Hakuna mtu kasema wapigania uhuru wa kiislamu wanataka KULIPWA!!
HAPA SUALA NI KUWATAMBUA NA KUWAPA HESHIMA ZAO KM HUYO NYERERE NA WENGINE!
Kila mara tumeskia fulani shujaa fulani alikuwa mstari wa mbele bla bla bla bla!
Na mara zooote wanaotajwa humo ni WAGALATIA TUPU!! Huku ni kuonyesha namna gani HILI TAIFA LINA UBAGUZI WA KIDINI VIBAYA!Na wanao uanzisha udini huo ni NYIE NYIE WAGALATIA NA KAMWE SIO WAISLAMU.
Nasubiri jibu!.
Pengine sijaelewa vema. Lengo ni lipi kati ya haya?.
1. Kutaka hao wanaodaiwa kusahaulika watambuliwe mchango wao katika upatikanaji wa uhuru
wa Tanganyika kama mtu mmoja mmoja kadiri ya michango yao?.
2. Inatakiwa watambuliwe kama ''Waislamu waliochangia upatikanaji wa uhuru?''
3. Waliochangia kupatikana uhuru ni watu binafsi au ni Uislam?.
Ninavyofahamu mimi swala la kupigania uhuru halikuwa la mtu mmoja wala kikundi fulani,
limeshirikisha watu na vikundi vingi sana. Wengi tuliowasoma kama akina Kawawa, Titi,
Julius, Kambona na wengine wengi ni viongozi tu lakini nyuma yao kulikuwa na watu wengi sana
wenye vipato tofauti tofauti na kila mmoja alitoa mchango mkubwa kulingana na kipato chake.
Muuza karanga akichangia sh 500, thamani yake ni sawa au pengine ni zaidi ya aliyetoa 500,000
lakini mwenye kipato 5,000,000.
Kila mtu au kikundi kilichoshiriki harakati hizo tuzo kubwa kuliko zote ni upatikanaji wa
uhuru japo ni wa bendera tu, lakini kwa kiasi walifanikiwa malengo yao. Sidhani kama lengo
lao mojawapo lilikuwa ni kutaka wasifiwe au au watambuliwe kwa imani zao au imani yao itambuliwe.
Waliotaka imani yao itambuliwe walianzisha chama cha kupigania hilo kwa mujibu wa sheria za
wakati huo.
Hata siku zijazo historia pengine itasomeka viongozi wa sasa wamejenga nchi, lakini ki-uhalisia ni
ni wananchi wa kawaida ambao wanalipa kodi na kufanya kazi usiku na mchana ndio wanaojenga nchi.
Kwa vile hao viongozi ndio wamesimama mbele na ndio wanaonekana na wengi kitaifa na kimataifa,
basi watakuwa wawakilishi wa walipa kodi wengi ambao ndio msingi wa ujenzi wa nchi.
Maoni yangu:
Kama Malengo ya hao waliosahalika yalikuwa ni kupigania maslahi ya waislamu
ni rahisi kuhisi ni kwa nini walipotea baada ya uhuru. Baada ya uhuru vita kubwa
ilihamia kupambana na ubaguzi wa kidini, kikabila, rangi, kupambana rushwa,ujinga,
maradhi na umaskini. Mtu yeyote aliyetaka kueneza hayo badala ya kuyatokomeza
aligeuka kuwa adui wa Taifa bila kujali imani yake ya kidini.
Pengine aliyeleta mtungo huu ataleta sababu pia kutoka kitabu hicho kueleza
sababu za watu hao mashuhuri kuachwa.
Naamini si kwa sababu ni waislamu bali sababu nyingine ambazo hazikuwekwa
wazi, pengine kwa makusudi ili kuepusha migongano isiyo na tija.
Naamini hivyo kwa sababu wapo waislamu wengi ambao wameshiriki katika
uongozi na kujenga misingi muhimu ya Taifa hili ambayo sasa tunaibomoa.
Ingekuwa tatizo ni ''Uislamu'' leo hii tusingesikia chochote kuhusu Titi, Kawawa n.k
Tusingekuwa na mitaa yenye majina ya viongozi waasisi wa Taifa waliokuwa
wanafuata imani ya ki-islam kama mojawapo ya historia ya michango yao kwa taifa.
JIBU:
Nyerere na wengine wote hawakutambuliwa kwa dini na imani zao, bali kama watu binafsi.
Hoja hii ingeonekana ya maana na pengine ingeungwa mkono na wengi kama ingejikita kuwafahamisha watanzania michango ya watu mbalimbali ambao hawajulikani katika historia ya sasa.
Suala la kuandika historia sio la siku moja ni swala endelevu.
Kutumia udini katika kujenga hoja kunaifanya hoja nzima kuonekana haina maana hata kama
lengo halisi lilikuwa jema.