Iringa: Kanisa Katoliki lawazuia waumini walioshiriki kongamano la Mwamposa kutopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu mpaka watakapoungama

Iringa: Kanisa Katoliki lawazuia waumini walioshiriki kongamano la Mwamposa kutopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu mpaka watakapoungama

Kuna dogo alinyang'anywa Bajaji na bosi wake. Amekaa wiki mbili hana KAZI. Siku Mwamposa ametua Iringa dogo akaenda kuombewa. Ametoka tu kuombewa akapigiwa simu na bosi njoo uchukue Bajaji. Dogo alinisimulia huku anatoa machozi ya furaha. MTU kama HUYO ukimwambia Mwamposa tapeli atakuelewa?
Mtu kama huyo ukimwambia mwaposa mmbaya hawezi kukuelewa kwanza anaweza kukutukana kabisa
 
Mkuu kwani watu wanaapa kwa mungu ama kwa kanisa? Haya makanisa ni taasisi za kitapeli. Hapo kinachowauma ni kukosa sadaka na mwamposa kula sadaka.

Kanisa Katoliki lina sakramenti zake, na katika hizo, ubatizo na kipaimara huwa kuna zoezi la kukiri imani. Iwapo muumini atakuja kukiuka imani aliyoikiri, kwa maneno au vitendo, basi atafungiwa sakramenti (hata kama ataendelea kuhudhuria ibada).

Mfano mzuri ni katika uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2010, mgombea mmoja wa ubunge wa CCM alitumia title ya Utatu Mtakatifu na kujiita yeye ni Mwana wa Mungu (Yesu), na aliposhinda uchaguzi, baadhi ya wafuasi wake waliendesha ibada ya mazishi makaburini kwa taratibu kama zile zile za Kanisa (kaburi, sala, jeneza, msalaba nk), kwa kufanya maigizo ya kumzika mgombea aliyeshindwa. Tukio hilo likatafsiriwa kama kufuru ya imani, na zaidi ya waumini 400 walifungiwa sakramenti zao, hadi walipokuja kurudia kukiri upya imani ya Kanisa.

Kwa hiyo ukifanya ibada inayokufuru au inayopingana na imani ya kanisa, huo ni utaratibu wa kawaida kabisa kufungiwa sakramenti
 

KANISA Katoliki katika Jimbo la Sumbawanga, mkoani Rukwa, limevunja ukimya na kunena kuhusu mambo yaliyosababisha waumini wake, kutengwa​

Sunday, December 19, 2010

Mussa Mwangoka,
Sumbawanga

KANISA Katoliki katika Jimbo la Sumbawanga, mkoani Rukwa, limevunja ukimya na kunena kuhusu mambo yaliyosababisha waumini wake, kutengwa na wengine kuwekewa pingamizi kwa kukufuru utatu mtakatifu wakati wa uchaguzi mkuu, uliomalizika Oktoba 31 mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya baadhi ya vyombo vya habari, kuandika na kuchapisha habari kuhusu sakata hilo huku kanisa likiwa halizungumzi lolote.

Kitendo hicho, kiliwafanya baadhiya wananchi waliowahi kusoma habari hizo kutaka kujua ukweli kuhusu madai kuwa kanisa, limewatenga baadhi ya waumini wake kwa kukufuru utatu mtakatifu wakati wa uchaguzi mkuu.

Jana, Wakili wa Kiaskofu katika Jimbo la Sumbawanga, Padri Modest Katonto, alikiri kuhusu adhabu hiyo kwa baadhi ya waumini wa kanisa hilo na kwamba hakuna anayeweza kuitengua.

"Kanisa lingependa ifahamike kuwa hakuna mamlaka yoyote ya kidunia, inayoweza kuwaoondolea waumini hao adhabu hiyo, isipokuwa kwa jitihada za mtu mwenyewe binafsi kujipatanisha na kanisa kwa wale waliotengwa," alisema Padri Katonto.
Kanisa hilo pia limesema halina itikadi za kisiasa na kwamba adhabu zimetolewa kwa waumini hao, hazijali wadhifa wa mtu yeyote katika jamii.

Alisema kilichozingatiwa ni makosa ya kwenda kinyume cha imani na kushabikia mafundisho potofu.

