Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata likipenya moja ni kipigo na jibu la uchokozi waoPia kuna airbase pale ya Israel.
Na madhara yametokea japo wanasema ni ya kawaida hivyo baadhi ya makombora yamepita.
Maana wanasema kiasi kikubwa wamelipua kiasi kidogo yamepenya.
Hata wakikaa miaka 50, Israel ikishambulia Iran, Iran itajibu!Bado upo kwenye fikra za mwaka 47..vita ni Mipango sio unapigana Tu kama mjinga angalia Toka Israel wameua Yule kiongozi wa Iran ni zaidi ya wiki mbili ndiyo tinaona wanajibu.
Hapo inatosha.Kama hawataki vita watulie.Retaliation na counter attacks siyo Vita ..
Huo uhakika umeutoa kwa kuthibitisha wapi?Hata wakikaa miaka 50, Israel ikishambulia Iran, Iran itajibu!
Kamikaze drones siyo missiles zitakazo tumia muda huo.Mkuu sidhani kama makombora yanahitaji masaa kutoka Iran mpaka Israel.
kwa vile umejenga hoja kama mtu timamu( maana humu wachambuzi wasio na mihemko wamekuwa adimu), unadhan nani atakuwa mhanga zaid wa hali hiiTatizo lako ni kwamba unachukulia hili suala kiushabiki.
Baada ya Israeli kushambulia na kuvunjavunja jengo la ubalozi kule Damascus, Iran wameketi na kuwa na plan ya ni targets zipi watazishughulikia.
Nyuma ya pazia Iran, Marekani, Jordan na Syria wote wazungumza na kuambizana namna ufanisi wa makombora na UAVs za Iran zitakwenda Israeli bila kuharibu targets zisizokusudiwa. Ukumbuke kwamba Iran bila kutumia anga za Iraq na Syria hana uwezo wa kuishamblia Israeli na ndo sababu ya kuwa vikosi vya Hezbollah, wahuthi na vingine ndani ya Syria na Iraq.
Ndo maana Israeli amekuwa akishambulia kambi na vituo vya kijeshi vya vikundi hivi bila mafanikio na ndo sababu kubwa ya kushambulia jengo la ubalozi wa Iran pale Damascus kwani majasusi wa CIA, Mossad na wa Jordan waligundua kuwa wale majenerali wa Iran ambao ndo wamekuwa wakitoa mafunzo kwa Hezbollah na vikundi vingine, siku ile walikwenda pale ubalozini kufanya kikao.
Nimesema mara nyingi hapa kwamba vita ya hawa jamaa wakubwa wa ulimwengu si vita ya kule Congo, bali ni vita iliyo na matumizi makubwa ya teknolojia na zana za kisasa kabisa ambazo hata nchi moja ya Afrika haiwezi kuwa nazo kutokana na gharama zake.
Hivyo basi, majasusi wa Iran tayari waliandaa mashambulizi dhidi ya targets ndani ya Israeli na hichi ndicho wanokifanya kwa sasa.
Marekani pamoja na kuisaidia Israeli kujilinda kwa ile "Iron Dome" hapohapo wafanya analysis ya ni aina zipi za UAVs Iran ametumia, umbali zilotumia na "impact" yake zifikapo chini. Kisha baadae watakuja na mbinu mpya za kuboresha "mitigation" juu ya mashambulizi mengine.
Ukumbuke pia kwamba hizo UAVs za Shaheed pia zasadia kuweka cover kwa makombora hivyo kuwezesha makombora hayo kukwepa mfumo wa kujilinda, hivyo analysis pia itaangalia kitu hichi.
Iran leo wametoa sababu za kufanya mashambulizi yake na wametumia Article 51 ya UN charter ambayo inaipa uwezo nchi kujibu mapigo pale inaposhambuliwa ndani ya eneo lake. Kwa maana hiyo ni kwamba kushambuliwa jengo la ubalozi wa Iran mjini Damascus ni sawa na kuishambulia Iran yenyewe.
Israeli walifahamu kuwa Iran itajibu mapigo na ndo maana wametumia muda mwingi kujiandaa.
Hivyo basi, tunapojadili haya masuala tuepuke ushabiki na tuombe wakubwa hawa wa dunia akili zitulie ili wasilete vita ambayo itagharimu maisha ya watu wengine ambao hawahusiki.
Siyo rahisi hivyo.Mwisho wa Iran unakuja muda mfupi. Iran ilikuwa kikwazo kwa nchi za magharibi hapo middle east sasa naona wamagharibi walishapata sababu ya kuiangamiza Iran.
Iran inaenda kubutuliwa kama Iraq na haitasimama tena pia natural resources zao zitamilikiwa na makampuni ya magharibi.
Magharibi wanaenda kuweka kibaraka wao aiongoze iran
Nimeuthibisha leo, baada ya Iran kuishambulia Israel kwa mibomu kibwena!Huo uhakika umeutoa kwa kuthibitisha wapi?
CNN ya bonyokwa? Au Aljazeera ya kwa Mpalange labdaHahahaaa acha kudanganya umma hakuna mahali hata kidogo Israel amesema atalopiza kisasi wameingiwa uoga na hofu kuona makombora yametua kwenye target licha ya kuanza kudunguliwa Jordan.
Marekani amesema hawezi kujihusisha na kulipa kisasi kwa Iran badala yake atatumia Diplomasia kutatua mzozo huu.
Tupo tunafuatilia Al Jazeera, CNN ,BBC na vyombo vingine vya habari hakuna kauli ya kulipa kisasi aliyoitoa Mzayuni.
