CattleRustler
JF-Expert Member
- Oct 26, 2013
- 1,055
- 467
Mohamed Said
Nimejaribu kukumbusha kuwa hawa vijana wanapokwenda si pazuri jaribu kuwarudisha katika mstari.
Ingawa nimeambiwa nakimbilia kulia kwako mimi sitasita kusema kwasababu huenda wanakusikia vema.
Imefika mahali ni kashfa za dini, na cha kusitikitisha kashfa hizo zimeaanza kuwarudi wenyewe.
Namsoma Khataan akiwatukana mashia kwa vilemba na majina kama Khomeni.
Huko nyuma ni vijana hawa hawa wamesema hakuna anayeruhusiwa umuondoa mtu katika Uislam wake.
Wakasema hata Bakwata ni waislam na hakuna anayeweza kuwaondoa huko.
Sasa inakuwaje hawa kina Khataan wanaanza kuwaondoa Shia katika Uislam?je si double standard
Pili, khataan kasema huu ni mnaksha wa kisiasa si wa kidini.
Lakini ni Khataan huyo huyo ametumia dini kuwatukana watu wa imani zingine.
Sasa Mzee Said hapa kweli kuna linaloeleweka?
Labda utufahamishe inakuwaje huu mnakasha unakuwa wa kisiasa kwa nyakati fulani na wa dini za kutukana imani nyingine na hata madhehebu mengine kwa wakati mwingine.
Tatu, kama Khataan anaona mama Aisha kutukanwa inamuuma sana vipi ana hisi maumivu ya donda la kuwatukana wakristo? Je Khataan haoni maumivu ya donda hilo ndiyo maumivu ya matusi yake kwa Wakristo?
Na ni wapi kwa mujibu wa imani imeruhusiwa kutukana watu wa imani nyingine?
Wapi imeelezwa kuwa tusi kwa mama Aisha ni baya zaidi kuliko tusi kwa mtu mwingine au nabii mwingine?
Mzee Said je hapa huoni vijana wamepindukia na sasa imefikia mahali wanazungumza hata kisicho cha dini na je huo si uhalifu!
Nguruvi3,
Tatizo ni title kwa ujumla inayoongelea mchango waislam kama vile uislamu ni dini moja. Angalau angesema mchango wa watu wa coast ingekuwa sawa. Uislamu si dini moja kuna mapingano mabaya sana ndani ya uislam. Kuna sheikh moja syria juzi tu kasema Shia ni makafiri kuliko wakristo na jews. Na japo shia hawaongeagi kuusu vitu wanavyo pinga kuusu sunni ina ukifuatilia utajua wanavyo wachukia sunni. Angalia tu jinsi iran wanavyoathimisha ashura(siku imam hussein aliyouliwa)kwa kujipiga bakora mgongoni na kuanza kulia. Mfano mwingine ni Sheikh Yaser Al-Habib na mpango wake wa kusherehekea siku aliyokufa Aisha(mke wa muhammad).
Hafazali ukabila kuliko udini
Last edited by a moderator: