IRAN - "Victim Card Strategy" Inawaumiza Kichwa Wazungu na Wazayuni wa Israel

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311

Victim Card Strategy ni nini?​

Victim Card Strategy (mbinu ya kujifanya mwathirika) ni mbinu ambapo mtu au kundi la watu hujifanya kuwa waathirika wa hali fulani au mazingira, kwa lengo la kupata huruma, uungwaji mkono, au kuepuka lawama.

1728018798601.png

KWA NINI IRAN HAIWEZI KUSHAMBULIWA NA MAREKANI NA WASHIRIKA WAKE?​

Iran Tayari yeye yupo na hoja zake za msingi ambazo alianza kuzitoa tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia. Hoja yake kuu ni kwamba mauaji ya wayahudi yaliyofanyika huko ulaya Responsible people ni wazungu kwahiyo wao walitakiwa wawatafutie wayahudi nchi yao huko huko Ulaya.

Hoja hii ya Irani haijawahi kujibiwa kokote, bali wao walilazimisha wayahudi wajengewe nchi katika ardhi ya Palestina

=> Baada ya kuangushwa kwa utawala wa kifalme wa Shah 1979, ambaye alikuwa karibu na Marekani, Iran ilijitangaza kuwa mwathirika wa uingiliaji wa nje. Iran inatumia kumbukumbu hizi kuonyesha kuwa inatetea uhuru wake dhidi ya ubeberu wa Marekani.

=> Iran imewekewa vikwazo vingi vya kiuchumi kwa sababu ya mpango wake wa nyuklia. Katika hili, Iran inadai kuwa ina haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani na inajiona kama taifa linalonyimwa haki hiyo na nchi zenye nguvu.

=> Iran mara kwa mara inadai kuwa wanasayansi wake wa nyuklia wanashambuliwa na nchi za Magharibi na washirika wao kama Israel, ikijitambulisha kuwa taifa ambalo linakandamizwa kimaendeleo kwa kuondolewa vipaji vyake.

=>Iran imejitambulisha kuwa mtetezi wa Wapalestina na Waislamu kwa ujumla kwa kusaidia vikundi vya Hezbollah na Hamas. Inaonyesha msaada wake kama juhudi za kuwakomboa Wapalestina kutoka kwa ukandamizaji wa Israel. Kwahiyo kuipiga Iran ni kumpiga mtetezi wa Waislam Duniani.

Iran inajenga picha ya kuwa taifa la kwanza linalopinga uwepo wa Israel, likiwakilisha sera zake kama juhudi za kuzuia upanuzi wa "ukoloni" wa Israel na Marekani. Katika hili, Iran inadai kuwa mwathirika wa njama za Israel, ambayo inaiweka katika hatari kubwa ya kushambuliwa kijeshi.

IRAN NI ILIATHILIKA WA MAENEO YAKE YA CAUCASUS KUCHUKULIWA NA URUSI​

Matukio haya yanahusiana sana na Vita vya Iran-Urusi vilivyopiganwa katika kipindi cha miaka ya 1804-1813 na 1826-1828.

1728020940076.png

Maeneo hayo ni kuanzia Azerbaijan mpaka Georgia yalikuwa sehemu ya Iran vita vilivyopiganwa. Hadi leo, kupoteza Caucasus ni suala linaloibua hisia kali nchini Iran, kwani maeneo haya yalikuwa sehemu ya himaya ya kihistoria ya Iran kwa karne nyingi. Hisia za kuwa waathirika wa upanuzi wa Urusi zimekuwa sehemu ya kumbukumbu ya kitaifa ya Iran.

ATHARI ZA MAREKANI NA MASHIRIKA YAKE WAKIIVAMIA IRAN NAYO ITAJITETEA KWA NAMNA GANI?​

Iran inaweza kujitetea kwa nguvu kubwa dhidi ya uvamizi wa Marekani na washirika wake, ikitumia mbinu za kijeshi, washirika wake wa eneo (proxy warfare), vita vya kiuchumi, na shambulio la kidiplomasia. Athari za uvamizi huo zitakuwa mbaya sio tu kwa Iran na Marekani, bali pia kwa kanda ya Mashariki ya Kati na dunia kwa ujumla, hasa kwa kuzingatia usumbufu katika soko la mafuta na hatari ya vita vya muda mrefu.

