Sio inavyosemwa tu. Go deep.
Soma malengo ya vita ya US katika vita hii yaliyotajwa kwa ufasaha na Donald Trump pale mwanzoni kabisa kama kuna lililotimia. Israel haikuweka malengo yake wazi bali ilishirikiana na Marekani katika vita hii. Lakini inajulikana tangu awali kuwa lengo kuu la Israiel ni kuangamiza utawala wa kitheokrasia wa Iran kuvunja nguvu ya kivita ya taifa hilo na hivyo kuondoa tishio lolote linaloweza kuzuia Israel isitawale Mashariki ya Kati ikiwa super power pekee eneo hilo.
Irani ilishtukizwa katikati ya mazungumzo ya amani hivyo inajulikana kuwa malengo yake yalikuwa kuzuia Marekani na Israel wasiondoe utawala wao (wa Ayatollah na IRGC) na kuzuia kutekwa kwa nchi yao. Walipata kipigo kikubwa sana kwa viongozi wao wote kuuawa (kwa kuviziwa). Silaha zao kubwa nyingi ziliharibiwa na wapiganaji na raia wao wengi wengi (pamoja na watoto wa shule 160) waliuawa.
Lakini Iran kwa kutumia teknolojia rahisi ya drones, AI, na makombora machache waliweza kuharibu vituo vingi vya kijeshi vya Marekani huko Mashariki ya Kati, kuua wanajeshi 13 wa US na kujeruhi wengine kama 140 hivi. Pia kubomoa mifumo ya rada, kuangusha ndege za vita, n.k. na, KIKUBWA ZAIDI, kudhibiti pito la bahari la Hormuz. Meli zaidi ya elfu 20 zilikwama. Hadi leo Iran wanadhibiti pito hilo na kukusanya tozo ambayo haikuwepo awali. Dunia nzima inateseka kwa uhaba na kupanda bei ya mafuta.
Marekani haikuwa na namna zaidi ya kutaka mazungumzo ya amani TENA. Juzi hapa Trump aliulizwa kuhusu kuwabana Iran wasiwe na ballistic missiles akasema haitakuwa haki kwani Saudi Arabia, Israel, na majirani wengine wanazo. Hivyo Iran nao lazima wawe nazo! Hataki hata kuongelea kuwadhibiti Houthi na Hezbollah. Kawaachia msala Israel.
Hadi hapo, soma yanayoendelea upime na kuamua mwenyewe kama Iran hadi sasa wameshinda vita au vipi katika malengo yote yaliyosemwa kuhusu vita hii.