Iran yatoa Onyo kwa nchi yoyote ya Kiarabu itakayoruhusu Israel na Marekani kutumia anga au ardhi yake kushambulia Iran itaadhibiwa vikali

Iran yatoa Onyo kwa nchi yoyote ya Kiarabu itakayoruhusu Israel na Marekani kutumia anga au ardhi yake kushambulia Iran itaadhibiwa vikali

Ki namna gani
Islam's dominant sect, which roughly 85 percent of the world's 1.6 billion Muslims follow, view Shia Islam with suspicion, and extremist Sunnis have portrayed Shias as infidels, heretics and apostates.
 
Soon tutasikia free Iran.

Mwanzo watu walidai Hezbula ni kiboko ya Isarel mwaka 2006 alikimbia, wakadai anawaonea Gaza. Sasa Hezbu wanaomba poo (pause) bila masharti ya kuihusisha Gaza huku mtarajiwa wa mrithi na mtarajiwa wa mrithi wa mrithi wakiungana na mrithiwa.

Yeye Iran anasema akipiga mkwara kwa nguvu zake hajui kimo cha nguvu za wengine.

Kikubwa ameyavulia nguo. Kitajulikana na uwanja wa vita utaamua, na hii inaweza ikawa jumlajumla maana mlengwa hapo ni Ayatollah.

Nakumbuka Iraq alitoa mkwara kama huo, mwisho wa siku ndio hivo tena.

Bila Urusi kuwa bize, ingekuwa ngumu kumpiga Iran, kama ilivyokuwa Syria. Sasa Urusi yupo bize na yake, yafaa sasa kulianzisha na huyu Iran.
Soon gani hiyo ambayo unatandikwa Kila siku lakini una kazi ya kusema soon tumechoka kusubiria
 
Kwa taarifa yako uelewe kwamba Israel ni muhimu kwa Saudi Arabia kuliko Iran na Saudi Arabia anaelewa kwamba Wairan ni makafiri tu.
😂😂😂😂 Leo mnawakumbatia waislamu wa Saudi Arabia ili tu kuepuka adhabu ya muirani . Na Bado mtasema yote
 
Huyo anakuja na ile mikwara kama ya Russia kwamba ole wake atakaye isaidia Ukraine atakiona kilicho mnyoa kanga manyoya lkn hadi leo hatujaona kitu...!!
 
Kiongozi, mimi najua kinachoendelea ME kuliko wewe.

Mimi ni sunni na nina ndugu Yemen ambao ni sunni.

Najua kilichotokea Yemen kwa undani kuliko wewe.

Najua kinachoendelea Syria kuliko wewe. Sheikh Muhammad Al Hudaa Al Yaaqoubi msimamo wa kwanza alidhani kama wewe ambaye ni Sunni. Baadaye alibadilisha msimamo wake.

Sheikh Said Ramadhan Al Bouti ni mwanawazuoni mkubwa sana wa kisunni. Kauliwa na hao hao Isis ambao Saudi Arabia alikuwa aki fund operation zao kisa Sheikh Al Bouti aligundua hila zao na kuwa pamoja na Bashar Al Assad.

Tena aliuliwa ndani ya msikiti na bomu la kutegwa. Alikufa yeye pamoja na mjuu wake na watu wengine 42 na 84 wakiwa maeruhi.

Katika haya uliyoandika huwezi kuniongopea hata nukta.

Saudi Arabia walishaiuza Palestina kitambo na miaka ya nyuma kama siyo 2003 au 2005 mwakilishi wa Saudi Arabia alizomewa na wapelestina na wengine kumtaka aondoke. Mohammad Bin Suleyman alivyokuwa crown prince aliwataka wa Palestina wakubaliana na matakwa ya Israel kabla hata hii vita yao ya oktoba kuanza.

Sijisikii kuandika sana naishia hapa!
ungeendelea kaka,Hawa wengine wamejaa ushabiki na kutulisha matango pori
 
1002306644.jpg
 
Kwa bahati mbaya sana viongozi wa nchi nyingi za Waarabu ni wale tunaowaita wanafiki na wamewekwa kwenye mamlaka yao na USA ikisapotiwa na Israel. Yani hapo Jordan, Saudi, Misri, UAE etc zote viongozi wao ni vibaraka wa USA na Israel na ndio maana huoni hata wakikemea dhuluma ya Israel dhidi ya Palestina.

