Iran yaishambulia Israel kwa makombora
Mwisho wa Iran unakuja muda mfupi. Iran ilikuwa kikwazo kwa nchi za magharibi hapo middle east sasa naona wamagharibi walishapata sababu ya kuiangamiza Iran.
Iran inaenda kubutuliwa kama Iraq na haitasimama tena pia natural resources zao zitamilikiwa na makampuni ya magharibi.
Magharibi wanaenda kuweka kibaraka wao aiongoze iran
 
Pia kuna airbase pale ya Israel.
Na madhara yametokea japo wanasema ni ya kawaida hivyo baadhi ya makombora yamepita.
Maana wanasema kiasi kikubwa wamelipua kiasi kidogo yamepenya.
Hata likipenya moja ni kipigo na jibu la uchokozi wao
 
Mwisho wa Iran unakuja muda mfupi. Iran ilikuwa kikwazo kwa nchi za magharibi hapo middle east sasa naona wamagharibi walishapata sababu ya kuiangamiza Iran.
Iran inaenda kubutuliwa kama Iraq na haitasimama tena pia natural resources zao zitamilikiwa na makampuni ya magharibi.
Magharibi wanaenda kuweka kibaraka wao aiongoze iran
 
Mara nyingi na mara zote Huwa nawaambia kwamba kinachoitwa Mifumo ya anga ni matakataka.

Umeshindwa Kuzuia drones ,utazuia bomu?
 
Tatizo lako ni kwamba unachukulia hili suala kiushabiki.

Baada ya Israeli kushambulia na kuvunjavunja jengo la ubalozi kule Damascus, Iran wameketi na kuwa na plan ya ni targets zipi watazishughulikia.

Nyuma ya pazia Iran, Marekani, Jordan na Syria wote wazungumza na kuambizana namna ufanisi wa makombora na UAVs za Iran zitakwenda Israeli bila kuharibu targets zisizokusudiwa. Ukumbuke kwamba Iran bila kutumia anga za Iraq na Syria hana uwezo wa kuishamblia Israeli na ndo sababu ya kuwa vikosi vya Hezbollah, wahuthi na vingine ndani ya Syria na Iraq.

Ndo maana Israeli amekuwa akishambulia kambi na vituo vya kijeshi vya vikundi hivi bila mafanikio na ndo sababu kubwa ya kushambulia jengo la ubalozi wa Iran pale Damascus kwani majasusi wa CIA, Mossad na wa Jordan waligundua kuwa wale majenerali wa Iran ambao ndo wamekuwa wakitoa mafunzo kwa Hezbollah na vikundi vingine, siku ile walikwenda pale ubalozini kufanya kikao.

Nimesema mara nyingi hapa kwamba vita ya hawa jamaa wakubwa wa ulimwengu si vita ya kule Congo, bali ni vita iliyo na matumizi makubwa ya teknolojia na zana za kisasa kabisa ambazo hata nchi moja ya Afrika haiwezi kuwa nazo kutokana na gharama zake.

Hivyo basi, majasusi wa Iran tayari waliandaa mashambulizi dhidi ya targets ndani ya Israeli na hichi ndicho wanokifanya kwa sasa.

Marekani pamoja na kuisaidia Israeli kujilinda kwa ile "Iron Dome" hapohapo wafanya analysis ya ni aina zipi za UAVs Iran ametumia, umbali zilotumia na "impact" yake zifikapo chini. Kisha baadae watakuja na mbinu mpya za kuboresha "mitigation" juu ya mashambulizi mengine.

Ukumbuke pia kwamba hizo UAVs za Shaheed pia zasadia kuweka cover kwa makombora hivyo kuwezesha makombora hayo kukwepa mfumo wa kujilinda, hivyo analysis pia itaangalia kitu hichi.

Iran leo wametoa sababu za kufanya mashambulizi yake na wametumia Article 51 ya UN charter ambayo inaipa uwezo nchi kujibu mapigo pale inaposhambuliwa ndani ya eneo lake. Kwa maana hiyo ni kwamba kushambuliwa jengo la ubalozi wa Iran mjini Damascus ni sawa na kuishambulia Iran yenyewe.

