SA, UK and EU kama ilivyo Houth na Hezbollah kwa Iran. Wanafanyia kazi wakubwa wakiwa mgongoni , wenyewe hamna kitu"
Huja quote vizuri, hayo ni maneno yangu si yako
Ila hizi akili, yaani unalinganisha Israel as a sovereign state na vikundi vya kigaidi (Houthi and Hezbollah) seriously [emoji848].
Nimekueleza Iran inatumia Proxy kama Houth na Hezbollah kufanya mashambulizi wanakotaka.
Marekani na EU wanatumia Israel kushambulia wanakotaka kama ilivyo kwa Iran
Saddam Hussein aliondolewa kwa hiyana tu, hakuna silaha ya nyuklia hata moja iliyopatikana.
Gen Collin Powell ameenda kaburini akijuta kuonyesha uongo UN.
Kilichosababisha Iraq na Saddam Kushambuliwa ni tukio la 1988 kama sikosei ambapo Saddam alituma kombora la SCUD likatua Israel. Hiyo ikawa ni ishara kwamba Iraq ni tishio.
Kama utakumbuka Israel ilishambuliwa Iraq kwa kudai ni mtambo wa Nuclear.
Israel haitaki Iran iwe na Nuclear Kwa miaka mingi Israel ilishawishi na hata kumshawishi Obama alipue mitambo ya nyuklia Iran, lakini USA inahofia vita kubwa mashariki ya kati.
USA ina kumbu kumbu ya Iraq na Afghanistan ya miaka 20, hivyo kuingia kichwa kichwa kwa Taifa kama Iran
Siku zinavyosonga Iran inakuwa tishio kwa Israel na nchi za Magharibi hazitaki
Jiulize kwanini Israel ina silaha za Nuclear lakini nchi za mgaharibihazitaki Iran iwe nazo
Au mi ndio sielewi?, Au kuna nchi duniani ina ubalozi wa Hezbollah na hatujui, tuweni serious basi, mahaba yanaruhusiwa lakini yasizidi Uwezo wa kufikiria sasa Daa aisee ni huzuni
Rudi usome nilichokieleza. Lazima utambue kibaraka si mtu hata mataifa yanakuwa vibaraka.
Uliaminishwa na nani wakati historia inaongea mkuu, si walisema bila support hawezi lipa kisasi, mbona USA ameshatangaza kutosupport kama atarespond, na still amerespond kwa nchi tena tatu ikiwemo ile inayoongozwa Na Islamic regime.
Hapa unaonyesha kiwango duni cha uelewa. USA kutangaza unaamini wala hujiulizi ni kwa vipi.
USA unayosema wiki hii imeongeza misaada ya sailaha na fedha kwa Israel. Kwani support unaelewa ni nini?
Jiulize kwanini G7 wamekutana kwa dharura na kuiwekea Iran Vikwazo
Kwanini kamanda wa central command ya pentagon na team zake wapo Israel
Zile fleet carriers zinafanya nini mediterrenean
Hivi nani mwenye ufunguo wa GPS na space communication duniani na kwanini USA ilizima GPS
USA, EU na UK zilikataa kulaani shambulio la Israel kwa Iran kule Syria, lakini inalaani shambulio la Iran! hujiulizi tu
Tatizo lako ukiangalia TV au kusomewa habari unabeba tu huna muda wa kutafuta na kusoma habari nyingine
Juzi Alhamisi USA imepiga Veto UN , unajua ni kwanini. Yaani ndio Taifa pekee linalokingia kifua Israel
Niambie ni azimio gani la UN linalohusu Iran au Palestina limeungwa mkono na USA
Halafu USA ikisema hai support huoni kama ni uongo kwasababu Biden anakabiliwa na upinzani mkubwa ndani ya chama chake. Yaani unadanganywa na wewe unabeba tu hata kutafuna kidogo huwezi! poor you
Nchi za EU, UK na USA wanatoa msaada wa kijeshi kwa Israel. Kila nchi ilishiriki , EU wanasema, UK wanasema ,USA wanasema na Israel inawashauri. Ni wewe tu uliyebaki
Nchi za kiarabu mbili, Jordan na Saudi Arabia zilishiriki pia. Jordan tunajua ni kwanini na Saudia tunajua pia
Saudi Arabia ilifichwa kwa jina la 'unknown Arab nation' wenye akili tulijua, sijui kama uliwahi kufikiri hata kidogo
Ngoja nikupe shule, baada ya Arab Spring ufalme wa Saudia ulitikisika sana. Springi ilianzia Tunisia kisha Egypt.
Huko kuna Salafi na Wahabi na inasemekana Shia wa Iran walikuwa nyuma ya yote si kwasababu ya itikadi bali kwa upinzani waodhidi ya marafiki wa USA ambao wao wanawaita vibaraka
Saudia inaiangalia Iran kama tishio la Super power na kama itaaacha hali ilivyo Ufalme utatikiswa na Shia.
Ndio maana nchi nyingi zilianza mahusiano na Israel, si kwasababu wanaipenda bali kwa usalama wao.
Kwahiyo mgogoro wa middle east ni complicated si kama unavyosimuliwa.
Mahaba yanaruhusiwa lakini yasizidi Uwezo wa kufikiria sasa [emoji16]
Hakuna mahaba tupo hapa kueleza ukweli kwa watu wasioelewa.
Wapo wanaosemewa hadithi na kuzibeba tu hawajui hata ramani ya mgororo wa mashariki ya kati
Na imwisho tunaomba utusaidie kufahamu haya, katika bandiko lako umesema ''Houth na Hezbollah ni vikundi vya kigaidi''
1. Ugaidi ni nini
2. Nani anatoa na kuondoa hadhi ya ugaidi
3.Magaidi ni watu wanamna gani
Usipoweza kujibu 1-3 kaa kimya! soma ujifunze