Hamas walilijuwa hilo mapema sana, wakasema tuitumie fursa hii vilivyo, kwani kama hatukuitumia wanatuuwa kila siku na tukiitumia watatuuwa vilevile. Wakaamuwa waitumie "to the maximum". Ndicho walichokifanya.
Hapo walioingia chaka Wayahudi, walifikiri hamas watapeleka mtu mmoja au wawili wakajitowe mhanga. Kinyume na mpango wao wayahudi wakashushiwa moto walioshushiwa moto wa vimondo vya tabata wasioutegemea.
Wapalestiina wameshasema sasa hawaachiihili mpaka waishe wote au myahudi arudishe arshi yao.
Hapa sasa ni nani tu atayekuwa na uvumilivu wa machungu zaidi? Yule aliyezowea starehe na ushoga au yule aliyezowea kuteseka toka anazaliwa?
Nilipoyaandika hayo hapo juu mwaka jana na majibu yaliyokuwa yanaletwa kwenye huu uzi nikafahamu kuwa wengi hawaelewi dunia inakwenda vipi.
Leo naendeleza:
Kanali wa jeshi la Marekani, Jasusi Mbobevu na mkaguzi wa silaha za maangamizi huko mashariki ya kati, ukimfatilia cha nnel yake (naweka link chini hapa) utakuta kuwa niliyoyaandika ndiyo anayayakinisha sasa hivi na anaongezea kwa kusema, Mossad walidhani wamewaingiza chaka Wakubwa wa Wapalestina kwa kuwatubuni kwa [pesa nyingi na kuwa wapo nao na wakapanga nao pamoja uvamizi, kwa bahati nzuri au mbaya, kumbe siku zote wale wakubwa wa wa Hamas walikuwa wanajuwa wanachokifanya na wakawa wanatumia pesa hizo na wanaitumia Israel (kama wapo nao vile) ili kupitisha pesa nyimgi sana kutoka kwa wahisani kupitia Israel, wahisani ni pamoja na nchi zote za Kiarabu zenye mahusiano na Israel, ikiwemo Saudi Arabia, UAE, Qatar na wengineo.
Hamas wakawa wanazutumia pesa hizo kufanya maandalizi makubwa ya kujenga "under ground metro", Wayahudi walikuwa wanaelewa kuwa yanachimbwa mahandaki ya kawaida kama yaliopo kwao ya kukimbizia raia wakati wa mashambulizi. Kumbe Hamas wanajenga mji kabisa wenye vichochoiro, vyumba, viwanda na kila kitu kinachohitajika kijeshi, chini kwa chini.
Lile shambulio la & Oktoba lilikuwa lifanyike siku nyingi lakaini majasusi wa Hamas ambao ni hao hao wakubwa wa Hamas walikuwa wanawazuia mazayuni kuwa lisifanyike sasa mpaka tutakapowapa go ahead.
Ilikuwa lifamyike shambilizi dogo na Hamas wawe hawajitayarisha ili israel waingie kama wanaenda sokoni vile na kuikalia Ghaza. Kumbe wameingizwa chaka.
Siku ilipofika Israel walikuwa wanajuwa kikundi kidogo cha Hamas wataingia watachukuwa mateka wenye kijiji cha karibu na hicho ndiyo chambo cha mazayuni kuingia na kuikalia Ghaza.
Hamas kumbe wamejitarisha mara elfu ya mazayuni walivyofikiri, kimbembe chake waote tulishuhudia.
Na hapo walipo sasa hivi ni Hams ndivyo walivyotaka, mipango ilisukwa ikasukika, hii siyo bahati mbaya.
Msikilize jasusi mbobevu Scott Ritter anavyochambuwa:
View: https://youtu.be/LJxvLhJqpR0?si=7fRaLa51UC8mmVCh