M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,027
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tusipende kufanya mambo yasiyofika mwisho. Kijana Abdul Nondo alisema katekwa serikali ikasema kajiteka. Leo mahakama inasema Abdul hakujiteka bali alitekwa , jee nani ndio mtekaji wake?
Siku za nyuma wamekuwepo waliotekwa kadhaa na wengine walikuja kupatikana wakiwa wameumia na kujeruhiwa wengine wamepotea kabisa. Kama taifa sio jambo zuri kulinyamazia bali lazima liwe mjadala mkubwa wa wazi utakao shirikisha watu bila kujali vyeo vyao.
Hivi akitekwa na kupotea Zitto au Mbowe tutanyamaza kama ilivyokuwa kwa MO au Azory? au akitekwa na kupotea CAG au Jaji wa mahakama kuu bado tutatulia na kuendelea na shughuli zetu kama wazungu wasemavyo Business as usual?
Tuwajue watekaji sasa badala ya kusemea chini chini kuwa na "kina Fulani" kisha tukasababisha kilio kwao baada ya mabadiliko ya uongozi maana kutakuwa na visasi vya dhahiri.
Ni wakina nani na kwa nini?
Hata hapa naweza kuongea ukweli.Ongea ukweli kuhusu jiwe huko fb au kwenye group za whatsapp ndiyo utaweza kuwa na uhakika kama mahakama zetu zipo huru au laa! [emoji30][emoji30][emoji30]
Hapa ni mafichoni na ni ngumu kuja kuchomolewa huku!!Hata hapa naweza kuongea ukweli.