Mkuu umejieleza vizuri sana, kinacho nishangaza mimi ni baadhi ya Wazalendo wenzetu kuchukulia kimzaa mzaa mambo ambayo yanaweza kabisa kusambalatisha Taifa letu - Katiba yetu inasema Serikali haina DINI, hapo hapo baadhi ya madhebu yanawekwa kwenye a hermitically sealed container wasifurukute - Serikali inafikia hatua ya ku-appoint viongozi wa dini!!! Ni mtu gani mwenye akili timamu anaweza kukubaliana na udikteita huu uliyo kubuhu - waislaam wakilalamika mnasema ni wabaya!!! Kama Serikali ya awamu ya kwanza iliweza kufanya vitu vya kukihuka haki za binadamu kwa kuingilia unnecessarily uendeshaji wa madhehebu hayo, mpaka Serikali inafikia kuchukua such drastic steps ili iwa-contain kwa nini tushangae anacho lalamikia MS, kusema kweli inaonekana wazi wazi kwamba operation hiyo haikuishia kuwachagulia viongozi wa dini tu, bali ilikwenda mbali zaidi kwa kufuta kutoka kwenye historia majina yanayo randana na dini yao, I have no doubt in my mind kwamba it was a well Organised scheme.Naona hapa baadhi ya Wazalendo wanatoa an impression kwamba MS anatetea Uislaam!! Hii si kweli na hilo wanalijua fika, MS anacho pigania hapa ni kuhusu kuandika historia ya kweli ya Taifa letu bila ya ku-arase majina ya wazalendo ambao Viongozi wetu walikuwa na bifu nao, na ukiangalia kwenye machapisho ya Mkuu MS utakuta ameweka majina ya wapiganaji wa dini zote mpaka ya wapagani, mbona suala zima liko wazi kabisa lakini members hilo hawalisemi. Watu wanazungumza mengi humu ya kupoteza lengo, lakini hakuna hata mmoja amawahi kuhoji ni kwa nini Serikali ya hawamu ya kwanza ilikuwa hell bent kusambaratisha organisations za kidini na za wafanyakazi zilizo play a big role kuwaodoa wakoloni wakishirikiana na chama cha TANU!! Sina shaka kwamba nguvu za makundi hayo yalionekana yatakuwa tishio kwa Serikali ya awamu ya kwanza siku za usoni - hii ndio ilikuwa sababu ya msingi ya Serikali kuanzisha BAKWATA na NUTA ili makundi ya awali yavunjwe nguvu - tuwe wakweli hapa. Naona ma-stalwart na mashabeki wa Serikali ya awamu ya kwanza wanajifanya kulisahau hilo na hawataki kuambiwa ukweli. Tukiwa wawazi tutalinusuru Taifa letu, kama Kambarage aliwahi kukili mwenyewe kwamba kuna baadhi ya vitu walifanya ambavyo vilikuwa havifahi - kwa nini wengi wetu tunakuwa na kigugumizi cha kukemea mambo ambayo haya tufahi, yanonekana wazi wazi yana kila dalili za kuvuruga Taifa letu - God forbid.Narudia kusema kwamba, tunacho sahau ni kwamba si rahisi kunyanyasa na kubeza beza kudi fulani la kidini 4ever, alafu mkategemea nyinyi mtabaki salama miaka yote - hilo amulioni!!! Ubishi bushi tu bila ya kutafakali mambo kiundani - hakuna anayejiuliza ni kitu gani kilifanya kundi la Boko-Haram kuhibuka North Nigeria au unafikiri Tanzania is an Island hawawezi kufanya kweli wakiamua - tunajitia ujuaji tu.JF ni barometer tosha ya kuonyesha mambo si shwali kidini-wise katika Taifa letu, jaribu kuangalia members wanavyo jibizana jibizana with emotions kuhusu mambo ya dini hata sehemu ambazo si mahali pake waitibukiza tu, kwa bahati mbaya sisi Wakristo ndio tunaongoza kubeza beza sana wenzetu, tunawasema mambo chungu mzima, kwani hata wakiswali mara elfu kumi kwa siku sisi inatuhusu nini - they know better wanacho kitaka katika maisha yao, Dini yao na Mungu wao.