Iringa mjini mtu ukiumwa usiku unaweza kufa, hakuna Hospitali au Zahanati wanayokesha.

Iringa mjini mtu ukiumwa usiku unaweza kufa, hakuna Hospitali au Zahanati wanayokesha.

Perry

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
10,058
Reaction score
2,195
Habari Zenu wakuu.

Nimekuja Iringa mara moja kikazi, sasa usiku wa kuamkia leo mwili ni kama ulibadilika nikapata kitu kama homa kali sana, ilikua ni kama saa 9 usiku hivi nikasema ngoja nivumilie kukikucha tu niwahi hapo Aga Khan.

Lahaula kwenye saa 12 alfajiri na madakika hivi nikamchukua boda nikamwambia aniwahishe Aga Khan cha kushangaza nikakuta bonge ya kufuli kupiga simu wakanijibu mpaka saa mbili asubuhi ndio watafungua nikatoka nikaenda Marie Stopes napo jibu ni hilo hilo.

Nikamwomba boda anipeleke tu dispensary yoyote ya mtaani anayoijua kwa msaada zaidi kwani nilikua najihisi hovyo, cha kushangaza kila dispensary tunayoenda inakua imepigwa kufuli..nilikua sitaki kwenda hospital ya serikali ila ikabidi tu nimwambie boda anipeleke hospital ya rufaa ya mkoa wa iringa.

Huko nako ndio vichekesho, kwanza manesi na madaktari hawako serious na kazi ni mwendo wa kutomasana tu kila saa, hawana maadili ya kazi na ni kama wamejikatia tamaa ya maisha..wakanichukua vipimo ambavyo baada ya majibu kutoka nikaandikiwa dawa,kwenda pharmacy pale nikaambiwa hawana Amoxillin wala paracetamol hivyo kama naweza niende nirudi saa 6 mchana au nikajinunulie mwenyewe.

Hili suala binafsi limenishangaza sana as huduma za msingi kama afya zinatakiwa kutolewa kwa masaa 24 kwani mtu hachagui aanze kuumwa muda gani inatokea tu automatically.

Kajifunzeni mikoa ya wenzenu jinsi watu wanavyochapa kazi usiku na mchana.
 
Hata mchana waweza kosa huduma...who cares?
 
Wanasema kazi za afya ni wito lakini kama hakuna pesa hata morali ya kazi hamna. Hao madaktari na manesi Nathaniel hawajalipwa call zao na extra ndiyo maana
Mkuu,kazi ni za wito ndio hatukatai.lakini hakuna aliyeshikiwa mtutu kuzifanya.
 
Kwahiyo hiyo hospitali wameajiriwa wahehe pekee?

Hospital za serikali kukosa dawa inawezekana kabisa kutokana na taratibu za manunuzi.

Ila dawa zina mbadala. Huyo pharmacist ilibidi atafute mbadala wa ulichoandikiwa.

Kama unaona kuna shida yoyote kwenye huduma mpigie simu DED au TMO
 
Watani zangu mbona wachapakazi Sana, labda hao watumishi ni watu wa mikoa kingine...😂😂
 
Back
Top Bottom