Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 14,762
- 32,386
Hamjambo!
Hakuna ambaye alikuwa na mahusiano mazuri na Baba yake alafu siku mzee amedanja akubali kirahisi kutohudhuria mazishi ya mzee wake. Tena kwa nafasi kubwa aliyonayo ya Ayatolla.
Iran inadai imeshinda Vita. Naamini wanamaanisha kuzuia lengo la kulinda dola Lao lisiangushwe na Marekani na Israel. Huo kwao ni ushindi.
Ila bado inaonekana Kuna tishio LA kiusalama. Na hawana uhakika wa ulinzi wa kutosha kumlinda Ayatolla Mojtaba Khamenei.
Au Pengine Mojtaba alijeruhiwa Vibaya sana kiasi kwamba ameathirika viungo hivyo wanafikiria watamtoaje.
Albu au kuepuka usumbufu wa kumbeba kiongozi wao.
Ijumaa Kareem
Aibu naona mimi. Kiukweli tulikuwa tunaaamini tumeshinda vita lakini kiuhalisia hali yetu ni mbaya sana. Kwa sasa hatuna nguvu kabisa tumekuwa na ulemavu. Na woga tulio nao ni mkubwa sana. Mtu kushindwa mzika babaye kwa sababu ya woga wa kuuawa ni kiwango cha juu kabisa cha woga na kushindwa.
Basi angalau hata wangemvalisha dera au abaya ahudhurie kama mwanamke kimya kimya. Nalo hilo wanasema wameona Mayahudi watamgundua watamwua. Na bado waliiomba Marekani iwaambie wayahudi wasifanye tukio siku hiyo...
Kwa kweli nimekuwa very disappointed na Iran. Nliitegemea sana imeniangusha