Hawa viongozi wao wanachojali ni maslahi yao tu hawajali chochote wala hawapo hapo kuwatetea wanaoonewa, infact wenyewe wanawaonea wananchi wao na katika hizo nchi hakuna demokrasia na hakuna uchaguzi. Lakini kamwe huwezi kusikia USA au UN wanasema hao viongozi kuwa ni madikteta. Kwa dunia ya leo Dikteta ni kiongozi ambaye hataki kufata masharti ya USA mfano Saddam na Gadafi au Mugabe lakini wanaotii kamwe sio madikteta.

Hawa viongozi waliowekwa na USA na Israel wanahakikisha wanalinda maslahi ya waliowaweka vinginevyo wanapinduliwa, na wote wanalindwa na USA na Israel. Na hawataweza kwenda kinyume na makubaliano yao na mabwana zao otherwise watakuwa eliminated. Hawa wameuza ubinadamu wao kwa mali na vyeo

Kwa hivyo ni ngumu sana hawa viongozi kubadilika labda kama yatatokea mageuzi kwenye nchi zao waondolewe madarakani. Na sisi tunaombea hilo na ninaamini ipo siku wataondoka na kupatikana viongozi wema na hapo ndio utakuwa mwisho wa Israhell.
Mugabe huyu huyu au mwingine! Kichaa aliyeng'ang'ania Madaraka mpaka anajikolea mwenyewe! Huu utani Sasa.
 
IRAN ajawatisha waarabu ila kawakumbusha tu kuwa kufanya kosa la aina hiii azabu yake ni aina hii chaguo wanalo wanyewe waarabu muimu wasije sema awakuonywa ujumbe umefika sote tumeshuhudia vibalaka matumbo joto. IRAN anawazoom tu.
 
Iran sio nyepesi kama unavyodhani.
Kama ingekua nyepesi ingeshavunjwa utawala wake miaka ile ya 1980s ikiwa bado nchi dhaifu.
Ila sasa ishakita mizizi no way unaweza iangusha Iran.
Hao USA wenyewe wanajua sio rahisi ndio maana kila siku wanaishia kutishia tu.
Unaizungumzia nchi iliyopigana vita miaka nane consecutively.
Bwana Yesu apewe sifa
 
Iran imetoa ONYO kuwa nchi yeyote ya kiarabu itakayosaidia Israel na marekani kuishambulia basi itakumbana na matatizo makubwa.

Iran imechukua msimamo mkali dhidi ya majirani zake baada ya kutoa onyo kali kuhusu ushirikiano wowote na Israel kwa ajili ya operesheni za kijeshi.

Msimamo huu mkali ni sehemu ya mkakati wa Iran kuzuia nchi za kiarabu kushirikiana Israel. Maafisa wa Iran wamesisitiza umuhimu wa "umoja wa kikanda" kukabiliana na kile wanachokiona kama tishio kutoka Israel, huku wakieleza pia umuhimu wa kudumisha utulivu huko Mashariki ya Kati

Soma pia: Israel kuishambulia Iran leo usiku, Marekani yaja juu

Onyo hilo halihusishi tu matumizi ya anga, lakini pia Iran inafuatilia kwa karibu uwezekano wa ushirikiano wa vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko katika eneo la Gulf

Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia, msimamo wa Iran uliwekwa wazi wakati wa mkutano wa hivi karibuni huko Doha.

Ujumbe ulikuwa wazi: taifa lolote la Gulf States litakaloruhusu anga yake au vituo vyake vya kijeshi kutumika kwa operesheni dhidi ya Iran litakabiliwa na kisasi.

Tehran inachukulia vitendo hivyo kama uamuzi wa pamoja wa mataifa yote ya Gulf, jambo ambalo linaweza kupanua wigo wa majibu yake.

Kazi kwako Saudi Arabia na vibaraka wengine wa marekani hapo Middle East .

Hata Russia alitoa onyo kama hili, lakini halikutiliwa maanani na wanaume, bado wanatoa misaada ya kijeshi huko Ukraine
 
Kama waisrael wenyewe ndio awa kilio tupu uyu mwarabu akijichanganya msiba unahamia kwao muiran onyo kashatoa baada y apo anabutua.
 
Iran imetoa ONYO kuwa nchi yeyote ya kiarabu itakayosaidia Israel na marekani kuishambulia basi itakumbana na matatizo makubwa.

Iran imechukua msimamo mkali dhidi ya majirani zake baada ya kutoa onyo kali kuhusu ushirikiano wowote na Israel kwa ajili ya operesheni za kijeshi.

