Iran yaishambulia Israel kwa makombora
Unafikiri hatujui haya yote unayosema mkongwe?
Tunajua sana, ila mahaba yetu hayapo Tanzania, yapo kwa Israel, USA, Iran na Russia, uzalendo wetu upo huko. Kitakachotokea Tanzania wala hatujali, sisi tunajali kinachoendelea kwenye nchi ambazo uzalendo wetu upo, Tanzania tunaishi tu, lakini akili zetu hazipo Tanzania.
Jifunze kutuelewa, wala hautapata shida na sisi!
Dini ndio zimesababisha huu ujinga wote.
 
kule Ukraine atamwachia nan ? Russia aliamua kuwadivert West kwa kuwaletea mgogoro wa Israel na wao wameamua kumdivert kumletea hili la Iran , achague kufa na ukraine au syria au iran au afrika maana anasema alijipanga na vita
Tuendelee kufuatilia. Muda utajibu utatujibu!
 
Tena ashukuru yule mfalme wa Jordan kamsaidia kuangusha baadhi ya drone za Iran, huyo ni kibaraka siku zote yuko upande wa Israel.
sio kibaraka bali sio zombi wa udini huyo , aliwakaribisha wapalestina wakataka kumgeuka , kwann aendelee kushabikia mazombi
 
Pia ukubwa wa nchi na majirani. Israel inahitaji msaada kufika Iran
Kitakachotokea kwasasa ni Israel kutumia Marekani kama kawaida. Marekani ina base zake Jordan, Saudi Arabia na Iraq. Tatizo ni kwamba Iraq hawataki Marekani, wanatak waondoke lakini pia katika mpaka na Israel kuna Shia wanaoweza kushambulia.

Haiwezi isipokuwa kwa msaada wa Marekani, EU na UK kama ilivyotokea leo

Na Marekani itawasaidia kama ilivyosaidia Israel kumuua kamanda wa Iran Qassam Suleiman na Mtaalaam wa Nuklia. Kazi yote inafanywa na Marekani kwa kujificha nyuma ya kivuli cha Israel.

Mashambulizi ya Marekani kwa Houth kule Yemeni yanasemwa kufanyika kutoka Texas, huo ni uongo
Shambulizi lilifanywa kutoka Israel lakini Marekani ilijificha ili kutochochea vita ya Gaza


Amethibitisha yanafika mahali popote kuanzia Haifa, Tel Aviv hadi Jerusalem. Hii ni disadvantage ya Israel kwasababu ni nchi ndogo. Makombora ya Iran ya leo ni SEJJIL inayoweza kufika KM 2500 umbali kupita Israel na Shahed.

Lakini somo kubwa pia ni kwamba kama Israel inakabiliwa na changamoto ikipambana na Mataifa kama Iran.
Israel itawasikiliza Marekani na EU kuliko wakati mwingine kwasababu bila wao ingekuwa tabu
kwann Iran asipigane pekee yake bila Yemen , Iraq , Gaza , Lebanon na Syria ?
 
Bahati mbaya sana sisi wa Tanzania tunachukulia haya mambo ya kishabiki na zaidi kidini ni ujinga kupitiliza. Hizi nchi zote hawana habari na sisi wala hawataki kujuwa hali zetu, leo tukichinjana ndio watafungua Google kutaka kujuwa Tanzania ni kina nani.

Maafa yoyote ya kivita aina kama hii ya Irani, Israel na USA kama tunavyojuwa Israel ni USA maana hawezi kupigana yeye kama yeye, hii vita itatuletea maafa makubwa ya kiuchumi sana kwenye hali yenyewe ni mbaya kwenye inflation. Vita havijawahi kuwa kitu kizuri kabisa na gharama tutalipa huku maisha yatapanda.
Lini maisha yetu yaliwahi kuwa mepesi? Wenye nchi ndio watatikisika na hali ya dunia ila sisi makapuku tushazoea mihogo yetu na dagaa wala haina tabu.
 
Kwa hiyo speed ya kuchechemea zitatunguliwa mbali huko kabla ya kufika Israel
Inategemea, lakini kwa uelewa wangu mdogo tu, ukiruhusu anga lako litumike kutungua hizo drone ina maana unaruhusu Iran ikuongeze katika list ya target zake, yaani unawekwa katika list ya adui wa Iran.
 
Acha uongo we mlokole drone bado zipo njiani Netanyahu ameshatoroka Jerusalem. Wenyewe wamekadiria drone zitaanza kushusha mabomu kuanzia saa 8 au 9 usiku.
Mkuu mpaka sasa saa moja hii mbona mabomu hakuna? Au 8 za usiku na tisa ni kwa saa za Iran au Israel?
 
Kama distance btn them ni sio chini ya 2500km basi hii itakukuwa a mechanical war na sio a physical one. Hii ni mbaya sana. Makombola, drones na airforce kwa ujumla vyote vitachangia tuikaribisha vita ya3 ya dunia. Iran atapondwa, nchi za mashariki n kati na sehemu nyingine za kiislamu zitaungana n kuwa kitu kimoja. Hapa Israel, USA n washkaji zake watachapwa kama vita ya bubu n kipofu. Yote kheri, tungojee masjid al alqasa ibomolowe, Jews watengeneze hekalu lao kwa ajili ya nabii wao ndio kinuke kibadbad
We jamaa una mawazo mabaya sana dah 😀
 
..makombora yameweza kufika Israel.

..Na Israel ameweza kutungua makombora ya Iran.

..kila upande utarudi mezani na kujifanyia tathmini.
Mkuu kambi kubwa moja wapo ya anga Israel imeharibiwa na mashambulizi ya jana imeharibiwa hivyo kuna makombora yalipenya na kushambulia.
 
kule Ukraine atamwachia nan ? Russia aliamua kuwadivert West kwa kuwaletea mgogoro wa Israel na wao wameamua kumdivert kumletea hili la Iran , achague kufa na ukraine au syria au iran au afrika maana anasema alijipanga na vita
Sasa Israel na Iran nani anajiweza?😂 Maana Russia na Iran wakiungana ni sekunde chache tu Israel inabakia historia😂 maana atachakazwa fasta.

Na kuna mahasimu wanamtamani huyo Mmarekani kama unavyolitamani tako la Poshyqueen lile. Yani wanaling'atia ulimi na lips kinoma akiwemo kiduku.
 
Mkuu kambi kubwa moja wapo ya anga Israel imeharibiwa na mashambulizi ya jana imeharibiwa hivyo kuna makombora yalipenya na kushambulia.
Hili watalifunika funika sababu hawatotaka Israel aonekane kinyonge
 
Back
Top Bottom