Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kinachoitwa shambulizi la Iran kwa Israel jana ni kelele kubwa tu za majidai na usumbufu ambazo hazikuleta chochote cha maana. Unashambulia nchi iliyo umbali wa KM 2300 kwa kutuma drones ambazo zinakatiza anga za nchi nyingine kadhaa kwa masaa na karibia zote kuishia kutunguliwa au kuanguka njiani kwa kuishiwa chaji!
Kwa alichokifanya Israel cha kushambulia ubalozi na kuua makamanda wa Iran kwenye ugomvi ni sawa na umepigwa kofi la usoni na ukaishia kumsukuma au kumkunja tu shati aliyekuzabua kofi. Aliyesukumwa ndio ataamua huu ugomvi utaendeleaje au utaishaje. Ngoja tusubiri majibu yake.