Iran yatishia kukata cable za internet zinazopita baharini

starlink bado zinatumia cable, starlink zinahitaji ground stations ambazo zinaungwa cable za fiber zinalazwa mpaka baharini zikaungane na "www"
 
Well said balaa lake litakuwa ni janga kubwa hakuna replacement ya hizo cable
 
Dunia inopoenda starlink internet itakuwa muhimu kama maji ya kunywa vile. Maana very soon malipo duniani yatategemena starlink internet.
Ndy mkuu ingawaje itachukua muda mrefu sana dunia kuamini mtandao unaomilikiwa na marekani kusimamia maswala ya miamala ya pesa ya dunia.
 
Starlink hata apewe miaka kadhaa hawezi akafidia, uwezo wa fibre optic kubeba data kwa sekunde, ukilinganisha na satellite za starlink zilizopo Kwa SASA angani, tofauti yake ni mbingu na ardhi
Ni kweli then Iran ataitishia dunia na Nini ili asipigwe?.
Kwasababu USA anahofia kuipiga Kwasababu ya uchumi wa dunia na uchumi wa marekani yenyewe lakini ukitoa hvy ni ngumu Iran kustahamili kichapo cha USA
 
Ni kweli then Iran ataitishia dunia na Nini ili asipigwe?.
Kwasababu USA anahofia kuipiga Kwasababu ya uchumi wa dunia na uchumi wa marekani yenyewe lakini ukitoa hvy ni ngumu Iran kustahamili kichapo cha USA
Hakuna cha maana wayamalize tuuh mezani, sasa hao waajemi wako level nyingine, ukimpiga haikawii majibu yake ni ya haraka mno, madhara yake tumeyaona hata sisi tulioko dunia ya tatu tunaona mambo yalivyomagumu
 

Wakate ili tuone itakuwaje. Kama mbwai na iwe mbwai. Maneno mengi badala ya kufanyia kazi vita iishe
 
Ni ngumu sana kuoatikana Kwa haraka yaani dunia itakuwa imeingia kwenye shida.
Kabsa Kwa sasa tunashuhudia maandamano nchi nyingi, changamoto ni hiyo strait of Hormuz, wakikata hizo cable hakuna mifumo itafanya KAZI, Sana haya mabank tunayategemea mno, changamoto za ghafla kama hizo tutaishije Kwa mfano
 
Hakuna cha maana wayamalize tuuh mezani, sasa hao waajemi wako level nyingine, ukimpiga haikawii majibu yake ni ya haraka mno, madhara yake tumeyaona hata sisi tulioko dunia ya tatu tunaona mambo yalivyomagumu
Hali ni mbaya
 
Wakuu salamu,
Kufuatia kauli ya Msemaji wa Jeshi la Mapinduzi la Iran (IRGC), Brigedia Jenerali Hossein Mohebi, kuwakumbusha "maadui" zake kuwa kuna nyaya kuu 7 za internet zinazopita chini ya Mlango-Bahari wa Hormuz, wadau wengi wameichukulia kauli hii kama tishio la kawaida la kijeshi.
Lakini ukisoma alichokifanya hapa Iran kwa jicho la Game Theory (Nadharia ya Michezo), huyu jamaa hajafanya mzaha kabisa. Ameweka mezani mkakati safi kabisa wa Tit-for-Tat (Jino kwa Jino) kwenye mchezo unaojulikana kama Iterated Prisoner's Dilemma (Mchezo wa Marudio wa Nani Atamfunga Paka Kengele).
 
Tuchambue kitaalamu hapa JF:
1. Mkakati wa Tit-for-Tat (Jino kwa Jino)
Kwenye Game Theory, mkakati wa Tit-for-Tat una sifa kuu nne: Ni Upole/wema (Nice), Unamaliza Kisasi (Retaliatory), Unasamehe (Forgiving), na Uko Wazi (Transparent).
Iran hajaanza kukata nyaya (bado yuko kwenye hatua ya 'Nice/wema). Lakini ameweka wazi (Transparent) kuwa: "Mkishambulia miundombinu yetu ya mafuta au nyuklia (Defection), hatua yetu inayofuata (Retaliation) ni kukata mawasiliano ya dunia." Huu ni ujumbe rahisi sana kwa adui kujua nini kitafuata akileta fyoko.
 