Israeli walifahamu kuwa Iran itajibu mapigo na ndo maana wametumia muda mwingi kujiandaa.

Hivyo basi, tunapojadili haya masuala tuepuke ushabiki na tuombe wakubwa hawa wa dunia akili zitulie ili wasilete vita ambayo itagharimu maisha ya watu wengine ambao hawahusiki.
kwa vile umejenga hoja kama mtu timamu( maana humu wachambuzi wasio na mihemko wamekuwa adimu), unadhan nani atakuwa mhanga zaid wa hali hii
 
Mwisho wa Iran unakuja muda mfupi. Iran ilikuwa kikwazo kwa nchi za magharibi hapo middle east sasa naona wamagharibi walishapata sababu ya kuiangamiza Iran.
Iran inaenda kubutuliwa kama Iraq na haitasimama tena pia natural resources zao zitamilikiwa na makampuni ya magharibi.
Magharibi wanaenda kuweka kibaraka wao aiongoze iran
Siyo rahisi hivyo.
Unafikiri walishindwa nini kuivamia au kuibutua miaka yote hiyo?
 
Hahahaaa acha kudanganya umma hakuna mahali hata kidogo Israel amesema atalopiza kisasi wameingiwa uoga na hofu kuona makombora yametua kwenye target licha ya kuanza kudunguliwa Jordan.

Marekani amesema hawezi kujihusisha na kulipa kisasi kwa Iran badala yake atatumia Diplomasia kutatua mzozo huu.

Tupo tunafuatilia Al Jazeera, CNN ,BBC na vyombo vingine vya habari hakuna kauli ya kulipa kisasi aliyoitoa Mzayuni.

Iran amesema hii ni rasharasha anasubiri Mazayuni wajibu mapigo halafu sasa Muajemi ashushe moto kamili.
CNN ya bonyokwa? Au Aljazeera ya kwa Mpalange labda
 
LIVE UPDATES; MBASHARA SHAMBULIZI LA IRAN DHIDI YA ISRAEL
Biden amaliza kikao na kutoa ujumbe huo: " I just met with my national security team for an update on Iran’s attacks against Israel. Our commitment to Israel’s security against threats from Iran and its proxies is ironclad."


IDF kuanza kujibu shambulizi la Iran muda wowote kuanzia sasa

Marakani yaingia rasmi kwenye vita

Makombora drones zaidi ya 100 za Iran zalipuliwa zikiwa angani kabla ya kuingia anga la Israel


Jeshi la Syria lajiweka katika hali ya juu ya tahadhari

Israel yaishambuliwa kila kona
WaHouthi waishambulia kwa drones kutokea Yemen

Magaidi wa Hezbollah waishambulia kutokea Lebanon


Iran yasema itaishambulia nchi yeyote itakayoruhusu anga lake kutumiwa na Israel

Rais Biden aitisha kikao cha dharula muda huu na washauri wake wa Usalama

Makombora yaliyorushwa kuelekea Israel yafikia 500

Rais Joe Biden asema watailinda na kuiunga mkono Israel



Waziri Mkuu Benjamin Netanyau aongoza Kikao cha dharula cha Baraza la mawaziri kwenye kambi ya kijeshi ya Kirya iliyopo Tel Aviv

Uingereza yalaani shambulizi la Iran

Lebanon yafunga anga lake usiku huu

Anga ya Israel kufungwa kuanzia saa 6:30 usiku kwa saa za Afrika mashariki

Israel yasema jumla ya mashambulizi ya drones 100 yamerushwa na Iran kuelekea Israel

Iran yafanya shambulizi cyberattack kwenye mfumo ulinzi wa IDF

Iran yathibitisha kuishambulia Israel

Jeshi la Israel ( IDF) limeanza kutungua drones zilizoingia kwenye anga ya Jordan na Syria

Msemaji wa IDF Jenerali Daniel Hagari amethibitisha nchi yake kushambuliwa na iran

Itachukua takribani masaa 9 makombora hayo ( drones) kuifikia Israel

Tayari makombora drones hayo yameshaingia kwenye anga ya Iraq

Mfumo wa GPS "wavurugwa" kuiwezesha Israel kuyanasa au kuyatungua makombora hayo

Ving'ora vya tahadhari vitapigwa mara TU makombora hayo yatakapoingia anga la Israel


Wadau hamjamboni nyote?

