Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa leo itasoma hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi #Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Katika kesi ya msingi, Nondo anakabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kuwa alitekwa, na kutoa taarifa za uongo, aliyoyatenda Machi 7, 2018.

Mliopo iringa update muwe mnatupa.

-------------- UPDATE-------------

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemkuta Abdul Nondo hana hatia hivyo imemuachia huru
Hizi kwa kweli ni habari njema sana. siyo kwa ile mihemko ya Serikali na "vyombo vya usalama", Nondo kuletwa mbele ya vyombo vya habari kuwaaminisha watanzania kwamba "Alijiteka mwenyewe", Chuo Kikuu kumsimamishia udahili wake, pia kumzuia asiingie maeneo ya chuo. haya yote mawili Utawala wa Chuo Kikuu ulifanya kwa sababu za woga usiomithilika.

Kwanza Nondo alikuwa na ni mtuhumiwa tu, na kwa sheria zetu, ni INNOCENT UNTIL PROVED GUILTY. Sasa "Wasomi wetu waliobobea" wakamhukumu wao kuwa ni Guilty na kumwadhibu. Lakini hata kama angekuwa guilty, kwa nini azuiliwe kuingia eneo la Chuo? kwa mujibu wa katiba, kila raia anao uhuru wa kwenda anapotaka. kama angefanya kosa akiwa ndani ya chuo hayo sasa ni mengine, angeshitakiwa siyo kwa kuingia chuo, bali kwa kutenda kosa.

Ni jambo jema kwamba kijana huyu ametumia vizuri muda mchache na nafasi finyu aliyokuwa nayo, kusimama kwa ujasiri na kutetea UKWELI. Tunahitaji watu wa aina hii wengi sana hapa nchini kwetu, hasa kipindi hiki ambacho watu wazito na wenye heshima katika nchi, wanashindana katika UNAFIKI. Naongelea mfano wa lile Kongamano feki lililofanyika Chuo Kikuu hivi karibuni, ni feki kwa sababu kusema kweli haikuwa Kongamano bali ni mkutano wa KAMPENI kwa ajili ya Magufuli.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa leo itasoma hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi #Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Katika kesi ya msingi, Nondo anakabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kuwa alitekwa, na kutoa taarifa za uongo, aliyoyatenda Machi 7, 2018.

Mliopo iringa update muwe mnatupa.

-------------- UPDATE-------------

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemkuta Abdul Nondo hana hatia hivyo imemuachia huru

View attachment 921914
Abdul Nondo ana kila sababu ya kumshukuru Mungu aliyekua waziri wa mambo ya ndani kutumbuliwa kwakua ndiye aliyeiforce hii case kwakutumia mapolisi wake
 
Wajuvi wa sheria,je anaweza kudai fidia juu ya kupotezewa muda na kuchafuliwa? Na pia je Chuo kinaweza kumpokea ili aendelee na masomo?Pia bodi ya mkopo ya elimu (kisheria)bado itakuwa inamtambua(baada ya kutoonekana kuwa na hatia) kama mteja wao?
 
Yule kinara wa kulia kanisani aliyemtaka dogo aletwe mkoani kwake ili amshughulikie sijui anajisikiaje hivi sasa...
Eti ndiye Amiri jeshi wa vikosi vya ulinzi na usalama mkoa wa Dar es salaam. Jamani imekaaje watu wa Dar kila kukicha kamanda wenu mkuu ni vilio tuu hadharan? hamjisikii aibu?
Kamanda wa hivi anaweza kuona panya chumbani akapanda juu ya kabati kujificha.
 
Back
Top Bottom