Wakili huyo wa kiaskofu, alisema waumini waliokumbwa na adhabu hizo wako katika makundi mawili na kwamba la kwanza, ni la waliotengwa kwa kosa la kujilinganisha na utatu mtakatifu na kushabikia mafundisho potofu, huku wakijua wazi kuwa kitendo hicho ni cha uovu.

Kwa mujibu wa Padri Katonto, kundi hilo lina jumla ya waumini 27.
Alisema kwa mujibu wa sheria ya kanisa namba 1364, kosa lililofanywa na watu hao, linawatenga na umoja wa kanisa hata bila kutangaziwa au kujulishwa na kiongozi wa kanisa.

Alisema chini ya adhabu waliyopewa, waumini hao wamepoteza haki ya kushiriki katika idaba zote za hadhara za kanisa katoliki, kutoshiriki katika maadhimisho ya sakramenti, kutopokea akramenti na kutoshirki katika shughuli za uongozi wa kanisa .
Alisema "ikiwa aliyetengwa atahudhuria au atakuwepo katika mazingira ya inapofanyika ibada, lazima aondoke au au kama hatatoka, ibada itasitishwa. Na ikiwa atakufa bila kutubu, hatapewa maziko ya kanisa," alisema Padri Katonto.
Padri Kantonto alisema kundi la pili ni la waumini waliowekewa pingamizi ambao hata hivyo, hakutaja idadi yao.

Alisema chini ya pingamizi walilowekewa, waumini hao wananyimwa haki ya kupata huduma za kanisa kwa muda, wakati makosa yao yakichunguzwa na kwamba kama itabainika kuwa hawakufanya, watarudishiwa huduma zote.

Alisema hata hivyo, pingamizi hilo haliwaondowi watu wa kundi katika umoja na kanisa, kama ilivyo kwa waliotengwa.

Alisema katika kipindi cha uchaguzi mkuu, kanisa lilijitahidi kuwakumbusha waumini wake kuhusu nafasi zao na wajibu wao, lakini kinyume chake kanisa limeshuhudia, na kusikia baadhi ya waumini wakionyesha utovu wa nidhamu kwa kukufuru utatu mtakatifu.

"Walikufuru utatu mtakatifu, baadhi ya wagombea wakajifafanisha na Mungu mwenye nafsi tatu, kukufuru msalaba mtakatifu wa kanisa kwa kuuzika, kukejeli, kutukana na kudharau viongozi wa kanisa na wakristo wenzao," alisisitiza Padri Katonto.

Alisema vitendo hivyo vimesikitisha mno mama kanisa kwa sababu vimeambatana na usaliti wa imani na maadili ya kikristo.

"Lakini pia vitendo hivyo ni makwazo kwa wana kanisa na wakristo wa madhehebu mengine na watu wote wenye mapenzi mema," alisema.
Alisema wanaotenda makosa kama hayo kwa mujibu wa sheria, kanisa, lina haki ya msingi ya kuwaadhibu na kwamba adhabu hizo si ngeni ndani ya kanisa.
Kasisi huyo alifafanua kuwa shutuma dhidi ya kanisa kuwa limewatenga na kuweka pingamizi waumini wake kwa sababu za itikadi za kisiasa ikiwa ni pamoja na kuipigia kura CCM ni uwongo na uzushi wenye lengo la uchochezi.

"Kanisa Katoliki linahoji hivi uchochezi huo unafanywa kwa maslahi na manufaa ya nani," alisema.
Alisisitiza kuwa kamwe kanisa halitokaa kimya bila kukemea uovu kwa hofu ya vitisho na uzushi unaolenga katika kutetea maslahi ya kundi la watu wachache wasio na dhamira safi
 
Mkuu kwani watu wanaapa kwa mungu ama kwa kanisa?

Haya makanisa ni taasisi za kitapeli.

Hapo kinachowauma ni kukosa sadaka na mwamposa kula sadaka.

Watu wazima kabisa wanaojiita mapadri wanakaa wanatoa waraka wa kisenge hivi utafikiri wanafikiria kwa kutumia makalio.

Hivi dini zimejaa watu wasenge kweli.
Nakazia..

#MaendeleoHayanaChama
 
Wana Uhuru wa kuabudu wapi na saa ngapi bila kuvunja katiba. Katoliki wajitafakari kwann waumini wao wanahama?

