Mohamed bado hujajibu hoja zangu hata kwa bahati mbaya.
Nimeuliza iweje Kirinjiko ifanye vizuri kuliko Masjid Quba.
Iweje Kilimanjaro na Bukoba ziwe katika hali tofauti na Mtwara na Lindi katika mazingira yale yale.
Suala la kujiunga na OIC halina uhusiano na elimu. Haya ni mambo ya kuzua tu.
OIC haitoe elimu wala mwalimu Mkuranga.
Ni wajibu wa wananchi kuibana serikali yao kuhakikisha ubora wa elimu. Hakuna nchi iliyowahi kupelekewa mwalimu wa sekondari na OIC. Ni kichekesho Mohamed achana na hoja za namna hii, zinatia aibu.
Kujenga chuo kikuu cha mwaka 1968 kupitia EAMWS ni suala la waislam.
Wanaouziana kiwanja hicho leo hii na kupigana Nyerere akiwa kaburini ni waislam.
Miaka 28 tangu Nyerere aondoke madarakani hakuna kitu kilichofanyika ku reflect yale yaliokuwa yafanyike mwaka 1968. Nimewahi kukuliza nini kinatokea na chuo cha Morogoro? Huna jibu unatafuta sababu laini.
Mohamed huwezi kulalamika kuhusu chuo kikuu wakati umeshindwa kupeleka mwalimu Mkuranga. White elephant!You must have a solid foundation ili kuwa na stable structure. Huwezi kuaminisha umma kuhusu chuo kikuu wakati una shule ya wanafunzi 250 na walimu 2. Unapata wapi wanafunzi wa chuo kikuu kama huna wa msingi na sekondari! hivi huoni kuna kicheko hapa Mzee Said.
Huko Nyuma ilisemekana Nyerere alihujumu kupitia NECTA. Sasa hivi inasemekana ni NECTA na wala si JK au Kawambwa.Pathetic! Mohamed anayesimamia na kuteua wajumbe wa NECTA ni JK kwa kushirikiana na Kawamba.Kama kuna tatizo lielekezwe huko na si kutafuta imani fulani kwa chuki tu.
Nimeshangaa majuzi watu wakisema hawana tatizo na wizara, tatizo lao ni NECTA.Yaani hawana tatizo na chanzo wana tatizo na matokeo. Kama tatizo la NECTA lipo basi limeanzia kwa Kawambwa na JK.
Ndalichako ni mteuliwa wa Rais JK. Kwa tatizo mtu wa kuulizwa ni JK. Ndalichako ni mhadhiri, kuteuliwa kwake ni kutokana na taaluma na sifa zake kielimu.
Hiyo imedhihirika baada ya kuteuliwa kuwa rais wa shirika la mabaraza ya mitihani Afrika kama sikosei.
Hana sababu za kuhujumu kwasababu hakujichagua aliteuliwa na alikuwa na kazi yake. Sijui na uhadhiri nao anafanya hujuma Anaishi maisha mazuri bila kuwa mkurugenzi na anahitajika popote duniani.
Sijui kuwekwa kwa mtu mwingine kutaleta mabadiliko yoyote. Kufeli hakuna uhusiano na NECTA.
Wakati wa Ndalichako Kirinjiko na Feza zimefanya vema sana. Sijui kwanini hazikuhujumiwa.
Tatizo la Mohamed ni kuandika kwa lugha tamu bila kufanya hata chembe ya utafiti achilia mbali fikra.
Kwavile lengo ni kuchonganisha watu atatafuta sababu za kuunga unga ilimradi apate ulua na mradi wake.
Mohamed angetembelea shule ya Ali Hassan Mwinyi akaona wanafunzi 250 wanfundishwa na walimu 2 asingeweza kuja mbele ya umma kwa flimpsy and unsubstantiated allegation kama hizi.
OMG! afadhali mimi ni kauzu maana naona Nyangumi hawana macho
Kuna mtu kaonyesha hapo juu jinsi shule zinavyofaulisha na kufelisha. Lau Mohamed angeamua kutua mzigo wa chuki kwa dakika kadhaa akapitia matokeo ya mitahani ya shule kwa kidato cha 4 na 6 asingeweza kuandika haya.
Na rudia kusema Mohamed uwezo wake wa kujenga hoja kwa mantiki ni mdogo sana.
Hili Mohamed ulikubali, ni mdogo sana kiasi kwamba madai yako yanakosa mashiko achilia mbali mantiki.