2. Asymmetric Payoff Matrix (Mizani Isiyolingana ya Hasara)
Hapa ndipo Iran alipopiga hesabu kali ya kihisabati. Ili tishio lako liwe la kuaminika (Credible Threat), lazima hasara ya utekelezaji iwe kubwa kwa adui kuliko kwako.
• Maadui (US & Washirika wa Ghuba): Uchumi wao unategemea sekta ya kidijitali, masoko ya hisa, na mifumo ya kibenki kwa takriban 90%. Nyaya hizo zikikatika, sekta ya fedha duniani inasimama na hasara inakuwa ya mabilioni ya dola kwa sekta zote.
• Iran: Kutokana na vikwazo vya miaka nenda rudi, Iran tayari ametengwa na mifumo ya kifedha ya Magharibi (kama SWIFT). Uchumi wake hauna cha kupoteza sana internet ya dunia ikizima kwa wiki mbili.
Kwa lugha rahisi: Mwenye nguo mwilini anamwogopa mtembea uchi. Iran anajua akipoteza miundombinu yake, adui atapoteza zaidi
 
3. Kulazimisha "Nash Equilibrium
Lengo la Iran siyo kuanzisha vita, bali ni kulazimisha mchezo ubaki kwenye Nash Equilibrium—hali ambayo hakuna upande unaoona kuna faida ya kubadili msimamo wake wa sasa wa amani. Marekani na washirika wake wakipiga hesabu ya hasara ya kiuchumi ya kupoteza hizo cable 7 za internet, wanajikuta wanalazimika kutoshambulia. Mchezo unakuwa wa Negative-Sum Game (kila mtu anapoteza), kwa hiyo amani ya mashaka inaendelea kulindwa.
Mytake: Iran ameweka karata yake ya kijografia vizuri sana juu ya meza. Je, unadhani Pentagon (Marekani) wataingia kwenye huu mtego au watafuta njia mbadala ya kucheza mchezo huu?
 
Watu wanaongelea data centre na AI kuzifunga we unaongelea starlink? Starlink ni internet yetu hii ya kufanyia mambo madogo ila huwezi kuitumia kurun data centre.
 
Trump hawezi kujali,watakaopoteza mawasiliano ni nchi za kiarabu na asia,kinachomfanya Trump asishambulie kwasasa ni hofu ya kupoteza uchaguzi wa midterm
 
watakaopoteza mawasiliano ni nchi za kiarabu na asia
cable ziko interconnected, kwengine hakutakata mazima ila net itakuwa slow, na kama una browse web ambayo server iko Europe, cable iko likely kupitia arabian sea hapo , web haitopatikana kabisa au ukawa rerouted na cable nyingine na access ya web kuwa slow
baadhi ya servers za Google zinazotumikia Africa ziko uarabuni, nazo hazitopatikana
kumbuka kuna data centers na network hubs kibao za kimarekani huko UAE , Bahrain, Qatar zote zinakuwa offline
 
Watu wanaongelea data centre na AI kuzifunga we unaongelea starlink? Starlink ni internet yetu hii ya kufanyia mambo madogo ila huwezi kuitumia kurun data centre.
Starlink inaenda take over internet dunia nzima na itakuwa ni households needs kama ilivyo maji ya kunywa. Elon Musk anadevelop tech ecosystem ambapo dunia nzima watatumia. Kwa mfano kuna X money ambapo miaka michache ijayo itatumika dunia nzima, na wanadamu na itakuwa linked na Neuralink ya huyohuyo Elon Musk. mpaka hapo tech tatu za Elon Musk zishatumika. Elon now anazungumzia Super AI sio AI tena. Hivyo Starlink sio internet ya kufanyia mambo madogo, tunazungumzia internet yenye product inayotumika jeshini (Zelensky analialia huko kubaniwa speed) hivyo hiyo sio internet ya kufanyia mambo madogo. Elon now anaanda kitu inaitwa large-scale orbital data center kwa kutumia hiyo hiyo starlink.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…