Iringa na Njombe ilivyoshambuliwa na chawa

inasikitisa lakini,
but hizo ndio indicator za nchi ya uchumi wa kati (sick)
5 tena oyeee
 
mimi chawa simjui na sijawahi kumuona ila kunguni balaa lake siyo la kitoto, wakikushambulia kwa muda mrefu unaweza ukaugua kiharusi.
kunguni nmemfahamu nikiwa secondary nakaa hostel
 
Hawa wadudu ni ishara njema kwetu hatujui tu. Ukiona mdudu ujue upo kwenye mazingira halisi (nachuro) kwa binadamu. Hawa wadudu wanakufa kirahisi sana sehemu yenye makemikali.
Kenya inaongoza EA kwa watu walioathirika na wanaokufa kutokana na funza hao. Kuna mashirika kabisa yanasaidia kupambana na hao funza na chawa jaribu kuingia youtube search "jigger in kenya" utajionea
 
Funza wanaingia ndani ya mguu inamaana?
Kiroboto kinapenya miguuni baadae kinanenepa kwa kunyonya damu. Linakuwa jeupe kama punje ya kunde. Ndani linakuwa na mayai kibao. Kama halijatolewa, hayo mayai yakitotolewa yanasambaa sehemu zingine za miguuni.
 
Ukweli mtupu! Nimetembelea maeneo ya Malangali, Ifunda, Nyololo, Makambaku, Ulayasi na Madaba chawa ndio kwao na mimi nimeondoka nao.

Nimerudi Same nimefua nguo kwa maji ya moto nikanyoa na mkulungu (kipara) angalau sasa nina ahueni.
Ukijipulizia na Marashi
 
Tatizo hawaogi, dawa ya chawa usafi (kwa uzoefu wangu)

halafu, hv funza ndo wapoje eti na wanasababishwa na nini? Nawasikia tu hawa wadudu.
 
Ubaridi unasingiziwa tu, issue ni uchafu.

Chawa wapo mikoa yote ila viunoni mwa wachafu tu.

Hao jamaa Wana tabia ya kutaga mayai kwenye "pindo" za nguo hasa viunoni.
Hata uache kuivaa hiyo nguo mwezi,siku ukiivaa tu lile joto la mwili linatotolesha mayai 😁 unaanza kupiga tena gitaa.
 
Ukweli mtupu! Nimetembelea maeneo ya Malangali, Ifunda, Nyololo, Makambaku, Ulayasi na Madaba chawa ndio kwao na mimi nimeondoka nao.

Nimerudi Same nimefua nguo kwa maji ya moto nikanyoa na mkulungu (kipara) angalau sasa nina ahueni.
Jamani! Jamani!,acheni kutudhalilisha,huo ulikuwa ni uchafu wako.
 
Wewe jamaa itakuwa tu Wewe mwenyewe sio msafi.chawa na funza wapo kila sehemu,ishu hapo ni usafi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…