Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mzee MS,
Aslaam aleykum na kisha shikamoo ndugu yangu habari muda mrefu.
Ukisoma nilichomjibu nnguu utagundua namwambia jambo jepesi sana. binadamu kukataa kutawaliwa na kudhulumiwa ni katika FITRA aliyotupa Allah SWT. Kwa fitra hiyo ndio maana Che Guevara (sio Muislam) akaja Kongo kupigana na wabelgiji. Mahtma Ghandi aliitumia kupambana na waingereza. Hapondipo nilipoanzia.
Kanisa katoliki tofauti na uislamu ni taasisi ambayo imefaidika na kutegemea sana dola tawala. Hiyo ipo katika historia ya kanisa lenyewe. Desturi hii haijaisha na ndio maana kanisa katoliki ni dhebu pekee lilijitalia kiti cha hadhi ya namna fulani UN. Wewe unasema masuala ya masheikh wa Ruvuma, nakukaribisha kuchunguza lengo halisi la Mussolini kuivamia Ethiopia 1935 na idadi ya waethiopia waliokufa pale majeshi ya kiitalia yakihaha kuitafuta "arc of the covenant" ambayo kuna hisia kubwa sana kuwa ilikwenda Abyssinia wakati wa mwiso mwisho wa utawala Solomon. Search (Ethiopia, arch of covenant, Musolini).
Kujibu swali lako halisi ni kwamba kanisa kama taasisi iliyokuja na kufaidika na utawala wa kikoloni haikutegemewa ligeuke na kuongoza mapambano dhidi ya mkoloni. Mimi nashauri tusilichimbe sana hili kwa vile hata masheikh wetu nao hawakufanya jitihada zisizo na shaka kutokomeza utumwa katika hii ardhi yetu japo waliuona na hata hao wachuuzi waliswali nao, lakini wazee wetu waliuzwa mbele yao. Badala yake tunakuja kuona mtu kama sultani wa zenj analazimishwa na waingereza kuweka saini ya kuridhia kusimamisha biashara ya utumwa kwenye eneo lake.
Hapa Mzee MS lazima tutenge kati ya sera za taasisi za dini kama Kanisa au misikiti na Watanganyika wakiristo au waislamu waliokuwa pia na moyo wa uzalendo na uchungu na nchi yao itakuwa vibaya tukiwachanganya.
Umesema nashangaa waislamu kuijenga TANU. Hapana. Nilishangaa waislamu kutotoka TANU kama BLOCK ili kui-support AMNUT. Hili jambo linaashiria kulikuwa mgawanyiko mkubwa katika waislamu wengine wakilitazama jambo zima kama waislamu na wengine wakilitazama jambo hilo hilo kama wazalendo na tofauti zingaliko hadi leo. Kuna waislamu hawachelewi kuwaita hadi kuwaua wenzao kuwa ni MAKAFIRI kwa vile suruali inagusa viatu na wengine wanatoa talaka wakijua mke kakubali kuhesabiwa.
Umeniuliza mbona maaskofu hawamo katika historia hii. Hii inalingana kama masheikh wetu walivyo wachache kwenye kukemea utumwa Pangani au Zenj enzi hizo. Hawa ni watu mwisho wa siku wanatawaliwa sana na maslahi yao. Nadhani nimeshakujibu. Nitashukuru kama paper yako iko online unipe link niisome nahisi ina mambo mengi mazuri.
Mawazo ya Nguruvi ya kuwaenzi watu kama kina Bibi titi kwenye baadhi ya hizi taasisi nadhani sio mabaya jaribu kulifuatilia.
Wickama,
Nitakujibu moja tu.
Waislam si wabaguzi.
Ubaguzi unapigwa vita na Uislam.
AMNUT ilikuwa na historia ya kuanzishwa kwake.
Ikiwa huijui soma kitabu changu.
TANU kilikuwa chama cha Waislam na ndiyo waliokiasisi
wakakipa viongozi na wanachama.
Hayo mengine ukitaka majibu lete uzi wake hapa ''we are
keeping our eyes on the ball.''