Nashukuru sana kuliona hilo mkuu, your alias name (Gombesugu) limenikumbusha enzi zangu pale Minaki nikiwa na rafiki yangu Kambangwa akitufundisha kucheza/piga ngoma za Mwaneromango na Kazimzumbwi. Karibu sana mkuu.
Haina neno ndugu yangu tuko pamoja!
Umenichekesha hizo enzi zako za hilo
Gombesugu kule Minaki!ahahaa!!
Nafikiri siku hizi hata hiyo
Minaki itakua iko taabani si kama hizo enzi zenu!?
Mzee wangu katika vitu alivyokua anavichukia na kuvidharau hakuna kama vile ngoma za ndugu zetu wa
Kizaramo!?ahahaa!!
Lakini mimi nimetumia hiyo alias ya
Gombesugu ili kuthamini flexibility,ukarimu na fadhila za hao ndugu zetu wa
Kizaramo,
Washomvi,Wandengereko,Wanyagatwa,Wakwere na wengineo...kwa kukaribisha
Watanzania woote katika huo mji wao mzuri mno wa
D'salaam/Mzizima bila ya kujali matabaka,kabila,rangi,udini na mengineo!
Inachosikitisha ni yakuwa nyingi ya comments humu
Jf...utaona baadhi ya jamaa wengi tu wanaojiita ati ni
"wasomi" lakini inapokuja masuala ya hawa ndugu zetu
Wazaramo/Watu wa Pwani, utaona ghafla mtu anashindwa kujizuia na
chuki zake za kikabila alokujanazo/alohamia nazo hapo
D'salaam zinaanza kumtoka na kutoa kashfa na kejeli nyingi tu kwa ndugu zetu hao!?
Mfano utasikia mtu anadai ati
Wazaramo ni wendawazimu,hawataki kusoma,hawajui kusoma wala kuandika na mengineyo mengi tu!? Lakini
"msomi" huyohuyo anashindwa kutazama majambo au
history katika ile
broader perspective!
Nashukuru tumezungumza leo japo kiduchu na tuko pamoja ndugu yangu.
Nakutakia siku njema.
Ahsanta.