Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

Iringa: Mahakama ya Wilaya yamwachia huru Abdul Nondo baada ya kutomkuta na hatia

Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa leo itasoma hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi #Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Katika kesi ya msingi, Nondo anakabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kuwa alitekwa, na kutoa taarifa za uongo, aliyoyatenda Machi 7, 2018.

Mliopo iringa update muwe mnatupa.

-------------- UPDATE-------------

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemkuta Abdul Nondo hana hatia hivyo imemuachia huru

View attachment 921914
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]utabiri wetu umetimia
 
Nasikia imekuwa hivi.


*GOOD NEWS:*
*ABDUL NONDO ASHINDA KESI DHIDI YA JAMHURI KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA IRINGA*

Swali la Hakimu la msingi, ni Je, Jamhuri wameshindwa kueleza kuwa mshatikiwa alifikaje Mafinga?? Pili, mahakama imekosa ushahidi kuhusu alifikaje Mafinga.

Tatu, hakuna ushahidi toka jamhuri kuwa mshatikiwa alikuwa wapi wakati wa tukio. Hivyo mashahidi wa jamhuri wametoa ushahidi wa hisia.

Nne, Jamhuri wameshindwa kuthibitisha uongo wa mshatikiwa kwa kila namna na hata kielelezo kilicholetwa na Jamhuri kinatia mashaka sana, kwa mkanganyiko huu makahama imejizuia kuyaamini maelezo yaliyoletwa mahakamani.

*Ifahamike siyo jukumu la mahakama kujua mshatikiwa alitekwa au hakutekwa, hilo ni jukumu la polisi*.

Hivyo basi, mahakama imeamua Abdul Nondo aachiwe huru.

Mwisho kabisa, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), unawashukuru mawakili wake waliosimamia kesi ya Abdul Nondo tangu mwanzo, lakini kipekee zaidi tunaishukuru mahakama kwa kutenda haki katika hukumu hiyo.

Imetolewa leo tarehe 5 Novemba 2018.
Na: THRDC
 
Mahakama zetu ziko vizuri...
Ongea ukweli kuhusu jiwe huko fb au kwenye group za whatsapp ndiyo utaweza kuwa na uhakika kama mahakama zetu zipo huru au laa! [emoji30][emoji30][emoji30]
 
Nadhani ni walewale waliomteka Mo, Ben Saanane, Azory na mum pyu pyu pyu Tundu Lissu. Ndo maana mpk leo pamoja na umahiri wa kesho letu, bado hawajafahamika na hawafahamiki...

Nadhani ni alliens...
It's so hectic
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa leo itasoma hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi #Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Katika kesi ya msingi, Nondo anakabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kuwa alitekwa, na kutoa taarifa za uongo, aliyoyatenda Machi 7, 2018.

Mliopo iringa update muwe mnatupa.

-------------- UPDATE-------------

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemkuta Abdul Nondo hana hatia hivyo imemuachia huru

View attachment 921914
Ila huyu binti kakaa kimtego mahakamani jamani
 
Wajuvi wa sheria,je anaweza kudai fidia juu ya kupotezewa muda na kuchafuliwa? Na pia je Chuo kinaweza kumpokea ili aendelee na masomo?Pia bodi ya mkopo ya elimu (kisheria)bado itakuwa inamtambua(baada ya kutoonekana kuwa na hatia) kama mteja wao?
naungana na ww kusubiri ufafanuzi
 
Tusipende kufanya mambo yasiyofika mwisho. Kijana Abdul Nondo alisema katekwa serikali ikasema kajiteka. Leo mahakama inasema Abdul hakujiteka bali alitekwa , jee nani ndio mtekaji wake?
Siku za nyuma wamekuwepo waliotekwa kadhaa na wengine walikuja kupatikana wakiwa wameumia na kujeruhiwa wengine wamepotea kabisa. Kama taifa sio jambo zuri kulinyamazia bali lazima liwe mjadala mkubwa wa wazi utakao shirikisha watu bila kujali vyeo vyao.
Hivi akitekwa na kupotea Zitto au Mbowe tutanyamaza kama ilivyokuwa kwa MO au Azory? au akitekwa na kupotea CAG au Jaji wa mahakama kuu bado tutatulia na kuendelea na shughuli zetu kama wazungu wasemavyo Business as usual?
Tuwajue watekaji sasa badala ya kusemea chini chini kuwa na "kina Fulani" kisha tukasababisha kilio kwao baada ya mabadiliko ya uongozi maana kutakuwa na visasi vya dhahiri.
Ni wakina nani na kwa nini?
 
Back
Top Bottom