Iringa Wanazalisha mbao, lakini Wanafunzi wa Iringa wanakaa Chini. Samia Suluhu hajali


KUTENGENEZA MADAWATI NALO LINAMUHITAJI RAISI??
Kule kilimanjaro utengenezaji wa madawati ya shule upo ngazi ya kijiji na kata wala sio wilaya na utekelezaji wake ni 100% ndio sababu hakuna mwanafunzi anakaa chini
TUTIMIZE WAJIBU WETU KAMA WANANCHI SIO KILA KITU KUSUBIRI RAISI!!!
 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Igeleke iliyopo katika Manispaa ya Iringa wanakabiliwa na mazingira magumu ya kujifunzia kutokana na uhaba mkubwa wa madawati unaowalazimisha baadhi yao kukaa chini wakati wa masomo.

Kipoti hicho kimebainika wakati wa sherehe za mahafali ya darasa la saba zilizofanyika shuleni hapo. Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Bi. Sikudhani Lucas, amethibitisha kuwa shule hiyo ina upungufu wa jumla ya madawati 106, hali inayokwamisha utulivu na ufanisi wa wanafunzi wanapokuwa darasani.

"Kwa kweli katika shule yetu ya msingi Igeleke tuna upungufu mkubwa wa madawati ambao unapelekea wanafunzi kukaa chini... Upungufu wetu mpaka sasa ni madawati 106," alisema Bi. Sikudhani Lucas.

Akizungumza katika mahafali hayo, Mgeni Rasmi Wakili Moses Ambindwile ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa elimu ndani na nje ya Mkoa wa Iringa, pamoja na waliosoma shuleni hapo kujitokeza kushirikiana na serikali ili kuboresha miundombinu na kumaliza changamoto hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Bwana Geoffrey Ngolo, alieleza kuwa kamati hiyo ilishatuma barua za maombi ya msaada kwa Mkurugenzi na wadau mbalimbali na bado wanaendelea kusubiri majibu ili kupata ufumbuzi.
Your browser is not able to display this video.
 
Hiyo maana umeitoa wapi? Mimi maana ni yangu ni hilo lizanzibari halitufai. Kauza bandari kwa DP, hela alipeleka oman halafu kakupa vocha uje kutetea ujinga wake
Ahaa kumbe issue yako ni Samia! Huyo ndo Rais wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu unapenda hupendi labda uhamie Burundi..
Sasa umeacha la madawati umehamia DPW!
 
Hoja nyingine za kingese sana
 
Sasa hapo kuanzia Halmashauri, Ofisi ya mkuu wa wilaya na mkoa wako wapi?, mbunge Yuko wapi? Hao watu ndio wanaohusika maana wako karibu na eneo Hilo tajwa, vitu vya Aina hii ni vya kumaliza haraka Sana kule kule chini.
 
ukishaona neno tanganyika , watanganyika lina tajwa kwa kasi, we jua tu hapo hata kinacholalamikiwa sio kinachotajwa
 
Tatizo ni sa100 huwa anatoa maelekezo mbao za wanairinga zipelekwe zanzibar ili wanafunzi wa zanzibar wanemeeke na sisi watanganyika tunabaki tunateseka
 
Sijui huwa kinatokea nini, mfano mwanza samaki wakubwa hawapo mimi nikajua sikuhizi wanavuliwa wakiwa bado! Nashangaa mahotelini, fillet factories na mkoa kama dar wana sangara wakubwa tena fresh wanapatikana kwa urahisi🤔
soko lipo huku walaji wapo huku, imefikia wakati mtu mwenye ng'ombe 40 , mbuzi 20 heka zaidi ya 20 anataka kumpiga mzinga mwenzake ambaye yupo aganga njaa kwa kua anatoka Dar
 
Halafu kwa unafiki wa viongozi wetu kipindi Cha uchaguzi utasikia wanamwambia Rais hatukudai chochote wewe ndiyo unatudai sisi kura.

Kuna muda unakaa chini ukitafakari aina ya viongozi tulionao unajikuta moyo wako unajaa hasira na ghadhabu
 
wengi wanalalamika bila plan maalumu ya kueleweka tu
Vijiji unakuta vina mashamba ya miti ukienda kununua huko Serikalini utalipia tozo tu ila mzigo wote unabaki hapo kijijini si wachane mbao wapeleke kwenye hizo shule waone kama zitakataliwa..
 
WHO CARES?
 
Vijiji unakuta vina mashamba ya miti ukienda kununua huko Serikalini utalipia tozo tu ila mzigo wote unabaki hapo kijijini si wachane mbao wapeleke kwenye hizo shule waone kama zitakataliwa..
na muda huo wanaweza wakawa wanapanda miti mingine kwa miaka ijayo,
shida karibu kila mtu hataki kuhusika kuanzia ngazi ya kata haki huko juu ,
miezi kama miwili tulikua na kikao kijiji fulani alifika diwani pale, huwezi amini diwani aligeuka kua ndo mtetezi wa mkuu wa wilaya na serikali. hapa kuna afya kweli?
 
Hivi tuseme ukweli,
Mwenyekiti wa mtaa ambayo hy shule ipo ameshindwa kuitisha mkutano ku mobilize wazazi, wafanyabiashara, taasisi na mashirika katika eneo hilo wakachanga pesa kupata madawati 100+kwa ajili ya watoto wetu?
Tanzania watu wengi ni wajinga sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…