Katoliki sasa lipo busy na michango kuliko neno.
Muda mwingi katika ibada zao sehemu kubwa n michango.

Ukweli usemwe
 
Wana Uhuru wa kuabudu wapi na saa ngapi bila kuvunja katiba. Katoliki wajitafakari kwann waumini wao wanahama?

Katoliki sasa lipo busy na michango kuliko neno.
Muda mwingi katika ibada zao sehemu kubwa n michango.

Ukweli usemwe
Tukutane kesho pake Tabata kwenye ufunguzi wa Moyo Mtakatifu wa Yesu.
 
Wana Uhuru wa kuabudu wapi na saa ngapi bila kuvunja katiba. Katoliki wajitafakari kwann waumini wao wanahama?

Katoliki sasa lipo busy na michango kuliko neno.
Muda mwingi katika ibada zao sehemu kubwa n michango.

Ukweli usemwe
Ndio wana Uhuru wa kuabudu ndio maana wamepewa uhuru wa kubaki kwa Mwamposa au kurudi ktk Kanisa Katoliki na kutubu kisha kukiri Imani tena.
 
Huu nao ni utumbo, wanamtisha nani, kila mtu ana haki ya kuabudu anachokiamnini, au wanahisi wanasimamia watoto wa chekechea?

Mtu ana uhuru wa kuwa anapotaka na siyo kushikwa masikio kama mbuzi anapelekwa machinjioni

Kama wakienda huko wanapokea uponyaji, watakuwa wanakosea sana,

Kuna story moja ndani ya biblia ipo very interesting, inafanana sana na wanachofanya hao mapadre wakatoliki,

Yohana 9: 16...., nakazia mstari wa 22 na 25

Waache wafuate imani wanayoona inawasaidia maishani mwao!!
Huo uhuru ndio wanaousema hapo. Kama unaona huko ni bora baki huko! Ila ukiwa huku masharti ni haya.
 
Ukiufuata na Kuuishi Ukatoliki ni sawa na chupa ya maji safi iliyo jaa hakuna nafasi tena ya kuweka uchafu[emoji123][emoji106]
Hao ndio wale watafuta miujiza mpaka wanakuwa washirikina. Angejua katoliki ndio mababa wa miujiza angejikuta mpumbavu. Eti hawana upako, kwahiyo lilivo jinga linatafuta mazingaumbwe.
 
Wana Uhuru wa kuabudu wapi na saa ngapi bila kuvunja katiba.
Wana uhuru wa kuabudu huko walikoenda. Hivi wangewafungia ndani si ndio tungetakiwa kusema wamewanyima uhuru wa kuabudu? Sasa wameambiwa nendeni tu, bado mnalalamika
 
Katoliki sasa lipo busy na michango kuliko neno. Muda mwingi katika ibada zao sehemu kubwa n michango.
Nadhani unaongea kinyume. Labda umejisahau, ulitaka kusema Mitume na Manabii wako busy na michango kuliko neno
 
Ni sahihi kabisa huwezi kushinda ccm ukalala Chadema. Kila mtu ale alikopeleka mboga.
 
Wao ni sawa kwa muumini kushinda kidimbwi Kula gambe hawana shida na huyo atapokea tu sakramenti , Ila mtu anaeenda kutafuta uso wa Mungu ndio shida
Umesahau Mapadre wanaozaa na wake na binti za watu ndo wanaozitoa hizo sakramenti...
 
Ndio ushangae sasa mkuu. Hawa jamaa wana ibada za wafu. Kiboko yao Martin Luther tu.
Shaangaa ww kutaka uzikwe na wenye ibada za wafu[emoji12]
Kwenda zenu achaneni na KANISA KATOLIKI! Pigeni kelele usiku mtalala, kukicha mtatuona Kanisani baada ya kazi
[emoji116][emoji116]

IMG_20220411_134737.jpg
IMG_20211225_153109.jpg
IMG_20211225_152956.jpg
 
Eti pokea
[emoji116][emoji116]
Pokea gari
Pokea kazi
Pokea mume
Pokea mke
Pokea Ada
Kwa jina la Yeeeeeesu....[emoji1787][emoji1787]
Oh nimesahau Pokea Nyumba
 
Back
Top Bottom