna aliyesema atawashambulia, lakini wakati wote wapo kwenye hofu ya kushambuliwa!! Ni aheri wangewekeza zaidi katika maelewano na majirani zake, na kuondoa yale matamko ya chuki ya kusema, "Israel haitakiwi kuwepo", "wasuni siyo waislam, na hivyo kila nchi yenye washia wahakikisha wanaondoa tawala zinazoongozwa na wasuni", "death to America"!!. Mahusiano mema, yatawafanya wairan waishi kwa kujiamini kuliko kuishi wakati wote katika hofu.