=> Iran inaweza kutumia vikosi vya wanamaji katika Ghuba ya Uajemi, ambayo ni njia muhimu ya kusafirishia mafuta. Kwa kushambulia meli za kibiashara au za kijeshi, Iran inaweza kuvuruga biashara ya mafuta duniani, hali inayoweza kusababisha ongezeko la bei ya mafuta na kupunguza uchumi wa dunia.

=> Itazuka vita kubwa ya kidini ambayo haijawahi kutokea tangu kuubwa kwa dunia hii. Watu watachinjana kwa kupigania dini. Amani itatoweka duniani kote. Nchi kama Indonesia, Sehemu ya Russia, na nchi nyingi za Kiislam zitaiunga mkono Iran. Kuivamia Iran ni risk kubwa mno katika dunia ya sasa.

=> Iran itaweza kulipua visima vya mafuta vinavyomilikiwa na wazungu huko Saudi Arabia, Qatar na UAE. Tayari Iran walishawahi kulipua Refinery za wazungu huko Saudia.

HAYO ANAYOYASEMA NETA NYAU NI SIASA TU HAYATEKELEZEKI​

Kutuma makombora kupiga Vinu vya Nyukilia vya Iran, Visima vya Mafuta na Refanery ndani ya Iran ni ndoto za mchana kweupe. Haya mambo ni almost Imposible. Neta Nyau hana uwezo wa kufanya hivyo. Mitambo ya Nyukilia ya Iran ipo chini ya ardhi ubali wa Mita 100. Maana yake unatakiwa usafirishe ndege ivuke Zagros Mountains Waajemi wamekuangalia tu. Na slaha ya kuweza kulipua mitambo ambayo ipo 100m chini ya Ardhi kwa sasa haipo.

1728022397854.png

HITIMISHO​

Taifa ambalo ni tishio kwa Marekani na washirika wake ni Iran. Iran yupo na victim card. Kwanza yeye ni Shia ambao ni Minority kwa Uislam. Pia yeye amejiweka ndiye mtetezi wa mataifa yote ya Kiislam. Kushambulia nchi hii risk zake ni nyingi mno.

KARIBUNI TUJADILIANE KWA STAHA
 
Nyau ni kibaraka tu msanii mkubwa kaingia nyumbani kwa pdidy. Juzi alikua anatetemeka kishenzi haamini wahuni wamepenya anaitumbukiza nchi yake kwenye vita visivyo na faida atabaki omba omba huku shughuli za uchumi zimesimama kisa ubabe usii na maana, muajemi hamuwezi wazungu sio wehu kutumia njia ya vikwazo
 
Wakiristo wa jf wa mbagala mbwa kachoka hawajaamka bado, wakija humu wataushambulia uislam utadhani hivi vita ni kati ya wakiristo na waislam.

Victim Card Strategy ni nini?​

Victim Card Strategy (mbinu ya kujifanya mwathirika) ni mbinu ambapo mtu au kundi la watu hujifanya kuwa waathirika wa hali fulani au mazingira, kwa lengo la kupata huruma, uungwaji mkono, au kuepuka lawama.

View attachment 3114765

KWA NINI IRAN HAIWEZI KUSHAMBULIWA NA MAREKANI NA WASHIRIKA WAKE?​

Iran Tayari yeye yupo na hoja zake za msingi ambazo alianza kuzitoa tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia. Hoja yake kuu ni kwamba mauaji ya wayahudi yaliyofanyika huko ulaya Responsible people ni wazungu kwahiyo wao walitakiwa wawatafutie wayahudi nchi yao huko huko Ulaya.

