Umeanza utabiri wako wa Baba Vanga (sijui kama umewahi kumsikia) ukiambiwa leta source:VoA unategemea nini kutoka source ya his Master's voice kama sio wanaongeza chumvi na kusema/zungumza adithi za kubuni/tunga ili kufurahisha baraza - tumekwisha wazoea hawatupi shida.
Hivi inaingia akilini kwamba Irani inaogopa mtu au Taifa lolote hapa Duniani - kwa kuwa wewe by default ni mbishi sana na unapenda sana kulazimisha mambo.
Hapa nataka nikukumbushe wewe na members wengine wa JF kuhusu umahili wa kiufundi (sayansi na teknolojia) linapo kuja suala la taifa la Kiajemi/Iran ili kudhilisha kwamba Iran haiogopi Taifa lolote - msiwe mnatuletea adithi za vijiweni - la kwanza: Je, unakumbuka mwaka 2011 jinsi Iran ilivyo ishusha kiufundi American Stealth Spy Drone type: RQ-170 Sentinel - US hawakuamini kilicho wapata, mwanzo walisema Wairan ni wazushi, mwishowe USA ilikubali baada ya Wairan kuonyesha picha live - je,Amerika ilichukuwa hatua gani mbona ilikaa kimya na kuiomba Iran iwarudishie Drone yao.
Hilo la kwanza, la pili linahusu Drone tena ya Kimerikani type: RQ-4A Global Hawk, mwaka 2019 Iranian integrated system of air defense ilitungua drone hiyo ya Kimerikani - mbona US ilikaa kimya bila ya kuichukulia Iran hatua yoyote - eti Iran inaogopa!!!
La tatu ambalo ni baya zaidi: miaka kama mitatu iliyo pita Iran ilivurumisha missiles 12 kwenda kushambulia kambi mbili za jeshi la Merikani nchini Iraq, missiles zote zilipiga designated target bila ya kuwa intercepted hata roketi moja licha ya Merikani kujidai kwamba kambi zao za kijeshi ni impregnable ie zinalindwa na ground breaking air defense system, lakini bado missiles za Iran zlifaikiwa kuharibu critical infrastructures pamoja na kujeruhi wanajeshi wengi walio kuwa wamejichimbia kwenye concret reinforced bunkers lakini walihumia na kukimbizwa kwenye Hospitali za Kuwait, Ujerumani na huko Merikani.
Dunia ilitegemea kwamba USA itaishushia Uran mabom kutoka B-52, B-2 nk lakini wapi wapo kimya mpaka sasa - halafu wanakuja waswahili hapa na kudai eti Iran inaogopa, Iran haiwezi kutishiwa Nyau na mifano hipo.
Sasa swali ni:je,missiles za Iran zilijipenyeza vipi kwenye kambi ambazo zinalindwa na teknolojia ya kufa mtu - hii inaleta picha gani kuhusu majigambo ya jamaa hawa,ambao wana kawaida ya kubeza beza teknolojia za Warusi - wakiongozwa na propaganda za MSM, wako very obsessed na everything Russian mpaka unashangaa!!
Tukija kwenye suala la Iran kukanusha kwamba ndio wanawauzia/patia jeshi la Urusi drone za Kamikaze - mbona kidiplomasia hilo ni jambo la kawaida lakini wenye akili wanajua muhusika mkuu ni yupi, hata kulipuliwa kwa bomba za gesi za Nord1 na Nord2 muhusika mkuu anajulikana lakini kwenye Public anakanusha - nyie mnaona ajabu gani Iran kukanusha mkadai eti Iran inaogopa - imuogope nani???