Yani umechanganya utumbo na dagaa dooh!Kama ni ardhi mbona hatuoni nchi za kiarabu zikipigania nchi ya Sakata magharibi ili ipate uhuru? Mbona wakrudi wanaodai ardhi yao nchini Turkey, Syria, Iraq, Iran mbona hawapewi nchi yao ya Kurdstan? Mgogoro wa Israel vs Palestina ni dini ya kiislamu na kiyahudi, mbona hatukuona kule Darful waarabu wanawapigania watu wa Darfull>
-Suala la Palestina na Israel ni ardhi sio dini,kwasababu hadi makanisa pia yamevunjwa na Israel kufanya upanuzi wa Israel ndani ya ardhi ya Palestina na ukitaka ushahidi tunakupa.Tokea kabla ya 1947 Jerusalem kumepiganwa mapigano tofauti ya kugombea ardhi baina ya wayahudi na waarabu.
-Wakurdi ni kabila ambalo linataka kuanzisha taifa lake lenyewe la kikabila,ni sawa WAARUSHA AU WAMERU watake kuanzisha taifa la kabila lao na wajitenge na Tanzania.Kama kiongozi wewe utakubali?
Ndio maana unaona wanavamia Uturuki,Syria na Iraq,Yani hawana specific target ilimradi popote waanzishe taifa.
Sasa ni kiongozi gani ataruhusu taifa la ukabila na alete mpasuko katika taifa!?
-Darfur ni vita ya RSF na jeshi kuu la Sudan kugombania utawala.
Mukae mtafute vyanzo sio kuongea tu.Hapo Palestina wakristo wenzako wanauawa kwa mabomu na sniper na mpaka makanisa kule Jenin yamevunjwa kupisha upanuzi wa makazi ya Wazayuni.