Iran na Israel: Kutoka Mabeste Hadi Maadui
Basi hebu nikusimulie hii stori kali – kama vile tupo vijiweni tunagawana kahawa ya jioni.
Zamani hizi, kabla mambo hayajaharibika, Iran na Israel walikuwa kama mabest wa damu. Walishirikiana kwenye biashara, walipigiana tafu kwenye siasa, na walikuwa upande mmoja dhidi ya maadui wa Kiarabu. Ila siku hizi? Wamegeukana kama wapenzi waliotemana kwa hasira – kila mmoja anangoja mwenzake adondoke.
---
Zamani za Mfalme Shah
Tukirudi miaka ya 1960 hadi 1979, Iran ilikuwa chini ya mfalme anaitwa Shah Mohammad Reza Pahlavi. Mfalme huyu alipenda maendeleo ya kisasa na aliendesha nchi kwa mwelekeo wa Magharibi alichukia sana utamaduni wa kiislam. Ndiyo maana akawa mshikaji mkubwa wa Israel – walikuwa wanasaidiana kiintelijensia, kwenye biashara, kilimo, hadi kwenye mambo ya kijeshi. Walikuwa close sana.
Lakini mambo yalibadilika mwaka 1979, wakati Waislamu wa Kishia walipochukua nchi na kumfukuza mfalme. Wakampandisha jukwaani kiongozi wa kidini aliyeitwa Ayatollah Khomeini. Huyu mzee hakuwa na mchezo – alitangaza wazi kwamba Israel ni "adui wa Uislamu" na "shetani mdogo". Hapo ndipo urafiki ulipokufa rasmi.
---
Kwanini Sasa Wanachapana?
Hebu sasa nikuchambue sababu kuu zinazofanya Iran na Israel wachungiane kwa jicho la kisasi hadi leo:
---
1. Siasa na Dini
Iran ni taifa la Kishia, lenye misimamo mikali ya Kiislamu. Wanajiona kama walinzi wa Waislamu wote duniani. Israel wao ni taifa la Kiyahudi. Kwa Iran, kuwepo kwa Israel ni sawa na udhalilishaji wa Wapalestina. Hivyo, kila Israel anavyowapiga Gaza, Iran anakasirika kama vile kakosewa binafsi.
---
2. Palestina na Makundi ya Kijeshi
Iran anawasaidia makundi kama Hezbollah kule Lebanon na Hamas kule Gaza – ambayo yanampinga Israel kwa nguvu zote. Israel akiona Iran anapeleka silaha au hela, anachukulia kama ni shambulio la moja kwa moja.
---
3. Bomu la Nyuklia
Iran inasemekana kuwa inajaribu kutengeneza silaha za nyuklia. Israel ana hofu kubwa – maana kama Iran atafanikiwa, basi Israel ataishi kwa hofu ya kubonyezwa “button” yoyote muda wowote.
---
4. Vita ya Proxy
Hawa hawachapani uso kwa uso mara nyingi. Wanapigana kupitia watu wa kati (proxy). Iran anasukuma makundi ya wapiganaji, Israel anapiga kwa drones na mashambulizi ya angani.
---
5. Marekani Katikati
Iran ana historia ya chuki na Marekani, hasa tangu mwaka 1979 walipopindua serikali na kushikilia mabalozi wa Kimarekani. Israel ni rafiki mkubwa wa Marekani, hivyo kila msaada Marekani anampa Israel, ni kama kumkuna Iran penye majipu.
---
Leo Hii Mambo Yakoje?
Sasa hivi hali ni mbaya zaidi. Israel anashambulia maeneo ya Syria na Lebanon, akidai anapiga wapiganaji wa Iran. Iran naye alishawahi kurusha makombora kuelekea Israel (2024)na sasa hivi wako kazini vitani, japo mengi yalidunguliwa njiani.
Dunia nzima inajiuliza, “Hawa si walikuwa marafiki zamani?” Lakini usiku wa manane, ni kama ex wako aliyekutumia DM alafu kesho anakutukana kwenye status – imebaki historia.
---
Tutaona Mwisho?
Hakuna ajuaye mwisho wa sinema hii. Ila ukweli ni kwamba urafiki wao wa zamani umemezwa na chuki, siasa, dini, na visasi. Na kama huelewi kilichoendelea, kumbuka tu maneno ya mtaa:
“Wadogo wakichapana, mara nyingi ni kwa sababu wakubwa wanagombana.”