Iran inaenda kuanguka na huenda baba wa Taifa hilo yakamkuta ya Sadam Hussein

Pamoja na hayo yote ......nyumba ya ayatollah imechomwa Moto SASA ayatollah anaishi jeshini......maana ulaiani watu wata mchoma mshikaki
 
Pamoja na hayo yote ......nyumba ya ayatollah imechomwa Moto SASA ayatollah anaishi jeshini......maana ulaiani watu wata mchoma mshikaki
Kawaida hiyo mbona. Tena huko Iran inaelekea Kuna demokrasia kubwa Sana.
Huko us waandamanaji waliingia ikulu kabisa wakachekewa. Baadae wakaguswa kwa vibao viwili vitatu ikawa kelele i'la baadae wakaondoka.
Kama Ni kweli wameweza kuisogelea nyumba hiyo na kuichoma as you said Ni Jambo kubwa la Uhuru. Huku kwetu Kenya hawatapata hi kitu.
Nb.
Iran will never fall again.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Serikali za kidini kuanguka siyo rahisi na hata zikianguka zitarudi tena madarakani. Angalia Taliban kule Afghanistan. America iliwaangusha, wakachapana miaka 20 na leo wamerudi tena madarakani. Usichezee dini wewe.
bepari2020 ilo neno chini ya uandishi wko lina maana gani mbna unatengeneza chuki zisizo na maan ingali ktk taifa tunaishi vyema
 
Mbinu iliyopo sasa na destroy them from within..muda utaongea ngoja tuone..hakuna taifa au ufalme mkubwa kuwahi kutokea kama ottoman na roman wako wapi leo hii.

#MaendeleoHayanaChama
 
Iran wataisikia kwenye bomba tofauti na wanavyoisoma
 
Dunia itapigwa butwaa kusikia Rais wa Taifa fulani lenye miguvu ya kiuchumi kulala usingizini.
Hii kauli au haya maneno unayarudia rudia sana.
Nakukubali kwenye utabiri wako wa mambo ya Bongo Land lakini kuhusu mustakabali wa Russia au Putin unaweza kupoteza credibility yako ya utabiri sijui unaita maono.

Kimsingi hiki unacho rudia rudia kutoa utabiri unarudia mawazo au kauli za watu wa Ukraine kinachoitwa THE BLACK SWAN EVENT au BLACK SWAN THEORY. Kwamba kuna Tukio lisilotegemewa la kushituwa litatokea nchini Russia na kusababisha Putin aondoke madarakani kisha Ukraine ashinde vita au watu wa magharibi USA/NATO waweke vibaraka wao nchini Russia.

Hii kitu ni kama ndoto au wishful thinking. Kwanini nasema hivyo?
Tangu mwezi March au May sikumbuki vizuri watu haohao walikuwa wanasema Russia ameishiwa silaha ( makombora) ya kuishambulia Ukraine kwa mbali na kwa usahihi, cha kushangaza siku wakimkorofisha kwa kushambulia kigaidi miundombinu ya Russia anajibu kwa kurusha kama mvua makombora waliyosema ameishiwa kisha wanalia lia ameshambulia miundombinu ya kiraia ashitakiwe The Hague. Wenye akili wanajiuliza haya makombora katoa wapi mbona walisema ameishiwa?

Watu haohao wamekunja mkia tukio la kombora lililouwa watu wawili Poland. Wamemkanya Zelenskyy na washirika wengine wa NATO wasitpige kelele kuomba Poland aitishe Article 4 au Article 5 ya NATO waweze kujibu mapio kuingia vitani na Russia, na sasa kimya kimya wanawaomba Ukraine wakae meza ya mazungumzo na Russia.

Unafikiri wanaogopa nini dhidi ya Russia?
Jiulize kwanini Israel anakataa kuwafungia Ukraine mfumo wa kujilinda anga lao unao itwa Iron Dome?
Kwanini wameshindwa kumuondoa au kumuuwa Assad wa Syria?
Je taarifa zao za kijasusi zinaweza kuaminiwa kwa 100% ikiwemo hiyo ya kifo tarajiwa cha Putin au kupinduliwa madarakani kunako tarajiwa?
 
Pamoja na hayo yote ......nyumba ya ayatollah imechomwa Moto SASA ayatollah anaishi jeshini......maana ulaiani watu wata mchoma mshikaki
Hiyo iliyochomwa sio ya huyu kiongozi wa sasa(Khamenei) ni ya yule mwasisi (Khomeini) ambayo ni museum
 
civil wars haitegemei ubora wa jeshi lako bali ubora wa intelligence yako maana unapigana na raia wako huenda wadhamin wakawa ndan ya serikali
 
civil wars haitegemei ubora wa jeshi lako bali ubora wa intelligence yako maana unapigana na raia wako huenda wadhamin wakawa ndan ya serikali
Hiyo kweli ila mfano uliotolewa wa Syria ndio ulisababisha niandike hivyo sababu wamagharibi walitumia mbinu hiyo Libya wakataka kutumia Syria na Venezuela ,wanaanza Raia wao mwishoni wanakuja kumalizia kwa mgongo wa UN .ndio maana nikamwambia kwa IRAN hiyo mbinu ya kitoto kutokana na uwezo wake wa kijeshi utakapoingiza ndege yeye anaweza kupiga kwako popote kwa makombora huwezi fananisha IRAN na Syria
 
Kwahyo imewauma sana Iran kuangusha ndege Yao ya abiria Hila wao walivyoangusha ndege ya abiria ya iran ilikuwa poa tu
 
Wasaudia wamesha infiltrate wajeshi wao.

#MaendeleoHayanaChama
 
siku hz hakuna wa kuja nchini mwako mbali na wakufunz wa kijeshi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…