Iran amesema hii ni rasharasha anasubiri Mazayuni wajibu mapigo halafu sasa Muajemi ashushe moto kamili.
Vita siyo kama kusutana akina mama wauza vitumbua mtaani.Nimeuthibisha leo, baada ya Iran kuishambulia Israel kwa mibomu kibwena!
Huwa mnashangaza sana mnapotuletea madaLIVE UPDATES; MBASHARA SHAMBULIZI LA IRAN DHIDI YA ISRAEL
Biden amaliza kikao na kutoa ujumbe huo: " I just met with my national security team for an update on Iran’s attacks against Israel. Our commitment to Israel’s security against threats from Iran and its proxies is ironclad."
IDF kuanza kujibu shambulizi la Iran muda wowote kuanzia sasa
Marakani yaingia rasmi kwenye vita
Makombora drones zaidi ya 100 za Iran zalipuliwa zikiwa angani kabla ya kuingia anga la Israel
Jeshi la Syria lajiweka katika hali ya juu ya tahadhari
Israel yaishambuliwa kila kona
WaHouthi waishambulia kwa drones kutokea Yemen
Magaidi wa Hezbollah waishambulia kutokea Lebanon
Iran yasema itaishambulia nchi yeyote itakayoruhusu anga lake kutumiwa na Israel
Rais Biden aitisha kikao cha dharula muda huu na washauri wake wa Usalama
Makombora yaliyorushwa kuelekea Israel yafikia 500
Rais Joe Biden asema watailinda na kuiunga mkono Israel
Waziri Mkuu Benjamin Netanyau aongoza Kikao cha dharula cha Baraza la mawaziri kwenye kambi ya kijeshi ya Kirya iliyopo Tel Aviv
Uingereza yalaani shambulizi la Iran
Lebanon yafunga anga lake usiku huu
Anga ya Israel kufungwa kuanzia saa 6:30 usiku kwa saa za Afrika mashariki
Israel yasema jumla ya mashambulizi ya drones 100 yamerushwa na Iran kuelekea Israel
Iran yafanya shambulizi cyberattack kwenye mfumo ulinzi wa IDF
Iran yathibitisha kuishambulia Israel
Jeshi la Israel ( IDF) limeanza kutungua drones zilizoingia kwenye anga ya Jordan na Syria
Msemaji wa IDF Jenerali Daniel Hagari amethibitisha nchi yake kushambuliwa na iran
Itachukua takribani masaa 9 makombora hayo ( drones) kuifikia Israel
Tayari makombora drones hayo yameshaingia kwenye anga ya Iraq
Mfumo wa GPS "wavurugwa" kuiwezesha Israel kuyanasa au kuyatungua makombora hayo
Ving'ora vya tahadhari vitapigwa mara TU makombora hayo yatakapoingia anga la Israel
Wadau hamjamboni nyote?
Hatimaye Serikali ya Iran imeamua kulipiza kisasi Kwa Israel kwa kuanza kurusha makombora ambayo yapo njiani na yanayorajiwa kuchukua masaa kadhaa kabla ya kutua nchini humo
Taarifa kamili hapo chini
Times of Israel
Report: Iran begins attack on Israel, launching dozens of drones that’ll take hours to arrive
Today, 10:48 pm
Summary
Mungu ibariki Israel
- Iran has launched dozens of drones and missiles at Israel in a retaliatory attack
- Israel has said the attack could take some hours to arrive, while Prime Minister Benjamin Netanyahu said the country is "ready for any scenario"
- Iran had warned that Israel would be "punished" for a strike on its consulate in Syria on 1 April
- Seven Revolutionary Guards, including two generals, and six Syrians were killed in the Damascus attack
- Israel has acknowledged carrying out hundreds of strikes in recent years on targets in Syria that it says are linked to Iran but has not claimed the Damascus strike
- President Biden has promised what he called "ironclad" support for Israel, saying the US will "do all we can to protect Israel's security"
- Iran had avoided direct confrontation with Israel during the Israel-Hamas conflict, but the Damascus attack was seen as a serious escalation
.
![]()
Wote.kwa vile umejenga hoja kama mtu timamu( maana humu wachambuzi wasio na mihemko wamekuwa adimu), unadhan nani atakuwa mhanga zaid wa hali hii
Muajemi hatanii akiahidi ankulipa lazima akulipe ipasavyo.Ujasiri wa Iran umeifanya Israel inywee kiaina tofauti na wengi tulivyotaraji kuwa ikipigwa kweli na Iran itarusha mvua ya makombora Tehran papo kwa papo.
Kitisho cha vita vikubwa zaidi kiko wazi baada ya Iran kuiambia Marekani ikae mbali katika vita vyake na Israel.
Baada ya mashambulio ya jana mpaka kwenye kambi za jeshi za Tel Aviv,Iran imesema mpaka hapo imefunga ukurasa wake wa mwanzo wa vita.Inasubiri iwapo Israel itajibu na wao waendeleze ukurasa mwengine mpana zaidi
Hahahaaa acha kudanganya umma hakuna mahali hata kidogo Israel amesema atalopiza kisasi wameingiwa uoga na hofu kuona makombora yametua kwenye target licha ya kuanza kudunguliwa Jordan.
Marekani amesema hawezi kujihusisha na kulipa kisasi kwa Iran badala yake atatumia Diplomasia kutatua mzozo huu.
Tupo tunafuatilia Al Jazeera, CNN ,BBC na vyombo vingine vya habari hakuna kauli ya kulipa kisasi aliyoitoa Mzayuni.
Iran amesema hii ni rasharasha anasubiri Mazayuni wajibu mapigo halafu sasa Muajemi ashushe moto kamili.