Iran: Nchi zilizopoteza raia katika ajali ya ndege zadai fidia

Iran: Nchi zilizopoteza raia katika ajali ya ndege zadai fidia

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mataifa yaliyopoteza raia katika ajali ya ndege ya Ukraine iliyodunguliwa na Iran yameitaka Tehran iwajibike kikamilifu, uchunguzi wa kimataifa uanzishwe na familia za wahanga zilipwe fidia.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Canada, Uingereza, Ukraine, Sweden, Uholanzi na Afghanistan wamekutana jijini London katika ubolozi wa Canada.

Mawaziri hao baada ya mkutano wao walitoa taarifa ya pamoja wakiitaka Iran ifanye uchunguzi wa kimataifa utakao kuwa huru na wazi hasa kwa mataifa yanayoomboleza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Francois-Philippe Champagne amesema wamekutana kutafuta uwajibikaji na haki kwa wahanga wa mkasa huo na kuongeza kuwa familia za wahanga hao zinataka majibu, jamii ya kimataifa inataka majibu na dunia nzima pia inasubiri majibu na kwamba hawatapumzika hadi watakapoyapata.

Watu wote 176 waliokuwa wameabiri ndege ya abiria ya Ukraine walipoteza maisha yao wakati ndege yao ilipodunguliwa na kombora muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomeini mjini Tehran tarehe 8 mwezi huu.
 
Ao nao wanawashwa! Ukraine si amesema wote walioua watalipwa fidia kwa familia zao! Na Iran ishatoa ripoti ya awali kuwa ndege waliitungua kwa makosa na msamaha wameomba! Sasa uchunguzi hupi wanauitaji tena? Au ndo wanataka kuuvaa uhanarakati kwa nguvu!
 
Jambo ambalo Iran halitolikubali ni uchunguzi wa kimataifa,kiusalama,uchunguzi wa kimataifa ni hatari ya pili kwa usalama wa taifa kwa sababu.
Hao wachunguzi wa kimataifa huwa hawafanyi kazi wanayopewa hadharani,wakifika huko hufanya kazi ya pili ya siri mno.
Iraq na Sadam Huseyn wanaelewa sana hilo...
 
Kabsa MKUU Nasidhanii Kama IRAN Anaweza Kubali Huo Upuuzi Wanaouwaza Hao Majamaa Maana Kama KUKIRI Kufanza Alishakiri Na Radhi Kaishaomba Kama Sijakosea MUHIMU Tararibu Tu Zafidia Zifanyike NO MORE.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima wachunguze kujua kama kweli ilikuwa bahati mbaya au kusudi. Kusudi au bahati mbaya ndo ita-determine kiwango na aina ya fidia. Ikibidi na vikwazo juu,huu upuuzi ambapo MTU hujifungia ndani na kuamua kufyatua mitambo ovyo,lazima ufike mwisho.
Iran keshakiri kuhusika kutungua hiyo ndege hakuna haja ya uchunguzi hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima wachunguze kujua kama kweli ilikuwa bahati mbaya au kusudi. Kusudi au bahati mbaya ndo ita-determine kiwango na aina ya fidia. Ikibidi na vikwazo juu,huu upuuzi ambapo MTU hujifungia ndani na kuamua kufyatua mitambo ovyo,lazima ufike mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app

Utaiwekea vikwazo gani vipya Iran? , vikwazo vyote vigumu unavyovijua wewe vimeshawekwa na Iran ipo inadunda tu.
Kama hao wazungu wanajiamini wanataka vita, hebu warushe risasi hata moja kwenye ardhi ya Iran wakione cha mtema kuni.
 
Mazungu yamehawa dharau Sana. Alipo uliwa muajemi generali na wale wairaq walioambatana nae hakuna aliyekemea kuwa Ni uharifu. Je nani auawe ili wakemee?
 
Hujaelewa kinachoendelea,Ukraine aliwapa kama rambirambi waliofiwa Ukraini ila alisema Iran ndiyo itatoa fidia pia hata kama ni bahati mbaya Fidia ni lazima ilipwe mfano nkuvunje mguu bahati mbaya Je mkiomba msamaha inatosha ww kupona maana kuna waliokufa na walikuwa tegemezi kwao sasa unawaachaje wale tegemezi?
Ao nao wanawashwa! Ukraine si amesema wote walioua watalipwa fidia kwa familia zao! Na Iran ishatoa ripoti ya awali kuwa ndege waliitungua kwa makosa na msamaha wameomba! Sasa uchunguzi hupi wanauitaji tena? Au ndo wanataka kuuvaa uhanarakati kwa nguvu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama vikwazo wanamuongezea na yeye akisema sitoi fidia hapo watamfanya nini ebu wajuzi niambieni.hapo sawasawa unanidai alafu unafunga biashara yangu alafu unataka nikulipe deni
 
Hakuna Atakae Kubali Uchubguzi Fidia Watalipwa Tu Hakuna Namna
Lazima wachunguze kujua kama kweli ilikuwa bahati mbaya au kusudi. Kusudi au bahati mbaya ndo ita-determine kiwango na aina ya fidia. Ikibidi na vikwazo juu,huu upuuzi ambapo MTU hujifungia ndani na kuamua kufyatua mitambo ovyo,lazima ufike mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vikwazo washa vizoea toka mwaka 1979 mpaka Leo

All Is Well In Turampet Voice[emoji23][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanachotaka siyo kufanya uchunguzi wa ajali,bali ni kuchunguza mambo ya anga ya Iran,Iran akilogwa akubali,imekula kwake.
IRAN Sio Mpuuzi MKUU Wanayoyawaza Wao Mwenzao Kaishayawaza Muda

Na kama ukiona kawaruhusu Basi Ujue Kaishaweka Mazingira Yake Salama Anajua Hatakama Watafanya Wanaoita Ukaguzi Hautamuathiri Katika Masuala Yake Ya USALAM

All Is Well In Turampet Voice[emoji4][emoji1][emoji2][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama vikwazo wanamuongezea na yeye akisema sitoi fidia hapo watamfanya nini ebu wajuzi niambieni.hapo sawasawa unanidai alafu unafunga biashara yangu alafu unataka nikulipe deni
Hawana lakumfanya Watalalamika tu ama waongeze tena vikwazo zaidi basi.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa hapo hajapingana na FIDIA Anapingana na UCHUNGUZI Jamaa washakiri Kuitungua Kinachotakiwa MAZINGIRA Yafidia Yaandaliwe Wafiwa Wapewe FIDIA Wanazostahili na Sidhanii Kama IRAN Kakataa Kulipa FIDIA Kwa Janga Alosababisha
Hujaelewa kinachoendelea,Ukraine aliwapa kama rambirambi waliofiwa Ukraini ila alisema Iran ndiyo itatoa fidia pia hata kama ni bahati mbaya Fidia ni lazima ilipwe mfano nkuvunje mguu bahati mbaya Je mkiomba msamaha inatosha ww kupona maana kuna waliokufa na walikuwa tegemezi kwao sasa unawaachaje wale tegemezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa wana MALENGO Yao Wanayo Yajua Nyuma Yapazia Ila Hawatafanikiwa Watafeli Tuu

All Is Well In Turampet Voice[emoji23][emoji16][emoji1][emoji2][emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom