Iran yatoa Onyo kwa nchi yoyote ya Kiarabu itakayoruhusu Israel na Marekani kutumia anga au ardhi yake kushambulia Iran itaadhibiwa vikali

Iran yatoa Onyo kwa nchi yoyote ya Kiarabu itakayoruhusu Israel na Marekani kutumia anga au ardhi yake kushambulia Iran itaadhibiwa vikali

Nani alipeleka majeshi Yemen juzi tu hapo akisaidiwa na USA Ili kupambana na Houth?. Mbona kwa sasa Yemen hakuna fujo?.
Nani kasema Yemen hakuna Fujo? Yemen imekuwa failed State no one care for it Ndio maana haiongelewi, kwa sasa Yemen imegawanyika vipande viwili
 
Iran.

Iran anazibadilisha kuwa Vassals
Na Marekan kwa nn aliivamia 2002/2003 alikua anataka nini?. Je baada ya hio 2003 imetulia ?. Hata hio 1980 Marekan alikua anasapot nchi gani na kwa nini aliigeuka 2002?.

Kua na kiasi na uzungumze logic basi maana Kila mtu anaelewa nini kinaendelea na nini kilitokea.
 
Makombora missiles yatafika tu Tehran bila kupewa ruksa ya kutumia anga air space. Hawa Iran ndiyo hawa waliopigana na Saddam wa Iraq miaka 10 kuifikia Baghdad hadi wakakubali yaishe.
 
Nani kasema Yemen hakuna Fujo? Yemen imekuwa failed State no one care for it Ndio maana haiongelewi, kwa sasa Yemen imegawanyika vipande viwili
Yemen ni Moja ndio maana hata juzi Marekan kasema Houth wasishambulie meli Ili aitambue kama Serikal halali. WEST na USA wakishindwa kutambua Serikali sio kwamba nchi imegawanyika. Hata Venezuela tumeona na tuliona.
 
Iran imetoa ONYO kuwa nchi yeyote ya kiarabu itakayosaidia Israel na marekani kuishambulia basi itakumbana na matatizo makubwa.

Iran imechukua msimamo mkali dhidi ya majirani zake baada ya kutoa onyo kali kuhusu ushirikiano wowote na Israel kwa ajili ya operesheni za kijeshi.

Msimamo huu mkali ni sehemu ya mkakati wa Iran kuzuia nchi za kiarabu kushirikiana Israel. Maafisa wa Iran wamesisitiza umuhimu wa "umoja wa kikanda" kukabiliana na kile wanachokiona kama tishio kutoka Israel, huku wakieleza pia umuhimu wa kudumisha utulivu huko Mashariki ya Kati

Soma pia: Israel kuishambulia Iran leo usiku, Marekani yaja juu

Onyo hilo halihusishi tu matumizi ya anga, lakini pia Iran inafuatilia kwa karibu uwezekano wa ushirikiano wa vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko katika eneo la Gulf

Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia, msimamo wa Iran uliwekwa wazi wakati wa mkutano wa hivi karibuni huko Doha.

Ujumbe ulikuwa wazi: taifa lolote la Gulf States litakaloruhusu anga yake au vituo vyake vya kijeshi kutumika kwa operesheni dhidi ya Iran litakabiliwa na kisasi.

Tehran inachukulia vitendo hivyo kama uamuzi wa pamoja wa mataifa yote ya Gulf, jambo ambalo linaweza kupanua wigo wa majibu yake.

Kazi kwako Saudi Arabia na vibaraka wengine wa marekani hapo Middle East .

Huo mkwara aliutoa Russia(baba ake Irani), mara oo atakaye mpa siraha Ukraine naye atajumuishwa kwenye mgogoro, miamba ilimpa siraha na ilikuwa ikitaja na aina iliyompa. Alifanya nn
 
Unajua Saudi Arabia kuna propaganda inazieneza kwa kutumia madhheb ya Salafi kuhusu Iran na kinachoendelea ME.

