Hapana, haichomoi kiuchumi wala kiufundi kufanya hivyo kwa mizunguko ya mjini pekee na hata mikoani.
Ingawa bei ya kuinunua Toyota Brevis kwa TSh Milioni 6 ni ya kuvutia sana, gharama za mwanzo za ufungaji wa mfumo wa gesi (CNG) na changamoto za kiufundi za injini za Brevis zitakula faida yote unayofikiria kuipata.
1. Changamoto za Kiufundi (Injini za Brevis)Injini za D4 (Direct Injection)
Toyota Brevis nyingi zinakuja na injini za mfumo wa D4 (kama 1AZ-FSE ya CC 2000 au 2JZ-FSE ya CC 3000).
Injini hizi zina changamoto sana kufungwa mifumo ya CNG ukilinganisha na injini za kawaida (VVTi).
Gharama Kubwa ya Kit:
Mifumo ya gesi ya injini za Direct Injection (DI) ni ya gharama kubwa zaidi (sequential kits za hali ya juu) na inahitaji mafundi wabobezi sana ili gari isiyumbe au kuzima hovyo mjini.
Ulaji wa Mafuta mchanganyiko..!
Kwenye injini za D4, gari haiwezi kutumia gesi pekee kwa 100%. Inalazimika kuchoma asilimia fulani ya petroli ili kupoza fuel injectors zilizopo ndani ya chemba ya mwako. Utajikuta bado unajaza petroli mara kwa mara.