Mohamed kuendelea kuipumbuza jamii hakusaidiii kitu.Hakuna fundi umeme au magari anayepatikana kwa jina, ukoo, kabila au dini. Hakuna mwanasheria, engineer au mhasibu na Daktari anayepatikana kwa kuteuliwa.
Kinachotakiwa ni shule na si shule tu kama majengio ni shule kwa maana ya shule.
Mwapachu alipelekea watoto shule na sasa inajirudia. Mshume Kiyate hakufanya hivyo na historia inasema hilo.
Tofauti ya familia mbili inatokana na 'ukatili wa Nyerere' real!
Mohamed ukipanda maharage utavuna maharage.Wenzako wakipanda mahindi wewe ukiwa unapiga hadithi basi ipo siku utavuna mabua.Acha kabisa kuipotosha jamii. Nasikitika sana kuona unakusudia kuiskuma jamii porini.
Mradi wa Darul islam wa Kibaha ulikuwepo kuanzia wakati wa Mwinyi. Kiwanja kilitolewa na upo ushahidi usio na shaka wafadhili waliondoka na kwenda Mbale Uganda kwasababu pesa zilikuwa zinatafunwa na kamati za waislam wenyewe.
Nyerere hakuwepo wakati huo na serikali ilikuwa ya Mwinyi. Huu ukweli unautafutia sababu za ajabu sana. Hebu kuwa mkweli kwasababu hakuna fadhila kwa kusema uongo hata kama ni upande wa dini.
Kuna kiongozi analalamika kuhusu madhila haya unayosema. Kiongozi huyo hajawahi kukaa katika chumba kinachoitwa darasa. Huyu kiongozi hakukaa darasani lakini ni bingwa wa kueleza hujuma za elimu.
Ni kituko kwakweli. Ni sawa na mtu akuelezee ugumu wa Biology wakati hakuwahi kusoma hata siku moja.
Acheni haya watu wakae chini wapime wanapambana vipi na dunia ya ushindani. Watu wanaandaa vipi watoto kwa siku za usoni. Mwapachu hakuishia kuandika tu alipeleka watoto shule. Wenzangu mimi wanadai majina ya mitaa ya barabara. Hadithi itakuwa hiyo hiyo kama watu wataendelea kuamini utunzi wa hadithi za kufikirika.
.Inasikitisha sana.
Nguruvi,
Unajua sababu ya serikali kuichukia Quba?
Unaijua historia yake?
Hebu soma hii hapa chini:
''Warsha responded to these accusations by distributing leaflets to these areas
explaining position on the future of Islam in Tanzania and made Muslims be aware
of their activities in trying to liberate Muslims.
The government and BAKWATA could not match Warsha's truth with their propaganda.
Muslims were sympathetic to Warsha and took Warsha's struggle as their own struggle.
Muslims helped Warsha to establish a school
Masjid Quba and Islamic Centre which was
owned and managed by them.
In retaliation to these efforts the government refused to register the school.
The school was perceived by the government as a centre of "Muslim fundamentalism."
The government went further to subvert the school by warning Muslim parents that
students completing their education at Masjid Quba would not be recognised by it and
would not be considered for further education or for employment.
Warsha was not to be deterred they decided to run the school and educate Muslim
children even without government registration.
Members of Warsha used to say that they have their consent from
Allah; they don't
need any permission from anyone.
This was Warsha's motto.
The school remained blacklisted by the government until 1988 when Prof.
Malima as the first Muslim Minister of Education registered it.''
Hii ndiyo sababu Shule ya Masjid Quba inapigwa vita hadi leo kuanzia
Nguruvi,
NECTA na serikali yenyewe.
Nguruvi,
Hujui kitu.
Fedha za ile shule ya Kibaha ndiyo iliyojenga chuo kikuu Tunguu Zanzibar.
Mzee Jumbe alipoelezwa kuwa serikali ya Tanzania Bara haitaki Darul Imaan iwasaidie
Waislam wa Tanzania Bara yeye akaingilia hilo suala na kuwaomba wauhamishie huo
mradi Zanzibar.
Hatukutaka lile lililotokea katika mradi wa kujenga chuo wa OIC serikali ukaupiga vita
ujirudie tena katika mradi huu kwa kuwa Darul Iman walikuwa wanataka kuuhamisha mradi
huu kwenda Somalia;
Na wazo la kutaka mradi ubadilishwe na sasa kijengwe chuo kikuu badala ya shule ya seokondari
ilitoka kwa vijana wa Kiislam Bara.
Inawezekana sana hawa vijana walikuwa vijana wa Warsha.
Ati fedha zilililiwa.
Huna moja ulijualo Bwana Nguruvi.
Waislam wa macho sana.