Hoja hii ya Irani haijawahi kujibiwa kokote, bali wao walilazimisha wayahudi wajengewe nchi katika ardhi ya Palestina

=> Baada ya kuangushwa kwa utawala wa kifalme wa Shah 1979, ambaye alikuwa karibu na Marekani, Iran ilijitangaza kuwa mwathirika wa uingiliaji wa nje. Iran inatumia kumbukumbu hizi kuonyesha kuwa inatetea uhuru wake dhidi ya ubeberu wa Marekani.

=> Iran imewekewa vikwazo vingi vya kiuchumi kwa sababu ya mpango wake wa nyuklia. Katika hili, Iran inadai kuwa ina haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani na inajiona kama taifa linalonyimwa haki hiyo na nchi zenye nguvu.

=> Iran mara kwa mara inadai kuwa wanasayansi wake wa nyuklia wanashambuliwa na nchi za Magharibi na washirika wao kama Israel, ikijitambulisha kuwa taifa ambalo linakandamizwa kimaendeleo kwa kuondolewa vipaji vyake.

=>Iran imejitambulisha kuwa mtetezi wa Wapalestina na Waislamu kwa ujumla kwa kusaidia vikundi vya Hezbollah na Hamas. Inaonyesha msaada wake kama juhudi za kuwakomboa Wapalestina kutoka kwa ukandamizaji wa Israel. Kwahiyo kuipiga Iran ni kumpiga mtetezi wa Waislam Duniani.
Iran inajenga picha ya kuwa taifa la kwanza linalopinga uwepo wa Israel, likiwakilisha sera zake kama juhudi za kuzuia upanuzi wa "ukoloni" wa Israel na Marekani. Katika hili, Iran inadai kuwa mwathirika wa njama za Israel, ambayo inaiweka katika hatari kubwa ya kushambuliwa kijeshi.

IRAN NI ILIATHILIKA WA MAENEO YAKE YA CAUCASUS KUCHUKULIWA NA URUSI​

Matukio haya yanahusiana sana na Vita vya Iran-Urusi vilivyopiganwa katika kipindi cha miaka ya 1804-1813 na 1826-1828.

View attachment 3114807

Maeneo hayo ni kuanzia Azerbaijan mpaka Georgia yalikuwa sehemu ya Iran vita vilivyopiganwa. Hadi leo, kupoteza Caucasus ni suala linaloibua hisia kali nchini Iran, kwani maeneo haya yalikuwa sehemu ya himaya ya kihistoria ya Iran kwa karne nyingi. Hisia za kuwa waathirika wa upanuzi wa Urusi zimekuwa sehemu ya kumbukumbu ya kitaifa ya Iran.

ATHARI ZA MAREKANI NA MASHIRIKA YAKE WAKIIVAMIA IRAN NAYO ITAJITETEA KWA NAMNA GANI?​

Iran inaweza kujitetea kwa nguvu kubwa dhidi ya uvamizi wa Marekani na washirika wake, ikitumia mbinu za kijeshi, washirika wake wa eneo (proxy warfare), vita vya kiuchumi, na shambulio la kidiplomasia. Athari za uvamizi huo zitakuwa mbaya sio tu kwa Iran na Marekani, bali pia kwa kanda ya Mashariki ya Kati na dunia kwa ujumla, hasa kwa kuzingatia usumbufu katika soko la mafuta na hatari ya vita vya muda mrefu.

=> Iran inaweza kutumia vikosi vya wanamaji katika Ghuba ya Uajemi, ambayo ni njia muhimu ya kusafirishia mafuta. Kwa kushambulia meli za kibiashara au za kijeshi, Iran inaweza kuvuruga biashara ya mafuta duniani, hali inayoweza kusababisha ongezeko la bei ya mafuta na kupunguza uchumi wa dunia.

=> Itazuka vita kubwa ya kidini ambayo haijawahi kutokea tangu kuubwa kwa dunia hii. Watu watachinjana kwa kupigania dini. Amani itatoweka duniani kote. Nchi kama Indonesia, Sehemu ya Russia, na nchi nyingi za Kiislam zitaiunga mkono Iran. Kuivamia Iran ni risk kubwa mno katika dunia ya sasa.

