Isaya Yunge, Kijana kutoka Mwanza, anamuoa binti wa Rais wa Kenya, Charlene Ruto, Hii hapa Cv Yake

Isaya Yunge, Kijana kutoka Mwanza, anamuoa binti wa Rais wa Kenya, Charlene Ruto, Hii hapa Cv Yake

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
1786220901083.png


Leo Agosti 8, nchini Kenya tukio kubwa ni engagement ya Charlene Ruto ambaye ni binti wa Rais Ruto. Katika tukio hilo, ametambulisha mumewe mtarajiwa ambaye ni Mtanzania Isaya Yunge. Historia yake si kubwa sana mtandaoni ila nimepata hints hizi. Kwanza jamaa kasoma IFM Bachelor of Science Degree in Insurance and Risk Management.

Isaya Yunge amewahi kutajwa na Forbes Africa 30 Under 30 miongoni mwa vijana wanaoleta mabadiliko barani Afrika. Pia, alitunukiwa The Queen’s Young Leaders Award 2018 na Malkia Elizabeth II, kwa kutambua mchango wake katika kutumia teknolojia kuboresha maisha ya jamii kupitia suluhisho endelevu za kidijitali.

1786221193542.png


Akiwa na umri wa miaka 17, Isaya alichaguliwa kuwa Balozi wa Vijana wa UNICEF Afrika kati ya mwaka 2007 hadi 2008, nafasi iliyompa fursa ya kuhutubia Mkutano wa G8 katika kuhamasisha na kutetea haki za watoto mbele za marais akiwemo Putin (slide uone picha akiwa na Rais Bush).

Lakini kabla ya hapo mwaka 2006 hadi 2007 alikuwa Mwenyekiti wa Tanzania Junior Council akiwakilisha watoto katika majukwaa ya kimataifa.

Huyu jamaa pia amepata mafunzo mbalimbali katika maeneo ya uongozi na biashara, ikiwemo Sustainable Business Models kupitia Swedish Institute, Leading Change kutoka Cambridge University, pamoja na kushiriki Harvard Ministerial Leadership Program.

Ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Goodsam Technologies, na ameanzisha Smart Kaya LLC, kampuni inayotengeneza spika janja ya kwanza barani Afrika inayoweza kutumiwa bila kushikiliwa kwa mikono. Kifaa hicho kimeundwa ili kutoshea katika maeneo mbalimbali ya nyumbani, kikiwa na lengo la kuifanya kila nyumba barani Afrika kuwa nyumba janja (smart home).

Mbali na hayo anamiliki SomaApp inayowezesha usomaji kwa njia ya mtandao.

Asili yake haijulikani kwa uhakika lakini watu wenye majina yafananayo aliwahi kuwepo Mnyamwezi aliekuwa nahodha wa kwanza wa timu ya Taifa ya Tanganyika ya mpira wa miguu, Yunge Mwanasali, Mtoto wa Mtemi MWANASALI / MWANSALI (Masunga Sali) wa USONGO,
 
Nyuzi kuhusu huyo mtu inatosha aise kwa leo
Kenya watakuwa wanajiona watu wa maana sana mnavyomake big issue out of this

Mnamtrendisha as if anakuja kuiondoa CCM madarakani aise

Wewe tuliza basi hayo matobo Yako.

Hapo ulipo UTI zimekujaa mwili mzima na maziwa yamekushuka kwa kunyonyesha vibabu. biKra za matundu yote huna, kazi kuiwaza CCM Tu.

Hapo ulipo NJAA NI KALI SANA na picha Yako fake hiyo wakati una sura ya BABA

Hebu tupishe huko
 
Wewe tuliza basi hayo matobo Yako.

Hapo ulipo UTI zimekujaa mwili mzima na maziwa yamekushuka kwa kunyonyesha vibabu. biKra za matundu yote huna, kazi kuiwaza CCM Tu.

Hapo ulipo NJAA NI KALI SANA na picha Yako fake hiyo wakati una sura ya BABA

Hebu tupishe huko
Tutumie busara na hekima kwa yote tuyanenayo.
 
Back
Top Bottom