Msimamo huu mkali ni sehemu ya mkakati wa Iran kuzuia nchi za kiarabu kushirikiana Israel. Maafisa wa Iran wamesisitiza umuhimu wa "umoja wa kikanda" kukabiliana na kile wanachokiona kama tishio kutoka Israel, huku wakieleza pia umuhimu wa kudumisha utulivu huko Mashariki ya Kati

Soma pia: Israel kuishambulia Iran leo usiku, Marekani yaja juu

Onyo hilo halihusishi tu matumizi ya anga, lakini pia Iran inafuatilia kwa karibu uwezekano wa ushirikiano wa vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko katika eneo la Gulf

Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia, msimamo wa Iran uliwekwa wazi wakati wa mkutano wa hivi karibuni huko Doha.

Ujumbe ulikuwa wazi: taifa lolote la Gulf States litakaloruhusu anga yake au vituo vyake vya kijeshi kutumika kwa operesheni dhidi ya Iran litakabiliwa na kisasi.

Tehran inachukulia vitendo hivyo kama uamuzi wa pamoja wa mataifa yote ya Gulf, jambo ambalo linaweza kupanua wigo wa majibu yake.

Kazi kwako Saudi Arabia na vibaraka wengine wa marekani hapo Middle East .

Hii sasa ni rasmi, Iran hawalali kwa uoga na hofu ya kushambuliwa.

Waambieni, hao persians, Waebrania hawana nia ya kuwashambulia, waache kujinyeanyea.
 
Kwa watakaoelewa tu.
Vita ya Israel na maadui zake haitaisha leo wala kesho. Bali kutakuwa na utulivu wa vipindi vifupi tu.
Na wengi hawajui kuwa mipaka iliyowekwa kimataifa Israeli hawaitambui.
Kwa wanaosoma Biblia kuna mipaka ya taifa la Israel imo mule na hiyo ndiyo wanayoitafuta.
Bado litafuata la hekaru lililojengwa na Suleiman.
Litajengwa palepale lilipobomolewa, haijalishi kimejengwa kitu kingine. Ni lazima kilichojengwa juu kibomolewe lijengwe Hekalu.
 
Hasara to which levels? Iran wali declare kuwa wanahusika na hizo attack?

A perfect attack ni kumuumiza adui asiweze kuendelea na operation zake. But then saudi ndio wana uchumi mkubwa kuliko iran, probably wana jeshi bora sasa kuliko nyuma

Tunarudi pale pale iran hamna kitu atafanya ni biti tu for nothing
Mkuu embu ongea kama mtu mzima basi.
Billions of dollars hiyo siyo hasara!?
Hata ingekua hasara ya mia moja ni hasara.
Houthi ni kundi linalopewa msaada wa silaha, jeshi na fedha na Iran.
Kuna IRGC soldiers ndani ya Houthi kama ulikua hujui.
Saudi Arabia kuwa na uchumi mkubwa hiyo inatambulika toka zamani,ila usisahau Iran ni nchi yenye economic sanctions 40+ years lakini ni middle upper income country.
Nenda kafanye tafiti ujengaji wa petroleum plant ni mamilioni mangapi kesha urudi hapa.
 
na hapo ndio utakuwa mwisho wa Israhell
Mzee hakuna nchi yoyote ya kufikisha mwisho wa Israel hapa duniani hata malaika mwenyewe hawezi, mpaka kwa idhini ya Mungu mwenyewe na haitatokea mpaka mwisho wa mbingu na nchi.

Huyo muajemi (Iran)Mungu mtu wenu mnayemsifia na kumuimbia haleluya,atachakazwa kama farao wa misri na Musa,mashabiki wote wa Iran wataona nyotanyota vichwani mwao na hawataamini kitakachotokea.
 
Mkuu embu ongea kama mtu mzima basi.
Billions of dollars hiyo siyo hasara!?
Hata ingekua hasara ya mia moja ni hasara.
Houthi ni kundi linalopewa msaada wa silaha, jeshi na fedha na Iran.
Kuna IRGC soldiers ndani ya Houthi kama ulikua hujui.
Saudi Arabia kuwa na uchumi mkubwa hiyo inatambulika toka zamani,ila usisahau Iran ni nchi yenye economic sanctions 40+ years lakini ni middle upper income country.
Nenda kafanye tafiti ujengaji wa petroleum plant ni mamilioni mangapi kesha urudi hapa.
Kaka huna point bado. If attack ya iran ingekuwa ina damage kihadi hiko leo saudi angekeua haganayi kitu bila iran kuruhusu, or wasingekuwa ecomic power house, billions of dollar is nothing kama saudi ame revover in short period of time

Once again attack ya iran ilikuwa na damage ndogo sana. Na kwa sasa hawatoweza kabisa
 
Back
Top Bottom