Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Victim Card Strategy ni nini?
Victim Card Strategy (mbinu ya kujifanya mwathirika) ni mbinu ambapo mtu au kundi la watu hujifanya kuwa waathirika wa hali fulani au mazingira, kwa lengo la kupata huruma, uungwaji mkono, au kuepuka lawama.KWA NINI IRAN HAIWEZI KUSHAMBULIWA NA MAREKANI NA WASHIRIKA WAKE?
Iran Tayari yeye yupo na hoja zake za msingi ambazo alianza kuzitoa tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia. Hoja yake kuu ni kwamba mauaji ya wayahudi yaliyofanyika huko ulaya Responsible people ni wazungu kwahiyo wao walitakiwa wawatafutie wayahudi nchi yao huko huko Ulaya.Hoja hii ya Irani haijawahi kujibiwa kokote, bali wao walilazimisha wayahudi wajengewe nchi katika ardhi ya Palestina
=> Baada ya kuangushwa kwa utawala wa kifalme wa Shah 1979, ambaye alikuwa karibu na Marekani, Iran ilijitangaza kuwa mwathirika wa uingiliaji wa nje. Iran inatumia kumbukumbu hizi kuonyesha kuwa inatetea uhuru wake dhidi ya ubeberu wa Marekani.
=> Iran imewekewa vikwazo vingi vya kiuchumi kwa sababu ya mpango wake wa nyuklia. Katika hili, Iran inadai kuwa ina haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani na inajiona kama taifa linalonyimwa haki hiyo na nchi zenye nguvu.
=> Iran mara kwa mara inadai kuwa wanasayansi wake wa nyuklia wanashambuliwa na nchi za Magharibi na washirika wao kama Israel, ikijitambulisha kuwa taifa ambalo linakandamizwa kimaendeleo kwa kuondolewa vipaji vyake.
=>Iran imejitambulisha kuwa mtetezi wa Wapalestina na Waislamu kwa ujumla kwa kusaidia vikundi vya Hezbollah na Hamas. Inaonyesha msaada wake kama juhudi za kuwakomboa Wapalestina kutoka kwa ukandamizaji wa Israel. Kwahiyo kuipiga Iran ni kumpiga mtetezi wa Waislam Duniani.
Iran inajenga picha ya kuwa taifa la kwanza linalopinga uwepo wa Israel, likiwakilisha sera zake kama juhudi za kuzuia upanuzi wa "ukoloni" wa Israel na Marekani. Katika hili, Iran inadai kuwa mwathirika wa njama za Israel, ambayo inaiweka katika hatari kubwa ya kushambuliwa kijeshi.
IRAN NI ILIATHILIKA WA MAENEO YAKE YA CAUCASUS KUCHUKULIWA NA URUSI
Matukio haya yanahusiana sana na Vita vya Iran-Urusi vilivyopiganwa katika kipindi cha miaka ya 1804-1813 na 1826-1828.Maeneo hayo ni kuanzia Azerbaijan mpaka Georgia yalikuwa sehemu ya Iran vita vilivyopiganwa. Hadi leo, kupoteza Caucasus ni suala linaloibua hisia kali nchini Iran, kwani maeneo haya yalikuwa sehemu ya himaya ya kihistoria ya Iran kwa karne nyingi. Hisia za kuwa waathirika wa upanuzi wa Urusi zimekuwa sehemu ya kumbukumbu ya kitaifa ya Iran.
ATHARI ZA MAREKANI NA MASHIRIKA YAKE WAKIIVAMIA IRAN NAYO ITAJITETEA KWA NAMNA GANI?
Iran inaweza kujitetea kwa nguvu kubwa dhidi ya uvamizi wa Marekani na washirika wake, ikitumia mbinu za kijeshi, washirika wake wa eneo (proxy warfare), vita vya kiuchumi, na shambulio la kidiplomasia. Athari za uvamizi huo zitakuwa mbaya sio tu kwa Iran na Marekani, bali pia kwa kanda ya Mashariki ya Kati na dunia kwa ujumla, hasa kwa kuzingatia usumbufu katika soko la mafuta na hatari ya vita vya muda mrefu.=> Iran inaweza kutumia vikosi vya wanamaji katika Ghuba ya Uajemi, ambayo ni njia muhimu ya kusafirishia mafuta. Kwa kushambulia meli za kibiashara au za kijeshi, Iran inaweza kuvuruga biashara ya mafuta duniani, hali inayoweza kusababisha ongezeko la bei ya mafuta na kupunguza uchumi wa dunia.
=> Itazuka vita kubwa ya kidini ambayo haijawahi kutokea tangu kuubwa kwa dunia hii. Watu watachinjana kwa kupigania dini. Amani itatoweka duniani kote. Nchi kama Indonesia, Sehemu ya Russia, na nchi nyingi za Kiislam zitaiunga mkono Iran. Kuivamia Iran ni risk kubwa mno katika dunia ya sasa.
=> Iran itaweza kulipua visima vya mafuta vinavyomilikiwa na wazungu huko Saudi Arabia, Qatar na UAE. Tayari Iran walishawahi kulipua Refinery za wazungu huko Saudia.
HAYO ANAYOYASEMA NETA NYAU NI SIASA TU HAYATEKELEZEKI
Kutuma makombora kupiga Vinu vya Nyukilia vya Iran, Visima vya Mafuta na Refanery ndani ya Iran ni ndoto za mchana kweupe. Haya mambo ni almost Imposible. Neta Nyau hana uwezo wa kufanya hivyo. Mitambo ya Nyukilia ya Iran ipo chini ya ardhi ubali wa Mita 100. Maana yake unatakiwa usafirishe ndege ivuke Zagros Mountains Waajemi wamekuangalia tu. Na slaha ya kuweza kulipua mitambo ambayo ipo 100m chini ya Ardhi kwa sasa haipo.HITIMISHO
Taifa ambalo ni tishio kwa Marekani na washirika wake ni Iran. Iran yupo na victim card. Kwanza yeye ni Shia ambao ni Minority kwa Uislam. Pia yeye amejiweka ndiye mtetezi wa mataifa yote ya Kiislam. Kushambulia nchi hii risk zake ni nyingi mno.KARIBUNI TUJADILIANE KWA STAHA