Hatimaye Serikali ya Iran imeamua kulipiza kisasi Kwa Israel kwa kuanza kurusha makombora ambayo yapo njiani na yanayorajiwa kuchukua masaa kadhaa kabla ya kutua nchini humo

Taarifa kamili hapo chini

Times of Israel


Report: Iran begins attack on Israel, launching dozens of drones that’ll take hours to arrive​

Today, 10:48 pm
Illustrative: Iranians attend the funeral procession for seven Islamic Revolutionary Guard Corps members killed in a strike in Syria, which Iran blamed on Israel, in Tehran on April 5, 2024. (Atta Kenare/AFP)

Summary​

  1. Iran has launched dozens of drones and missiles at Israel in a retaliatory attack
  2. Israel has said the attack could take some hours to arrive, while Prime Minister Benjamin Netanyahu said the country is "ready for any scenario"
  3. Iran had warned that Israel would be "punished" for a strike on its consulate in Syria on 1 April
  4. Seven Revolutionary Guards, including two generals, and six Syrians were killed in the Damascus attack
  5. Israel has acknowledged carrying out hundreds of strikes in recent years on targets in Syria that it says are linked to Iran but has not claimed the Damascus strike
  6. President Biden has promised what he called "ironclad" support for Israel, saying the US will "do all we can to protect Israel's security"
  7. Iran had avoided direct confrontation with Israel during the Israel-Hamas conflict, but the Damascus attack was seen as a serious escalation
Mungu ibariki Israel


.


Huwa mnashangaza sana mnapotuletea mada

Umeandika kuwa Iran yaishambulia Israel kumbe hata bado hawajafanikiwa na drones hazijakaribia hata kufika katika anga la Israel...

Ukiulizwa walivyoshambulia wameua watu wangapi utajibu nini?

Hapo ni wamejaribu kuishambulia sio Wameishambulia
 
Ujasiri wa Iran umeifanya Israel inywee kiaina tofauti na wengi tulivyotaraji kuwa ikipigwa kweli na Iran itarusha mvua ya makombora Tehran papo kwa papo.
Kitisho cha vita vikubwa zaidi kiko wazi baada ya Iran kuiambia Marekani ikae mbali katika vita vyake na Israel.
Baada ya mashambulio ya jana mpaka kwenye kambi za jeshi za Tel Aviv,Iran imesema mpaka hapo imefunga ukurasa wake wa mwanzo wa vita.Inasubiri iwapo Israel itajibu na wao waendeleze ukurasa mwengine mpana zaidi
Muajemi hatanii akiahidi ankulipa lazima akulipe ipasavyo.
 
Hahahaaa acha kudanganya umma hakuna mahali hata kidogo Israel amesema atalopiza kisasi wameingiwa uoga na hofu kuona makombora yametua kwenye target licha ya kuanza kudunguliwa Jordan.

Marekani amesema hawezi kujihusisha na kulipa kisasi kwa Iran badala yake atatumia Diplomasia kutatua mzozo huu.

Tupo tunafuatilia Al Jazeera, CNN ,BBC na vyombo vingine vya habari hakuna kauli ya kulipa kisasi aliyoitoa Mzayuni.

Iran amesema hii ni rasharasha anasubiri Mazayuni wajibu mapigo halafu sasa Muajemi ashushe moto kamili.

IDF hapo wamesema nini? Kobaz, hiyo CNN yako au hujui Biden kasema atai support Israel hadi mwisho wa vita hii, na akatumia support ya US kwa Israel is Ironclad, unajua maana yake?


View: https://youtu.be/Cg3YMWcjLI4?si=3bqw_BpJY1sB4Y8y

IMG_2587.png
 
Back
Top Bottom