Is it worth it kununua Brevis milioni 6 na kuigeuza kutumia mfumo wa gesi kwa mizunguko ya town ?

Is it worth it kununua Brevis milioni 6 na kuigeuza kutumia mfumo wa gesi kwa mizunguko ya town ?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Gari ni Brevis

Kwa hali ya sasa ilivyo mafuta yapo juu sana, watu wengi wanayauza kwa bei ya kutupa hata milioni 5 lqkini kupata clean kidogo inaweza kuwa milioni 6

Makadirio ya kufunga gesi ni Milioni 2

Makadirio ya Service yanaweza kuwa milioni 1

Kwa hio gharama zote zinakuwa MILIONI 9

Is it worth it ?
 
Tuanzie gharama za kuinstall huo mfumo bei gani.
 
Kwahiyo jumla kama Mil 8.5? Bado Brevis ya Mil 6 itahitaji service kama ya 2 Mil?

Me naona bora utafute pesa pengine ununue gari nyingine.
Services milioni 2 zipo juu sana, gari zinauzwa zikiwa zipo good condition lakini bado watu wanazikimbia

Bei ya gari milioni 6

Gharama za kufunga gesi ni milioni 2 kwa kg 15

Kumbuka hata Raum Mpya huwezi kuipata kwa nusu bei, zinaanzia kwenye 21
 
Gari ni Brevis

Kwa hali ya sasa ilivyo mafuta yapo juu sana, watu wengi wanayauza kwa bei ya kutupa hata milioni 6

Je yafaa kununua na kubadili kuweka mfumo wa gesi kwa mizunguko ya town ?

Makadirio ya kufunga ni Milioni 2..

Kwa hio gharama zote zinakuwa MILIONI 8

Is it worth it ?
Hakikisha bei ya juu kabisa umenunua brevis iwe ni M3 kushuka chini.

Kama ishu ingekua bei za mafuta ndio zinaporomosha thamani ya magari basi VII EITEE zingeuzwa bei ya vitz.

Hayo ma Brevis ni yeboyebo sana, ugonjwa wake mkubwa ni busta la breki(hili busta mimi ofisini kwangu naliuza 700k). Likianza kusumbua hili hakuna rangi utaacha kuona.

Ugonjwa mwingine ni vitasa vya nje, kitasa cha dereva ofisini kwangu nauza 400k - 350k. Vingine @ 250k

Mara mia Ni bora ukachukua gx 110 kuliko brevis.
 
Kuweni na huruma jamani, mnyama kama 1jz-fse ukamlishe gesi kweli, mbona humtendei haki!
 
Hapana, haichomoi kiuchumi wala kiufundi kufanya hivyo kwa mizunguko ya mjini pekee na hata mikoani.

Ingawa bei ya kuinunua Toyota Brevis kwa TSh Milioni 6 ni ya kuvutia sana, gharama za mwanzo za ufungaji wa mfumo wa gesi (CNG) na changamoto za kiufundi za injini za Brevis zitakula faida yote unayofikiria kuipata.

1. Changamoto za Kiufundi (Injini za Brevis)Injini za D4 (Direct Injection)
Toyota Brevis nyingi zinakuja na injini za mfumo wa D4 (kama 1AZ-FSE ya CC 2000 au 2JZ-FSE ya CC 3000).

Injini hizi zina changamoto sana kufungwa mifumo ya CNG ukilinganisha na injini za kawaida (VVTi).

Gharama Kubwa ya Kit:
Mifumo ya gesi ya injini za Direct Injection (DI) ni ya gharama kubwa zaidi (sequential kits za hali ya juu) na inahitaji mafundi wabobezi sana ili gari isiyumbe au kuzima hovyo mjini.

Ulaji wa Mafuta mchanganyiko..!
Kwenye injini za D4, gari haiwezi kutumia gesi pekee kwa 100%. Inalazimika kuchoma asilimia fulani ya petroli ili kupoza fuel injectors zilizopo ndani ya chemba ya mwako. Utajikuta bado unajaza petroli mara kwa mara.
 
kwa hiyo 6m kwa maoni yangu ni bora uende kwa mark2 grande ya 1G alafu ndo ufunge gesi ? maana nazo bei yake mserereko
 
kwa hiyo 6m kwa maoni yangu ni bora uende kwa mark2 grande ya 1G alafu ndo ufunge gesi ? maana nazo bei yake mserereko
Halafu hii engine ya 1G itamstiri sana maana ni vumilivu.
 
Back
Top Bottom