TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

Jeshi hili livunjwe rasmi kama ilivyovunjwa "Scorpion" ya South Africa.
 
Msitujumlishe watanzania wote, andamananeni na wapuuzi wenzenu. Mkifuata sheria mnapungukiwa nini?

wewe maskini wa mawazo!kuchoma file za cdm ndo kufuata sheria?kumuua mwandsh wa habari pia ni sheria?naifahamu katiba nieleze hvo vifungu.je kuendelea kwa mikutano ya ccm ndo sheria?acha upumbavu wewe!
 
Advicer, hebu mshauri huyu jamaa, kwani hajui asemalo.
 
Mambo mawili yanatakiwa kufanyika ili kumaliza hili tatizo.
1.Askari wote walio husika washitakiwe,RPC asimamishwe kazi,IGP asimamishwe kazi.
2.Chadema ifutwe.

lazima uwe unatumia miguu kufikiri sio kichwa. tafsiri ya kuuwa adhabu yake kusimamishwa!
 
Pumzika kwa amani kaka yangu nakukumbuka kwa mengi sana mungu akulaze mahali pema peponi.
 
Hawa polisi kama bado wanajifunza kuua, basi raia sasa tunajifunza kuuawa. Kumbukeni kuwa nyie polisi mnaendelea kuongeza idadi ya watanzania wanaoichukia serekali kwa hizi tabia zenu.
 
Watu watashangilia kifo cha Mwangosi. jamani hivi vifo si vizuri ni Ishara mbaya kwa nchi hii.
 
death of one by police bullet/gun id too many. is there a way for our independent lawyers can file a case in the ict-what are we waiting for?hivi jk ataiacha nchi yetu salama au ndo ya Syria?
 
Ulinzi shirikishi na askari jamii vitatoka wap kwa hali kama hii. Askari sasa ni adui wa raia badala ya kuwalinda.
 
hata channel Tena hawajaonyesha hii habari?
Vituo vya tv vinakua kama vimefungwa na serikali hii habari haijaonyeshwa kwenye taarifa ya habari yoyote ni aibu kubwd sana kuwa na vyombo vya habari kama hivi
 
Bado Polisi Tanzania wanashangaza pamoja na malalamiko ya wananchi bado hawataki kusikia na kushaurika, nguvu wanazotumia zingetumika pia katika kuyalinda maandamano na mikusanyiko ...... .... R. I. P Mwangosi
 
viongozi wa chadema mnawindwa kwa udi na uvumba,msifanye makosa tutawakosa kabla ya 2015,mwangosi aliwasumbua sana iringa kwa kusimamia haki
 
Mpaka dakika hii , hatujaona hiyo taarifa ya mauaji yaliyofanywa na Police ! Why? Why?.

Aliyepata na tatizo hili ni Mtanzania mwenzao, katika nchi yao, and above all MWANDISHI MWENZAO..lakini mambo wanayoyafanya ni haya??!

ITV, people rely on you for information, news, updates at times b'se you call yourselves INDEPENDENT TV (ITV), But this is what you do among family(profession)!!
-what info to the public do you give?
-what abt to your viewers and fans?
-and young journalists?

It's unfair, inhuman and disgusting.
 
577101_377757872294889_183352309_n.jpg


Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC),
Daudi Mwangosi, ambaye polisi wamemwua kijijini Nyororo Iringa

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisui na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hali ilivyokuwa

IMG_1935.JPG
IMG_1917.JPG
IMG_1943.JPG
Mwili%2Bwa%2B%2BDaudi%2BMwangosi%2Bukiwa%2Bumechanika%2B%2Bvibaya.JPG
IMG_1983.JPG
Gari%2Bya%2Bkamanda%2Bwa%2B%2Bpolisi%2Bmkoa%2B%2Bwa%2BIringa%2BMIchael%2BKamuanda%2Bakiongoza%2Bmsafara%2B%2Bwa%2BFFU.JPG
Daud%2BMwangosi%2B%2Bkulia%2Benzi%2Bza%2B%2Buhai%2Bwake.JPG
ofisi%2Bya%2BChadema%2BNyololo%2Bikifuk%2Bmoshi%2B%2Bwa%2Bmabomu.JPG
 
Ukiangalia mtiririko wa taarifa ni kama CDM wameanza kujitoa mhanga kwa mabomu ya kujilipua wenyewe,hongera Dr Slaa kwa kuendeleza vurugu na kusababisha mauaji.

una upeo mdogo sana! Inaonekana umeishia darasa la nne!
Mwenye utu hawezi kutoa maneno kama hayo!
 
Hivi chadema lazima waivuruge hii nchi,hawa kweli ni watanzania? Huu sio uroho wa madaraka tena.
 
Back
Top Bottom