Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

Hii ni aibu kubwa sana kwa serkali ya CCM na wafuasi wake. Tutasikia mengi sana mwaka huu na mpaka kufika 2025 nchi itakuwa imeoza kabisa.
 
Asiwe kama hakimu wa kesi ya sugu kapokea maagizo katoa hukumu kalala mbele

Hivi huyu hakimu si alikataa kujitoa dogo aliposema hana imani nae? Tutegemee hukumu ya namna gani?
Hakimu kukataa kujitoa kwenye kesi sio kujiandaa kulipa kisasi. Mahakimu weledi hutenda kulingana na sheria na kuuchambua ushahidi. Kesi nyingi za serikali zina madoa ya kisiasa na haziwapi shida mahakinu wanaojitambua.
 
Hivi ishu yake na uhamiaji iliishaje.
 
Nae analia nini sasa,kama uko sahihi ujatenda kosa ulie nini.
 
Huyo ni bingwa sana wa kuchanganya dini na siasa. Unakumbuka wakati ule wa dawa za kulevya? siku hiyo alienda kusali makanisa matatu sasa umewahi kuona wapi mkristo anasali makanisa matatu kwa siku moja au mwisilam kuingia kuswali misikiti mitatu kwa sala ya ijumaa tu?
 
Hii hukumu ukiiangalia kwa makini unapata picha nani alimteka Nondo na pia nani ni mhusika mkuu wa utekaji wa watu wenye maoni kinzani na viongozi wa serikali.
 
Hivi serikali wamewahi shinda kesi? Niabu sana kwa serikali na kambuka waziri wa kipindi kile aliongea kwa dharau sana kuwa dogo alikuwa anamfata mpenzi wake. Daahh inaumiza sana
 
Wakuu nimefuatilia katika mitandao naona watu wanatoa pongezi kwa Mahakama kutoa dhamana kwa NH. Zitto na kumwachia huru Abdul Nondo.
Nimebaki na mawsali yasiyokuwa na majibu.
Ivi Mahakama kama chombo cha kutafsiri Sheria inapotimiza wajibu wake kuna sababu ya kupongeza?
Mfano mdogo Baba ukinunua nguo za watoto na mahitaji mengine je kuna sababu ya kukupongeza? Jibu ni HAPANA maana unakuwa unatimiza wajibu.
 
Kupongezwa ni ishara ya kuaminiwa, raia kupongeza mahakama ujue wana imani nazo. Na kupongeza si kosa kisheria.

Japo siku hizi tunashuhudia watu wakipongeza kinafiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…