Heshima yako mkuu Royals,
Kama nilivyoendelea kusikia kutoka kwa wengine pia waliochangia, naomba radhi kama nilikukwaza.
Mungu Ampumzishe mahali pema mwandishi wetu Daudi Mwangosi na Awape faraja wote walioguswa na msiba huu mzito.
Ninaamini ya kuwa kifo chake na vifo vya wengine wengi waliouawa na vyombo vya dola katika kutafuta haki ya wanyonge havitakuwa vya bure. Walioko madarakani wamejisahau, lakini ukweli unabaki pale pale.
Mwisho wa ccm ni huu. Udhalimu sasa basi. Hakuna katika historia duniani kote utawala ulioweza kuendelea baada ya kuanza kuwaua wananchi wasio na hatia ambao kosa lao tu ni kutetea haki za wanyonge!
Pumzika kwa Amani Daudi Mwangosi!