=> Iran itaweza kulipua visima vya mafuta vinavyomilikiwa na wazungu huko Saudi Arabia, Qatar na UAE. Tayari Iran walishawahi kulipua Refinery za wazungu huko Saudia.

HAYO ANAYOYASEMA NETA NYAU NI SIASA TU HAYATEKELEZEKI​

Kutuma makombora kupiga Vinu vya Nyukilia vya Iran, Visima vya Mafuta na Refanery ndani ya Iran ni ndoto za mchana kweupe. Haya mambo ni almost Imposible. Neta Nyau hana uwezo wa kufanya hivyo. Mitambo ya Nyukilia ya Iran ipo chini ya ardhi ubali wa Mita 100. Maana yake unatakiwa usafirishe ndege ivuke Zagros Mountains Waajemi wamekuangalia tu. Na slaha ya kuweza kulipua mitambo ambayo ipo 100m chini ya Ardhi kwa sasa haipo.
View attachment 3114811

HITIMISHO​

Taifa ambalo ni tishio kwa Marekani na washirika wake ni Iran. Iran yupo na victim card. Kwanza yeye ni Shia ambao ni Minority kwa Usislam. Pia yeye amejiweka ndiye mtetezi wa mataifa yote ya Kiislam. Kushambulia nchi hii risk zake ni nyingi mno.

KARIBUNI TUJADILIANE KWA STAHA
 
Unaamini ulichokiandika au umejiandikia tu ili na wewe uwe victim wa kutaka sympathy ya JF?Hivi ni kipi ulianza kukisikia kati ya Izraeli na Palestina kabla haujafikisha umri wa miaka saba?Je,unaamini kwamba Israeli haikuwepo hapo kabla na imeanzishwa miaka hiyo uliyoitaja ya 1948?Amka!
 
Kwa mantiki hiyo hata Israel anayo hiyo Victim card
Tayari Iran yupo na Upper Hand. Tangu kuisha kwa vita vya pili vya Dunia victims walikuwa Jews. Walikuwa wanalilia kupata eneno litakaloitwa nchi yao. Maana waliuliwa kwa wingi huko Ulaya.

Iran alitoa msimamo wake Tangu mwanzo kuwa. Wayahudi watafutiwe nchi yao huko huko Ulaya. Still Iran is a Victim.
 
Unaamini ulichokiandika au umejiandikia tu ili na wewe uwe victim wa kutaka sympathy ya JF?Hivi ni kipi ulianza kukisikia kati ya Izraeli na Palestina kabla haujafikisha umri wa miaka saba?Je,unaamini kwamba Israeli haikuwepo hapo kabla na imeanzishwa miaka hiyo uliyoitaja ya 1948?Amka!
Tuambie Taifa la Israel lilikuwepo kuanzia mwaka gani na likakoma kuwepo mwaka gani na likaanzishwa tena?

Toa Maelezo acha mipasho.
 
Kwa hiyo wewe unaamini kila unachoandikiwa?Acha u-hopeless!
Hasira za nini mdogo wangu. Naenda na wewe taratibu tu.
In 1920, the League of Nations granted Britain the mandate to govern Palestine, leading to the subsequent period of British administration.

Mpaka hapa Taifa la Israel halipo
 
Hasira za nini mdogo wangu. Naenda na wewe taratibu tu.
In 1920, the League of Nations granted Britain the mandate to govern Palestine, leading to the subsequent period of British administration.
Bwana mkubwa(ingawa ni mtoto kiakili)unadhani kwa nini Uingereza ilipewa mamlaka kuidhamini Palestina mwaka huo?
 
Tunaendelea taratibu kijana. Maana inaonekana wewe ni mweupe kichwani. Hata Tanganyika ilikuwa chini ya Uingereza baada ya vita vya kwanza vya dunia.

Baada ya Ottoman Empire kukoma ndio Eneo la Palestine likawa Chini ya Waingereza hujui hilo?

1728024911904.png
 
Back
Top Bottom