Baada ya Iraq kuparaganyika Saudi Arabia anataka ukiranja mkuu wa waarabu wote hapo ME.

Tatizo la Saudi Arabia hana nguvu ya kijeshi, basi angalau ingelikuwa kwenye diplomasia kama Qatar inavyopambana kuweka mambo sawa Saudi Arabia yeye hashighuliki kabisa. Angalau angelikuwa anaongea ingeliwajaza nguvu wenzake.

Hii hatua kaichukua Iran kwa Saudi Arabia kwake hii ni bahati mbaya na anaona jinsi waarabu wengineo wanashawishika na ushawishi wa Iran kitu ambacho kwake ni hatari anaona anapoteza ukaka mkuu kwa waarabu wenzake.

Vurugu zote zinazotokea ni hapo ME Saudi Arabia na Uran ni kugombea ukiranja mkuu hapo ME.
Migogoro ilianza wakati mtume anaumwa na alivyofariki ndo zikwa brutal battle na hazitakaa ziishe
 
Walishakaririshwa hawa watu, daima wako upande wa wasio waislamu, isipokua baadhi wenye kujitambua, hata Qur'an imeshawazungumzia hawa watu, hawatakua radhi nasi mayahudi na Manaswara mpaka tufuate mila zao
Kama mlishindwa kuzuia kuanzishwa kwa taifa la israel mwaka 1946 ndo mfute mila zao
 
Yemen ni Moja ndio maana hata juzi Marekan kasema Houth wasishambulie meli Ili aitambue kama Serikal halali. WEST na USA wakishindwa kutambua Serikali sio kwamba nchi imegawanyika. Hata Venezuela tumeona na tuliona.
Yemen sio Moja

1000039115.png

Hii ni Taarifa ya Al-Jazeeraa kuhusu Houthi na Yemen.

Yemen inaserikali inayotambulika Dunia nzima na kuna Kundi la waasi wa Kabila la Kishia kinaitwa Houthi ambao wanapokea Silaha nyingi sana kutoka Iran

Asichotaka Iran ni makombora kurushwa kutokea ndani ya nchi nyingine tofauti na Israel. Kwa mfano base za USA zilizopo Saudia zimshambulie Iran kutokea Saudia hapo Iran atashambulia Moja kwa moja makombora yalikotokea. Nadhani umeelewa.
Kwenye vita huwezi mpangia adui yako jinsi ya kupigana anachofanya iran ni kichekesho
Hata kama saud arabia anamsaidia iran kwa akili yako unadhani atamwambia iran kwamba nimemsaidia israel
Kauli nyingine ni za kiogo yeye ajiandae

Hezbollah walirusha makombora zaidi ya mwezi israel ya kaskazini amekuja kujibu kaanza na vifaa vya mawasialiano, kaja solar panel mara redio maeneo ambayo hutegemei kabisa alafu mwishoni kau uongozi wote wa hezbollah

Aache kelele na mikwara ya kichaa cha mbwa
 
Na Marekan kwa nn aliivamia 2002/2003 alikua anataka nini?. Je baada ya hio 2003 imetulia ?. Hata hio 1980 Marekan alikua anasapot nchi gani na kwa nini aliigeuka 2002?.

Kua na kiasi na uzungumze logic basi maana Kila mtu anaelewa nini kinaendelea na nini kilitokea.
Inabidi nitulie nije niandikie Why baada ya Ottoman kuanguka na vita za middle east zilizopo sasa zikaanza rasmi... I see wapi Watu wengi hamuangalii sababu ya Nchi za Mashariki zinapigana kila siku...

Hata Iran isipopigwa na Marekani itapigana yenyewe kwa yenyewe ni suala la muda
 
Yemen ni Moja ndio maana hata juzi Marekan kasema Houth wasishambulie meli Ili aitambue kama Serikal halali. WEST na USA wakishindwa kutambua Serikali sio kwamba nchi imegawanyika. Hata Venezuela tumeona na tuliona.
Yemen sio moja acha ubishi wa kitoto
 
Back
Top Bottom