- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwa na machapisho kadhaa yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya na Tanzania, yakidai kuwa kijana Mtanzania, Isaiah Yunge, ametoa zaidi ya shilling billion 7 za Kenya ili kufanikisha ndoa yake na bintiye William ruto huko nchini Kenya
Miongoni mwa machapisho hayo kuna ujumbe unaodaiwa kutolewa na Isaiah Yunge ukisema:
I paid 7 billion Kenyan shillings as dowry for my beautiful wife Charlene Ruto. I added 2 choppers to the first family and also awarded my in-law George one nganya bus. I also bought my wife Charlene a golden ring worth 56 million. That is the little I could afford. I thank my father-in-law Dr. William Ruto for accepting my humble dowry.
Aidha, baadhi ya machapisho yamekuwa yakisambaza nukuu inayodaiwa kutolewa na Charlene Ruto, ikisema:
“Kwanzia leo mimi naitwa Charlene Yunge. Msiniite Charlene Ruto. Pia mimi ni Mtanzania sasa. Sitaingia mambo yenu ya Kenya hata kidogo. Jameni, kupendwa raha, ribo ribo.”
Hata hivyo, ufuatiliaji wa taarifa kwenye akaunti rasmi za Isaiah Yunge haujaonesha ushahidi wowote wa yeye kutoa kauli kwamba amelipa mahari ya Shilingi bilioni 7 za Kenya kwa ajili ya kumuoa Charlene Ruto.
Vilevile, hakuna ushahidi unaoonesha kuwa kauli hizo zilizoambatanishwa na jina la Charlene Ruto zilitolewa na yeye kupitia akaunti zake rasmi.
Kwa upande mwingine, vyombo kadhaa vya habari nchini Kenya bado havijaweka wazi kiwango cha fedha kilichotolewa kama mahari katika tukio hilo. Radio 47, kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa, pia imeeleza kuwa madai kuhusu kiasi hicho cha fedha ni ya upotoshaji, huku ikibainisha kuwa wahusika wa ndoa hiyo hawajathibitisha kiwango cha mahari kilichotolewa.
Pia, nukuu zinazodaiwa kutolewa na Isaiah Yunge na Charlene Ruto kuhusu ndoa hiyo hazijaonekana kwenye akaunti zao rasmi.
Hata hivyo kurasa za Kenya news flash kwa siku za hivi karibuni zimekuwa zikichapisha taarifa potoshi na nukuu potoshi juu ya masuala mutambuka nchini Kenya hivyo kutibitisha kuwa taarifa hiyo ni potoshi
Sambamba na hivyo rais wa Kenya William ruto alichapisha kwenye mitandao ya kijamii wa facebook kuhusiana na ndoa akisema kuwa “Today, mama Rachel ruto and I celebrate with grateful hearts as our daughter Charlene begins a beautiful new chapter with her fiancé, Isaya. Congratulations to you both on your engagement. May God bless your union, deepen your friendship and fill the home you build together with love, joy and enduring peace.As your parents, we are proud of you, we rejoice with you, and we will always stand beside you.
Sambamba na hilo, kumekuwa na nukuu potofu zinazosambazwa kupitia machapisho yanayohusiana na tukio hilo la jana. Mojawapo ya nukuu hizo potofu inahusishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye inadaiwa alitoa tamko kuhusu ndoa hiyo. Hata hivyo, Rais Samia Suluhu Hassan hajatoa tamko lolote kuhusu ndoa hiyo.