TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

hivi watasema tena kapigwa na kitu kizito? halafu si ni huko huko chanel ten ndo walitumia kujisafisha baada ya mauaji ya Moro? Jamani vyombo vyetu vya habari muwe mnatendea haki taaluma yenu. vinginevyo na nyinyi mjue hamko salama hata kidogo chini ya uongozi huu dhalimu.

what goes araundi kamu araundi,,,,ndio maana kuna watu huwa wanasema hapa vyomba vyetu vya habar vya tanzania si vya kuaminika na hutumika kama tissue kufutia mkojo,,,mmeona????waliwapa kavareji polisi je na leo watawapa kavareji????
 
vyombo vya ulinzi viache kutumia nguvu nyingi kwa watu wasio hata na siraha,hii inaleta chuki sana kwa wananchi na kupunguza imani kwa jeshi lao.

oneni maandamano ya nchi nyingine,waandamanaji wanazuiwa na sio kuwapiga risasi ama mabumu
 
Habari zipo nyingi hata wewe hujui kilichotokea kuna wengine wanasema kapigwa bomu wengine risasi labda tuambie wewe habari ya uhakika.
Swali lako ulilojibiwa uliuliza sababu na siyo ameuwawa na kitu gani,don't confuse yourself.Swali la kuhusu ni kitu gani kilimwua pia ulishajibiwa,wewe ulisema inakuwaje bomu limuuwe peke yake.Sijui huwa unafikiriaje wewe?!unatumia vitu gani?are you on medication?
 
Ishakuwa noma, R.I.P. Mwandishi tunajua umefia kwenye taharuma yako
 
Kwa mara ya kwanza toka nikujue leo umeandika kitu kikanifurahisha

Tumezubaa kweli sio uongo........kazi kubwa tunayoijua ni kulalamika kwenye keyboard bila kuchukua hatua!

Kweli kabisa Mkuu!!
Wananchi waliuliwa Arusha tukakaa kimya,Juzi polisi wameua Morogoro,sisi kimya,wameua wengine North Mara,kimya!!Leo wameua mwandishi itapita kimya!!!!
Natamani nione mshikamano wa Vyombo vya habari kutoa TBCCM
 
Unajua mazingira aliyokuwa wakati anapigwa risasi? polisi walikuwa wana-target waandishi wa habari, au alikuwa katikati ya umma?
wewe mbona unakua hivi??

kwahiyo kama alikua katikati ya umma ni sawa kuuwawa sio??........... do you want to justify police shooting people ?

this is the stupidest comment i have ever read in JF
 
jamaa kafariki.soc ITV.
CCM WANAMPANGO WAKUUA WATAFUTA HAKI ILI KUZUIA MABADILIKO YA KIUTAWA.KWA KUA MUNGU YUPO WATAABIKA SIKU SI NYINGI.
 
CHADEMA itatumaliza watanzania!
Hiki chama hakitufai ata kidogo aise.......
 
Na yeye alikua anafanya nn huko?

yeye ni muandishi wa habar, ivyo ni jukumu lake kuwepo hapo na kuchukua habari na hali ya kuwa hao polisi wanalazimika kuhakikisha usalama wake akiwa hapo! mtoto wa mjini vipi wewe bana mona unaniambisha sasa
 
DAUD MWANGOSI......kapigwa na bomu wakati akiwa kazini kwenye kufungua shina na ofisi ya CHADEMA....KAFARIKI HAPO HAPO NA UTUMBO KUTOKA NJE.

RPC ALIHOJIWA NA ITV NA HAKUTOA JIBU NA KUKATA SIMU...!! NGOJA TUSIKILIZE CHANNELL TEN SASA HIVI TUTAWAJUZA MORE.
 
Ndio maana serikali iliongeza posho ya kuchunguza maiti kwa madaktari na sio ya mazingira hatarishi,wala mazingira magumu wala kununua vifaa vya hospitali,wala kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwe mahospitali,ila wachunguza maiti yaani [Forensic Pathologist] wanavuta laki kwa maiti,kuna tetesi za kuongeza vyumba vya maiti na kuviongezea ukbwa zaidi,kwasababu mauaji yataendelea!!
 
sichangii hadi nipate habari za uhakika

unafanya nini hapa kama unaona hakuna habar za uhakika hapa,,,usingefungua uzi kabisa,,,,hao unaowaona wanaripot habar za uhakika wengi wao wanazitoa habar hapahapa
 
IMG_1935.JPG

IMG_1917.JPG

Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi
IMG_1943.JPG

Mwili%2Bwa%2B%2BDaudi%2BMwangosi%2Bukiwa%2Bumechanika%2B%2Bvibaya.JPG

Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini
IMG_1983.JPG

Gari%2Bya%2Bkamanda%2Bwa%2B%2Bpolisi%2Bmkoa%2B%2Bwa%2BIringa%2BMIchael%2BKamuanda%2Bakiongoza%2Bmsafara%2B%2Bwa%2BFFU.JPG

Daud%2BMwangosi%2B%2Bkulia%2Benzi%2Bza%2B%2Buhai%2Bwake.JPG

Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake
ofisi%2Bya%2BChadema%2BNyololo%2Bikifuk%2Bmoshi%2B%2Bwa%2Bmabomu.JPG


Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.
 
Mwwenyekiti na Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na mwandishi wa habari wa Channel 10 amepigwa risasi na polisi kwenye mkutano wa CHADEMA Mufindi

Ni kweli amekufa confirmed RIP Mwangosi
 
nadhani ni too much of a too much tonavyokaa na kulalama kwenye keyboards tu

Tangua mauaji ya polisi kwa raia yaanze (zaidi ya miaka miwili sasa); sijasikia mkuu yoyote wa polisi iwe kata, wilaya, mkoa taifa aliyechukuliwa hatua yoyote zaidi ya wao kutoa matamko yasiyo na maana kwenye media

NA USISHANGAE UKAONA HATA MEDIA, AMBAYO SASA IMEGUSWA DIRECTLY, BADO KWA KUPITIA BROWN BAGS, IKAKAA KIMYA
This time Police are in for it
 
CHADEMA itatumaliza watanzania!
Hiki chama hakitufai ata kidogo aise.......

chadema au polisi ndo watatumaliza! sababu ya kutumia risasi hapo ikowapi? yani wanashindwa njia za kutuliza vurugu mpaka utumie risasi ndugu, tusilete uchama kwenye maswala ya msingi mkuu! hawa jamaa wanatumia nafasi ya upolisi kinyume na kanuni za kazi yao
 
Kweli kabisa Mkuu!!
Wananchi waliuliwa Arusha tukakaa kimya,Juzi polisi wameua Morogoro,sisi kimya,wameua wengine North Mara,kimya!!Leo wameua mwandishi itapita kimya!!!!
Natamani nione mshikamano wa Vyombo vya habari kutoa TBCCM

Yaani huu ukimya wetu wananchi ndio unawafanya wazidi kuua kila kukicha......na wataendelea kuua sana manake washatuona mazumbukuku......wanajua tutasema tutachoka na maisha yataendelea kusonga! Inauma sana asee yaani sana marejesho! Tusubiri tuone huo mshikamano kama upo basi!
 
Last edited by a moderator:
Hilo bomu limemuua peke yake?

Ulitake wafe wangapi? Au kwa kuwa wewe upo upande wa Jeshi la Polisi la Kua Wananchi, yaani nguvu ya SSM? Kifo ni kifo tu na ni lazima tusikitike hata kama tuko na itikadi tofauti ya siasa. So sad. Haya mambo yataisha lini Tanzania?
 
nyie lazimisheni maandamano lakini hayo maandamano ndio mnatafuta kutoweka kwenye ramani ya vyama vya siasa, iko wapi cuf ngunguri, wapi Nccr , kimsingi hiyo huruma mnayotaka kutoka kwa wananchi hamtaipata kwa staili ya maandamano

:alien:
 
Back
Top Bottom